Mtaji kidogo kwa aliekosa kazi unapatikana

Kwa majina naitwa Joshua chuwa...nipo moshi...Ifuatayo ni Biashara ya kilimo nayoenda kuifanya na nadhani itanipa matokeo chanya ndani ya mda mfupi...mchanganuo ni kama ifuatavyo...
KILIMO CHA NYANYA

Ndio, kilimo cha nyanya. Kujikita katika kulima nyanya na kuwa na uhakika wa kupata soko. Nyanya inastawi katika maeneo mengi nchini hivyo ukilima katika eneo ulilopo unaweza kupata mavuno mengi. Kilimo cha nyanya kinawatajirisha watu wengi, hilo nimejiridhisha nalo sina wasiwasi.

Najishauri nianze kulima nyanya mwezi huu wa Septemba ili kufikia mwezi wa kumi na mbili ninze kuvuna na kupata million tano yangu kama full estimation niliyojiwekea kutokana na mchanganuo wa kina.

Mimi nitaamua kulima nyanya; nitaanza na maandalizi ya awali ambayo yakikamilika ikiwa ni pamoja na kuandaa shamba la ekari moja, kusia mbegu za nyanya na kutafuta mbolea ya samadi, yote hayo nitafanya kwa uweledi ili tukija kukutana Mwezi Disemba Nikuonyeshe Milioni Tano Yangu
Sitaki kusema maneno mengi, ufuatao ni mchanganuo wa kilimo cha nyanya ninacholima mimi. Unaweza kuandaa wa kwako utakapo anza kulima.


KILIMO CHA NYANYA

Awamu ya Kwanza: Septemba 2015

S/No Mahitaji Idadi/Kiasi Gharama Jumla

1. Kulima shamba Ekari 1 40,000/=

2. Kuandaa matuta Ekari 1 50,000/=

Jumla ya gharama zote za kuandaa shamba 90,000/=

3. Kununua mbegu Packet 4 28,000/=

4. Kuandaa kitalu cha kusia

mbegu na kumwagilia

mbegu 5m2 10,000/=

Jumla ya maandalizi ya mbegu 28,000/=

5. Kupanda miche shambani Ekari 1 50,000/=

6. Mbolea ya samadi Trip 5 25,000/=

7. Kununua jenereta 1 500,000/=

8. Kumwagilia (mafuta) Mara 10 250,000/=

9. Kupalilia Mara 2 20,000/=

Jumla ndogo 845,000/=

10. Mbolea ya kuzalishia (CAN) Kilo 10 50,000/=

11. Madawa ya kutibu magonjwa ya nyanya 40,000/=

12. Kuvuna mara 4 100,000/=

Jumla ndogo 190,000/=


JUMLA YA GHARAMA ZOTE 1,163,000/=

Mavuno ya nyanya kwa ekari moja ikitunzwa vizuri yanaweza kufikia tani arobaini (40) sawa na madebe 2,200 ya lita ishirini. Lakini kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, magonjwa na sababu nyingine, kiwango cha chini cha kuvuna nimeweka tani kumi na nane (18) sawa na madebe 1000 ya lita ishirini.


Debe moja la nyanya hapa Bariadi linauzwa kwa Tsh 10,000/=. Labda kutokana na mabadiliko ya bei sokoni, bei ya chini ninayoweza kuuzia iwe Tsh 8,000/= kwa debe.


Nitavuna jumla ya madebe 1,000 na kila debe nitauza kwa Tsh 8,000/=, nitapata jumla ya Tsh milioni nane 8,000,000/=.


Jumla ya mauzo yote 8,000,000/=

Jumla ya gharama zote 1,163,000/=

Jumla Ya Faida nitakayopata 6,837,000/=


JUMLA YA FAIDA NITAKAYOPATA KWENYE MRADI HUU AWAMU YA KWANZA NI TSH 6,837,000/=
Mkuu ulifanikiwa? Upo bariadi sehemu gani?
 
Nilikuwa Nikilifikiria wazo kama lako ila kwa namna tofauti na nilianza kulifanyia kazi. Niliamua kutoa ajira kwa vijana walio na moyo wa kufanya kazi na nikaanza na vijana 7, mpaka sasa nimewasaidia vijana kama 80 kwa kupitia channel mbalimbali za shughuli zangu.
 
Back
Top Bottom