Mtaje aliyeua Mchina upate milioni 5/-

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125
JESHI la Polisi nchini limetangaza zawadi ya Sh milioni 5 kwa atakayewezesha kukamatwa kwa watuhumiwa waliohusika na mauaji ya raia wa China, Zhang Hongfa (23), ambaye alikuwa mhandisi wa kampuni ya ujenzi wa miundombinu ya maji safi mkoani Pwani.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani, Absalom Mwakyoma, ametangaza zawadi leo alipozungumza waandishi wa habari ofisini kwake.

Kamanda Mwakyoma, amesema, fedha hizo zimetolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Saidi Mwema, kama motisha na kivutio kwa watoa taarifa.

Alisema Oktoba 17 mwaka huu, saa 1.30 usiku Kwa Mathias, wilayani hapa, kundi la majambazi wapatao kumi, wakiwa na silaha za aina mbalimbali zikiwamo shotgun, MarkIV, mapanga na marungu, walivamia kambi ya ujenzi wa miundombinu ya majisafi wilayani hapa ya kampuni ya China Hunan and Constraction na kumuua Mhandisi Hongfa.

Uchunguzi wa daktari ulionesha kuwa mtu huyo alifariki dunia baada ya kutokwa na damu nyingi katika tukio hilo ambapo raia wengine watano wa China walijeruhiwa kwa mapanga.

Waliojeruhiwa ni Huii Quan (52), Liuo Guobo (24), Huxiao Jie (28), Wu Jiano au Ping (35) na Yong Chin Jiao (23) wote wahandisi wa maji kutoka China na walipelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.

Kamanda Mwakyoma alisema kabla ya kuingia kwenye kambi hiyo majambazi hao walifyatua risasi nne angani kwa lengo la kuwatisha watu waliokuwa jirani na eneo hilo, wasisogee kwenye tukio ili waweze kupora kirahisi.

Baada ya kufyatua risasi hizo, majambazi hao waliwaweka chini ya ulinzi watumishi wote waliokuwa kwenye kambi hiyo na kupora silaha ya mlinzi wa zamu katika kibanda cha ulinzi huku askari akiwa ameiacha bila taarifa zozote.

Siku hiyo kulikuwa na walinzi watatu wa kampuni ya ulinzi ya Muungano ya Maili moja, mmoja kati yao akiwa na silaha aina ya shotgun na risasi tatu za mlinzi.

Alisema makachero wa Polisi wanawahoji walinzi wote watatu kuhusiana na tukio hilo huku likiwatafuta majambazi waliohusika.

Walinzi wanaohojiwa ni Abdallah Katema (34) ambaye alikuwa na silaha ya zamu siku ya tukio, Abdallah Moyo (45) na Asha Musa (32) wote wa Muungano.

Katika tukio lingine juzi saa 6.30 mchana kwenye barabara ya Mkuranga-Kisiju mkoani Pwani gari namba T 541 AWL aina ya Toyota Corola ikiendeshwa na mtu aliyejulikana kwa jina moja la Charles liliacha njia na kugonga mti na kuwaka moto.

Dereva na abiria, William Matola, walikufa papo hapo na abiria mwingine kujeruhiwa. Aliyejeruhiwa ni Martin Samwel (30), mkazi wa Kawe, Dar es Salaam.

Maiti wamehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam wakisubiri ndugu kuwatambua na majeruhi alipelekwa Muhimbili kwa matibabu zaidi.


http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=3942
 
Si kwamba natetea uuaji ila nina swali linalonisumbua. Hivi aliekufa angekua ni Mbongo mweusini kama Mzizimkavu, Polisi wangehangaika kuahidi zawadi kwa atakaetoa taarifa? Au kuna watu ambao ni bora kuliko wengine katika nchi hii?
 
Si kwamba natetea uuaji ila nina swali linalonisumbua. Hivi aliekufa angekua ni Mbongo mweusini kama Mzizimkavu, Polisi wangehangaika kuahidi zawadi kwa atakaetoa taarifa? Au kuna watu ambao ni bora kuliko wengine katika nchi hii?

Kwa nini Mchina? Albino kauwawa sijui kati ya jana au juzi Mwanza, hawatoa hata zawadi ya ng'ombe basi kwa atakayepeleka taarifa.
 
Kwa nini Mchina? Albino kauwawa sijui kati ya jana au juzi Mwanza, hawatoa hata zawadi ya ng'ombe basi kwa atakayepeleka taarifa.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mwanza ametoa ahadi ya zawadi ya tshs milioni 1 kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa watu waliohusika na ubazazi huo!
 
Si kwamba natetea uuaji ila nina swali linalonisumbua. Hivi aliekufa angekua ni Mbongo mweusini kama Mzizimkavu, Polisi wangehangaika kuahidi zawadi kwa atakaetoa taarifa? Au kuna watu ambao ni bora kuliko wengine katika nchi hii?

Huenda wachina wenzake wale waliokuwa wakiruka sarakasi kuwatisha manesi walipoambiwa mwenzao amekufa ndiyo wamewapa hizo 5M/- police ili watangaze zawadi kwa atakayetoa taarifa ya mauaji ya Mwenzao (think outside the box)
 
Halafu hawa polisi wasituzuge, mahambazi wote wanawajua, yani network nzima, hili changa la macho tu.
 
Ni kwa sabau ya swala zima la uwekezaji.Serikali inaogopa kuharibu reputation kwa wawekezaji wengine wa nje kwani itakuwa ni sifa mbaya.vilevile serikali itabidi ilipe gharama kubwa kwa kuwa haikuwa makini ku-guarantee security yao.ingekuwa ni mbongo amekufa wanawabembeleza wafiwa kisiasa basi yamekwisha.
 
Na ukienda kutoa taarifa we ndo unakuwa wa kwanza kuisaidia polisi, wajanaja sana hawa
 
Back
Top Bottom