mambo ndio yanaanza sasa
Nimeangali kidogo ila mtandao umeniharibia hapa so endelea kuweka update hapa.ndio hilo linaanza sasa
KGM
Nimeamka sa kumi huku bongo lakini hawajaonyesha hebu tupe muhtasari ya yaliyojiri!
KGM
Nimeamka sa kumi huku bongo lakini hawajaonyesha hebu tupe muhtasari ya yaliyojiri!
Kwa kifupi Mtagwa kaonewa, alistahili ushindi. alipigwa pigwa round za mwanzo lakini si sana. Round ya 10-12 alikuwa moto, huwezi amini. Lopez sijui kwanini hakuanguka, alimchakaza vibaya sana. Baada ya matokeo kutanganzwa ukumbi mzima ulizomea sana sana kupinga matokeo. watu wengi wanaamini mtagwa alishinda lile pambano. Kusema kweli amenifurahisha sana.
Mwanzo wa pambano aliingia huku akiwa na wapambe wakiwa wanapeperusha bendera ya TANZANIA , akielezewa na mtanganzaji kama Rogers 'Tiger' Mtagwa kutoka DODOMA-Tanzania. ameipa heshima Dodoma na Tanzania kwa ujumla