ni kweli tupu. We rejea tu mikataba ya madini na vitu kama iptl, songas, escrow, epa, richmond na mgodi wa makaa ya mawe huko mbeya( kiwira ).
Rejea namna serikali yetu inavyoendeshwa, mauaji ya ndugu zetu albino, mauaji ya vikongwe na wenye macho mekundu. Rejea migogoro ya kidini na viongozi wa kidini wanavyo-ongeleshana maneno makali hadharani.
Rejea mimba za utotoni na watoto wadogo kulazimishwa kuolewa.
Rejea mitaala yetu ya elimu kama inaendana na mazingira tuliyopo. Rejea akili za vijana wa sasa kutaka utajiri bila kutoa jasho wala kushiriki kwenye kuijenga nchi.
Rejea maneno ya viongozi wetu, kama pale kaka mkubwa alipoulizwa kwanini tanzania ni maskini na akasema hajui. Wassira aliambiwa watu wa jimbo lako wanalalamika njaa hawana chakula, akasema " mimi si mungu, siwezi kuleta mvua".
Rejea aliyesema watanzania tuna wivu wa kike na yule aliyesema tutakula majani ili ndege ya rais inunuliwe.
Rejea jinsi watoto wa viongozi wanavyonyakua madaraka kirahisi. N.k.
Hayo ni machache tu wadau, lakini yanaonyesha kuafikiana na kauli kuwa tuna iq ndogo.
Mtu mwenye iq kubwa hawezi kuruhusu :
1. Uingizwaji nchini wa bidhaa feki toka china.
2. Raia wa kigeni kufanya shughuli ambazo zinaweza kufanywa na wazawa.
3. Wageni kumiliki 100% ya uwekezaji. Ilitakiwa wazawa 51% na wageni 49%
4. Kuingiza nchini complete set ya bidhaa mfano simu, kama simu inatoka china basi battery itoke tanzania. Gari likitoka japan basi vioo na matairi vitoke tanzania na kadhalika.
5. Wala rushwa na mafisadi kuendelea kutamba bila kuchukuliwa hatua kali. Hii ina direct impact kwa kizazi cha wanaokuwa sasa as wanaona sio lazima wafanye kazi ili wapate.
6. Vijana kumaliza masomo ya juu bila kujua watafanya kazi gani.
7. Kupeleka vijana jkt en mass bila kujua wakimaliza watafanya nini?
8. Mkulima baada ya miaka 54 ya uhuru kuendelea kuteseka kwa kutegemea mvua na jembe la mkono bila masoko madhubuti.
Na mambo mengine mengi.
Unajua kuna article nilisoma, nikipata link yake nitaiweka hapa. Kwenye article hiyo wanaongelea kuhusu kupunguza population ya dunia as muda unavyokwenda resources zilizopo hazitaweza kutosheleza watu.
Of course kwenye hiyo article waliongelea kuhusu kupunguza watu kila bara kwa vita, magonjwa na mass killings kama wanavyofanya isil.
Lakini walivyofika kwa upande wa bara la africa wakasema " tons of africans have to go as there is no way those people will be able to feed themselves by 2025"
sasa angalia ukame na kukauka kwa mazao dodoma na kilimanjaro then tafakari hiyo kauli.
# watu weusi tuna safari ndefu sana. Tatizo hatutaki kulowa tope ilihali tunafanya kazi kwenye mvua#