Mtaani kwetu hakuna kabisa stori za Lissu

Mtaani kwetu hakuna kabisa stori za Lissu

Huku kwetu wanaongelea treni ya stiglers gorge
 
Kama hana madhara yoyote baada ya kufanya huo utafiti ungekaa kimya. Kitendo cha kujishughurisha
1,kuwaza juu ya Lissu
2kufanya utafiti
3,kuandika
Tayari una hofu kubwa sana,vinginevyo ungekaa kimya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanaogopa wanafikiri wewe ni mtu usiejulikana. Nao sio wajinga kama unavyodhani.
 
Hata mkuu akihutubia watu hawana habari nae wamesusa utaona siku ya kupiga Kura
Chadema wamtafute Yule ombaomba awe awe mgombea matonya vs..... wa ccm
 
Siku hizi watu hatuaminiani wenyewe kwa wenyewe, unaweza ukawa unasimlia habari za Lissu kumbe unayemsimlia ni mtu asiyejulikana, yakakukuta ya Lissu bure.
 
Wewe huwezi kuuzima moto wa Lissu na Upinzani sio Lissu tu Maalim na yeye ana mialiko kibao Zitto anaamdaa Mambo na Tishekedi ili Bandari ya Dar iwe ziara za kushtukiza kuangalia Makomtena yalioshaondoka.
Hao wanasiasa wa upinzani ni mabingwa wa udaku, ni kuwasamehe tu hasa waliponyimwa fursa kupanda majukwaani kujikweza na ahadi lukuki zisizotatua shida za maendeleo za MTz.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ukiona hivyo jua kuwa mtaani kwenu wewe tu ndiye umebakia mwaccm. Maana hata huku jf wanapandisha nyuzi zinazomhusu lissu ni wanaccm
 
Mi naishi dsm sinza mugabe huku hadi watoto wadogo wanafahamu na kufuatilia ishu zilizompata lisu yaani wanamuonea huruma ingekuwa kuna kura zinazohusisha watoto basi huku watoto wote wangempigia kura
 
Ukikuta Mtu anaongelea Siasa muda wa kazi huyo ni mvivu sio mtu wa kuwa karibu yake au kuwa Rafiki yake.


Wavivu wote chaka lao limekuwa kwenye maongezi ya Siasa, hasa Mashabiki wa Mtoto hasie thamini na mwenye kupaka matope kwao.

Ukiwa unaenda Matombo kutokea Morogoro mjini, kuna kijiji kinaitwa MTU KWAO. TL nahisi sio Mtanzania kwasababu anatudhalilisha na kutufedheesha Watanzania sana.

Be Positive

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unakaa kona bar muda wa siasa hakuna ni mbunye kuuzwa kama njugu
Toka wiki iliyopita nikiingia JamiiForums nakutana na nyuzi nyingi kuhusu Lissu na ziara zake nchi za Magharibi.

Juzi nikasema nifanye utafiti; je, wananchi wa kawaida mitaani ambao sio member wa JF wana habari zozote zinazoendelea?

Nikapita katika vijiwe vyangu (mitaa ya Ubungo na Tabata) kiukweli kabisa sijabahatika kusikia watu wakizungumza hizi habari. Sanasana utakuta wanajadili mipira, kubet n.k.

Nikaenda kwa mafundi masofa, gereji, madukani nikawa nawasimulia zile interview za Lissu yaani huwezi amini hawajui lolote linaloendelea wakabaki wananisikia mimi.

Toka juzi natembelea vijiwe vya watu wengi nakuta stori kubwa ni mpira na watu wengi wanajadili namna ya kuanza ratiba za kufanya mazoezi ili kujiweka vizuri kiafya.

Sasa kama huku mijini watu wa kawaida hawana habari za Lissu je huko vijijini kabisa? Kwahiyo Lissu na ziara zake hazina madhara yoyote kwenye siasa za nchi yetu.

Hizi habari zinaishia Jamiiforums pekee wakati jamii kubwa ya watanzania hawapo JF.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom