ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 23,717
- 57,243
Toka wiki iliyopita nikiingia JamiiForums nakutana na nyuzi nyingi kuhusu Lissu na ziara zake nchi za Magharibi.
Juzi nikasema nifanye utafiti; je, wananchi wa kawaida mitaani ambao sio member wa JF wana habari zozote zinazoendelea?
Nikapita katika vijiwe vyangu (mitaa ya Ubungo na Tabata) kiukweli kabisa sijabahatika kusikia watu wakizungumza hizi habari. Sanasana utakuta wanajadili mipira, kubet n.k.
Nikaenda kwa mafundi masofa, gereji, madukani nikawa nawasimulia zile interview za Lissu yaani huwezi amini hawajui lolote linaloendelea wakabaki wananisikia mimi.
Toka juzi natembelea vijiwe vya watu wengi nakuta stori kubwa ni mpira na watu wengi wanajadili namna ya kuanza ratiba za kufanya mazoezi ili kujiweka vizuri kiafya.
Sasa kama huku mijini watu wa kawaida hawana habari za Lissu je huko vijijini kabisa? Kwahiyo Lissu na ziara zake hazina madhara yoyote kwenye siasa za nchi yetu.
Hizi habari zinaishia Jamiiforums pekee wakati jamii kubwa ya watanzania hawapo JF.