Mtaalamu wa kuedit sauti (Audio) anahitajika

Mtaalamu wa kuedit sauti (Audio) anahitajika

ANKO JEI

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2018
Posts
1,319
Reaction score
2,504
Habari wakuu naimani mapambano yanaendelea. Naomba nirukie fasta kwenye mada.

Ajira zimekua ngumu hivyo tunachopata wacha tugawane. Kifupi natafuta mtu anaejua vizuri kuedit audio na ninaposema Kuedit simaanishi kuweka ma auto tune na ma"effects" ya mziki, namaanisha kukata vipande vilivyokosewa na kuviondoa ili ibaki audio clean (isiyo na makosa).

Mimi ni voice over artist, na huwa napata kazi za kurekodi audio books (vitabu kwa njia ya sauti) na makala mbalimbali, hivyo nahitaji mtu wa kuedit mana audio huwa ndefu sana na natakiwa kukamilisha kazi kabla ya deadline.

Sasa kama unaweza kuedit vizuri na KWA UMAKINI kupitia programe yoyote iwe Adobe audition au Cubase n.k naomba ni PM.

nimesema umakini kwakua audio hizi ni ndefu sana hivyo kuna sehemu zimekosewa na haitakiwi kubaki hata moja.

MALIPO
Niwe muwazi kuwa kazi hii ni ya kanisani kwetu hivyo pesa sio kubwa (nimeichukua kama kuonyesha uwezo wangu kwa clients naoweza wapata kanisani),utakapo edit audio ya masaa 4, nakulipa elfu 10. Na unatakiwa kukamilisha kwa siku 2 tu.

Naomba niseme sio kazi rahisi hivyo, na kwa wengine hilo dau linaweza kuwa dogo,ila kama unaona litakufaa naomba nicheki PM.

Ukiwa mkali wa kuedit kwa umakini na kwa wakati, yajayo yatafurahisha.

Asante.

Sent from my SM-J260F using JamiiForums mobile app
 
Naedit kwa kutumia Audacity, nitakutrain kidogo uweze kuifanya hiyo kazi mwenyewe niandalie elf 50,000
 
Naedit kwa kutumia Audacity, nitakutrain kidogo uweze kuifanya hiyo kazi mwenyewe niandalie elf 50,000
Asante mkuu, mimi naweza but tatizo muda na kazi zinanibana kufanya kila kitu mwenyewe.
 
Back
Top Bottom