Mtaalamu aponda 'Maadili' katika ripoti ya mto Mara

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
419
670
Mtaalamu Mmoja wa kutoka University of Dar es Salaam anaongea hapa kwenye kongamano la wiki ya Udhibiti na tathmini. Moja kati ya jambo kubwa analizungumza ni maadili. Ambapo kwenye maadili ni kuripoti hali jinsi ilivyo na sio kuandika ripoti kwa kumpaka mafuta aliyekupa hela ya kufanya study.

Kimsingi hii ni changamoto kubwa kwa walio wengi kwa kuwa maadili katika kufanya study. Na suala la maadili huanza muda ambao unaanza kuandaa study yako ambapo mara nyingine ni muhimu kushirikisha ERBs/IRBs. Hata hivyo maadili huongoza baada ya hapo hata unapoendelea na study ikiwemo kwenye ripoti.

Mtaalamu huyu ametoa mfano wa Ripoti ya Mto Mara kama moja ya ripoti ambayo imeshindwa kufuata maadili ya kufanya study na ndio sababu matokeo yake yamekuwa kituko hata kwa mtu asiyejua kuhusu tafiti.

Kimsingi amenikumbusha andiko la wadau walioandika kulalamikia jinsi siasa inavyoathiri kazi za sayansi ambapo mara nyingine watafiti wamekuwa wakitoa matokeo tofauti na data zilizokuwa analysed zinasema ( When science mixes with politics, all we get is politics).

Kwa wito huu, ni muhimu kuwataka waliofanya study kuhusu mto Mara walete proposal yao tuone kwa uwazi namna walivyoandaa study yao, ikibidi wajiuzulu.
 
Umenikumbusha ya ng'ombe wa kienyeji kuzalisha samadi kg25 kwa siku!

Eti tafiti imefanywa na kufungwa na Propesa!

Ndiyo maana Magu alilifukuza kidhalilishaji, halifai hata kulifungulia thread kulijadili jitu kama hilo!

Mtu kaboronga kwa ufisadi kila kona alipopita katika utumishi, utashauri ajiuzuru?
Ni kufukuza tu ndiyo dawa.
 
Back
Top Bottom