Mtaalam- UMEME WA 110V to 220V

Mtaalam- UMEME WA 110V to 220V

shilanona

Member
Joined
Oct 31, 2010
Posts
55
Reaction score
22
Nahitaji mtaalam wa mambo ya umeme ambaye anaweza kunibadilishia mashine washers na Driers na zile za kutotolea vifaranga vya kuku ambazo nimezinunua Marekani. Zote zinatumia umeme wa 110V.
Nahitaji mtaalam aje ashughulike nazo ili ziweze kuingiza na kufanya kazi kwa umeme wa 220V-240V. Wataalamu wa TANESCO chukueni tenda hii.
 
Ni PM mim ni mtaaramu nimeshawahi kufunga umeme ikulu ya Muleba.
 
Nunua transformer 220v to 110v zipo madukani bongo . Binafsi nilinunua moja miaka mitatu nyuma kwa ajali ya generator ambayo output 110v. Transformer inaweza kutumika kukuza 110v kwenda 220v au kupunguza 220v kwenda 110v . Bei wakati huo tsh 75000. Mitaa Dar siyafahamu vizuri kwa majina ila ikitoka railway station kuelekea mitaa ya kariakoo duka la vifaa vya umeme lipo kulia baada roundabout ya mwanzo na kabla kufika duka maarufu la kuuza kanga kwa jumla. Hope this will help.
 
Mashine ya kutotolea vifaranga unaweza kutumia hiyo transformer simplemind amesema inauzwa elfu 75. Kwa driers, power huwa kubwa kidogo, inabidi uwe na right transformer kufanya ifanye kazi. Hebu soma specifications za bidhaa zako kuhusu kiwango cha power, mara nyingi itakuwa imeandikwa namba ikifuatiwa na W au VA, mfano 1500W. Post hapa, unaweza kupewa ushauri wa transformer inayofaa.
 
va specification ni kipimo cha "mzigo jumla" transformer inaweza kuhimili. Haina maana mzigo ukiwa kiduchu mfano energy saver 10w itadhurika! Mfano transformer ya 1500 inaweza kuhimili bulb 150 za 10w au pump mbili za 1hp each au tv 20 za 75w au, washing machine 5 za 300w.
 
Nunua transformer 220v to 110v zipo madukani bongo . Binafsi nilinunua moja miaka mitatu nyuma kwa ajali ya generator ambayo output 110v. Transformer inaweza kutumika kukuza 110v kwenda 220v au kupunguza 220v kwenda 110v . Bei wakati huo tsh 75000. Mitaa Dar siyafahamu vizuri kwa majina ila ikitoka railway station kuelekea mitaa ya kariakoo duka la vifaa vya umeme lipo kulia baada roundabout ya mwanzo na kabla kufika duka maarufu la kuuza kanga kwa jumla. Hope this will help.
hio transformer ya 75K inapiga mziki? mie niliyooiona ktk maduka ya hapo hapo round-about ya Uhuru + chingaz maximum ilikua 40K kwa mashine ya 1000W.
 
va specification ni kipimo cha "mzigo jumla" transformer inaweza kuhimili. Haina maana mzigo ukiwa kiduchu mfano energy saver 10w itadhurika! Mfano transformer ya 1500 inaweza kuhimili bulb 150 za 10w au pump mbili za 1hp each au tv 20 za 75w au, washing machine 5 za 300w.

Nilichomshauri ni kupata "mzigo jumla" wa kila kifaa chake, siyo transformer, maana nafahamu driers zinakuwa na heaters ambazo zinakula ampia kubwa kuweza kuhimiliwa na transformer ndogo. Hilo duka ulilosema nalikumbuka, na kama sikosei hiyo bei ni ya Transformer ya 500W, na sijui kama ni kweli au ndiyo mambo yetu ya bongo tena wanaandika 500W lakini ni chini ya hapo. Sijawahi kuona dukani Transformers ya zaidi ya 1500W Dar, zaidi ya kwenye minada.

Ushauri mwingine, ni yeye kumtafuta mtaalamu wa umeme ( haitaji kuwa mhandisi) kuweza kukupa mahitaji kamili ya transformers unazotakiwa kununua. Sikushauri kubadilisha mashine zako toka 110V to 220V, na kama hiyo ndiyo option unayotaka kuchukua, peleka kwenye karakana zinazoeleweka.
 
Mashine zangu zinakula 3500W na ni 3phase, hakuna transformer inayoweza kuhimili umeme huu. Wataalam wa umeme wanasema ni possible kuzibadilisha hizi mashini na kuwa 220V tena bila shida kubwa. Nitafutieni mtaalam anisaidie nami nimpe ajira.
 
Back
Top Bottom