Msutaji akisusa

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,208
4,406
MSUTAJI AKISUSA.









1)Samani poleni sana,japo yaweza kuuma.
Ila nikuchukizana,mdomo waweza sema.
Kwa bidii kukazana,bora ninene mapema.
Msutaji akisusa,msutwaji hufurahi.





2)jasiri mwenye ujana,hawezi kukata tama.
Ila muoga wa jana,ni kurudi nyuma nyuma.
Mbele kusonga laana,acha pate alochuma.
Msutaji akisusa,msutwaji hufuraji.





3)suta bila kupigana,tumi akili si sima
Ila vyema uko sana,kama mnyama wa kuhama.
Manyumbu wapo kazana,kufatana ni lazima.
Msutaji akisusa,msutwaji hufurahi.



4)kama ni kuburuzana,japo lo ngumu kusema.
Ila mlishauryana,naona nyote mwavuma.
Ala kumbe danadana,zipigini mle nyama.
Msutaji akisusa,msutwaji hufurahi.




Shairi:MSUTAJI AKISUSA.
mtunzi:Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
0765382386.
0655519736.
iddyallyninga@gmail.com
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom