Bahari ya kifo

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,209
4,406
1)walikuwa na amani,kabla wao kuingia.
Wakisali mjengoni,chuki wakiuchukia.
Ila wale mashetani,chuki wakawapandia.
Ukaota na vichwa,huku wakiitambua.
Wakimbizi wangamia,kwenya bahari ya kifo.
2)wanatoroka vitani,vile mloanzishia.
Mafuta ya kisimani,mlitaka yachukua.
Leo nyote hatarini,tamaa mtajutia.
Mmejiweka motoni,kaa lawaunguzia.
Wakimbizi wangamia,kwenye bahari ya kifo.
3)wanafia baharini,halaiki kwa mamia
Na machozi mashavuni,yadondoka wakilia.
Mmeufanya uhuni, binadamu kuonea.
Wakimbizi wangamia,kwenye bahari ya kifo.
Shairi:BAHARI YA KIFO.
Mtunzi:Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
0765382386
iddyallyninga@gmail.com
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom