Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,209
- 4,406
NG'E WA KAYA.
1)wazee walishasema,kaziyo siyo rahisi.
Wakakuonya mapema,ukawahisi mijusi.
Kwamba kweli mwanachama,utaifuta najisi.
Hawa ndo ng'e wa kaya,lazima uwafute.
2)salamu zangu natuma,mzee usodadisi.
Mijibwa uloituma,yakutia ukakasi.
Matunda utayochuma,yatawa laana fisi.
Hawa ndo ng'e wa kaya,lazima uwafuate.
3)vya kunyonga ni lazima,vibaya wala wahisi
Wamezweya kula kima,na fahari kwa harusi.
Wanajiona taruma,kuibia mafulusi.
Hawa ndo ng'e wa kaya,lazima uwafuate.
4)japo wa kulisha sima,akuchekea Anasi.
Tupa i yako ilima,wao wapake kamasi.
Hujui wao ni duma,au wataka uasi.
Hawa ndo ng'e wa kaya,lazima uwafuate.
5) makoloni unolima,yataja iva kwa kasi.
Upepo unaovuma,utakunyima nafasi.
Tukuombee karima,na vibaya tukihisi.
Hawa ndo ng'e wa kaya,washakushika akili.
Shairi:NG'E WA KAYA.
Mtunzi:Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160.
iddyallyninga@gmail.com.
Facebook page:Idd ninga na mashairi.
1)wazee walishasema,kaziyo siyo rahisi.
Wakakuonya mapema,ukawahisi mijusi.
Kwamba kweli mwanachama,utaifuta najisi.
Hawa ndo ng'e wa kaya,lazima uwafute.
2)salamu zangu natuma,mzee usodadisi.
Mijibwa uloituma,yakutia ukakasi.
Matunda utayochuma,yatawa laana fisi.
Hawa ndo ng'e wa kaya,lazima uwafuate.
3)vya kunyonga ni lazima,vibaya wala wahisi
Wamezweya kula kima,na fahari kwa harusi.
Wanajiona taruma,kuibia mafulusi.
Hawa ndo ng'e wa kaya,lazima uwafuate.
4)japo wa kulisha sima,akuchekea Anasi.
Tupa i yako ilima,wao wapake kamasi.
Hujui wao ni duma,au wataka uasi.
Hawa ndo ng'e wa kaya,lazima uwafuate.
5) makoloni unolima,yataja iva kwa kasi.
Upepo unaovuma,utakunyima nafasi.
Tukuombee karima,na vibaya tukihisi.
Hawa ndo ng'e wa kaya,washakushika akili.
Shairi:NG'E WA KAYA.
Mtunzi:Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160.
iddyallyninga@gmail.com.
Facebook page:Idd ninga na mashairi.