Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,208
- 4,406
KUMBE TAMBARA.
1)mwanzo nilipokiona,nikiwa siambiliki.
Niliona amenona,kikinukia iliki.
Bichwa langu likatuna,na mkono sishikiki
Nilijua hajaguswa,kumbe haswa ni tambara.
2)kile nilichokiona,kisima kiso riziki.
Nahisi mkiwa mwana,nimeshikiwa mkuki.
Sikipendi tena sana,tunda gani haliliki.
Nilijua hajaguswa,kumbe haswa ni tambara.
3)kutapika nikaona,kitu hakizuiliki
Nikaanza kulumbana,ilaye halalamiki.
Katulia na kitana,muziki hauchezeki.
Nilijua hajaguswa,kumbe hasa ni tambara.
4)mwanzo ni kutazamana,harufu mbata inuki.
Na vidogo kupeana,ningejua mbona nduki.
Awali kuburuzana,hata kama hauchoki.
Nilijua hajaguswa kumbe haswa ni tambara.
Shairi:KUMBE TAMBARA.
Mtunzi;Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
0655519736.
0765382386.
iddyallyninga@gmail.com