Msukule ni nini?

Msukule ni mtu anayechukuliwa kimiujiza na wachawi na kwenda kufanyishwa kazi. Msukule huwa hauna uwezo wa kuongea maana hukatwa ulimi
 
Huyu binti wa juzi inamaana hakufikia hatua ya kua msukule, sioni mkiongekea habari yake ilihali ni habari mpya kabisa ingefaa kuifanyia rejea.

Vyovyote iwavyo ni kwamba yule binti anamhusu muhusika mwenyewe kwani ingekua kinyume chake wangesha jitokeza wazazi wake kwa makelele.

©mzizimkavu
mshanajr
 
Lipo pia hili la watoto wadogo/wachanga wanafariki na kusemekana nao wamefanywa msukule angali hawana nguvu za kufanya kazi au hili nalo lipoje hili..na je hizo dawa source yake ni nini?

Binadamu ana mwili na ndani ya mwili kuna roho, roho ya mtoto, roho ya kijana na roho ya mzee zote ziko sawa, tofauti ipo kwenye mwili uliovalishwa hiyo roho. Kwa taarifa yako watoto ndio wanaotumiwa sana kwenye ulozi kuliko vijana na wazee.
 
Poneaponea ni kuwa mvivu.hawachukui wavivu.haha
 
Kariokoo yote ile wale wengine sio watu nadhani ndo sehemu inayoongoza dar kwa misekule inabeba mizigo ile pale acha tu
Hivi misukule hufanyishwa kazi wazi wazi katika macho ya binadamu wa kawaida.
 
Kwa nyongeza ni kwamba, msukule huwa unakufa na ukifa huwa ni chakula cha wachawi.
 


Arusha kati ya mwaka 1989 au 90 mwanzoni wakati wahindi wanakimbia uhujumu uchumi na kwenda Kenya, kuna familia ya kihindi walikimbia na kumuacha msukule muhindi mwenzao karibu wiki nzima ndani ya nyumba. Watoto walikuwa hawapiiti pale mtaani kwenda shule kuogopa kunyonywa damu. Cha kushangaza yule msukule alikuja kupotea kimaajab na mpaka leo imebaki hadithi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…