Kuna watanzania wengi wanaokuwa kwenye vyama mbalimbali kama binadamu wamefanya makosa na chama hakikuhusishwa Ditopile alivyomuua dereva wa daladala kwa pisto hakuna aliyesema ditopile wa CCM ametumwana CCM au hakuna aliyesema Rafiki wa KIKWETE aliyesimamia harusi ya KIKWETE NA SALMA ameua dereva kwenye makutano ya barabara ya Kawe na Lugalo watu tulimtuhumu Ditopile kwa matumizi mabaya ya pisto kama mtu binafsi
Hata alivyowekwa nje ya rumande tofauti na watuhumiwa wote wenye kesi za mauaji hakuna aliyesema Mwenyekiti wa CCM Jakaya Kikwete amemtoa kwa vile ni rafiki yake au ni mwanaCCM sisi tulisema polisi ni vipi wamefanya upelelezi wa haraka kwa Ditopile wakati kunawatu wako ndani kwa makosa
Chenge alipotumia gari lake na kuuwa wanawake wawili halafu akakimbia hatukusema Chenge mwanachama wa CCM ameua wanawake wawili alafu akatimuka alituhumiwa kama chenge
Masha alipotishia wanachi kwa pisto hatukusema Masha mwanachama wa CCM anatumia vibaya silaha,sasa huyu diwani wa Chadema atuhumiwe kama mtanzania yeyote atakayetuhumiwa anayemiliki silaha kinyume cha utaratibu
sidhani hii kampeni kama itasaidia ,endelea tuu wanachi wanajua kupembua pumba na mchele ,eneo la Bunda ,serengeti,tarime mara ngapi silaha zimekamatwa toka kwa wananchi na zikachomwa