Msomali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msomali

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mentor, Oct 19, 2016.

 1. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2016
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 19,299
  Likes Received: 9,770
  Trophy Points: 280
  Msomali


  Inasemekana katika mataifa barani Afrika yenye wadada wenye ulimbwende wa asili basi mataifa haya matatu; Eritrea, Ethiopia na Somalia, kamwe hayawezi kukosekana katika namba za juu kabisa.


  2016, Chuo Kikuu

  Nilikwenda pamoja na baadhi ya wenzangu chuoni hapo kutoa mada juu ya soko la ajira kama njia ya kujitoa kwenye chuo kilichotulea wakati tukisoma huko (giving back to your alma mater).

  Tulikutana wengi tuliokuwa tumesoma mwaka mmoja na wengine wa miaka ya nyuma na mbele yetu. Ilikuwa siku nzuri sana maana tulikumbushana mambo mengi ya ujana tuliyofanya tukiwa chuoni hapo.

  Wengi sasa walikuwa na familia zao – ndiyo, isipokuwa mimi – na wale ambao walibahatika kuwa na wake zao ambao nao tulisoma wote chuo hicho walikuja nao kuturingishia sie. Ilipendeza sana walipokuwa wakiwaambia wanafunzi kuwa wao walikuwa wapenzi miaka kumi na iliyopita na sasa ni familia moja. Waliwatia moyo wanafunzi kuwa kama wanapendana haimaanishi kuwa wakimaliza chuo ndiyo mapenzi yataisha. Niliamua kujiondoa kwenye mjadala huo maana ulinikumbusha machungu tu.

  Nilitoka ukumbini na kuanza kutembea bila kuwa na lengo maalum la nilipotaka kwenda isipokuwa tu kwa lisaa limoja lijalo nisiwepo ukumbini kule kwenye mada ya 'ujana na mahusiano'. Nilitakiwa kurudi tena kutoa mada ya 'Morality in the Workplace: How university experience can shape you'.

  Nilijikuta nimesimama ghafla baada ya kuisikia sauti, sauti ambayo sikujua kama bado ningeweza kuikumbuka. Nilijua hii sauti nilishawahi kuisikia, miaka mingi iliyopita. Nilitembea kwa kunyata na kuchungulia kuthibitisha sauti ile ilikuwa ya yule niliyemdhania.

  Mentor huyu huyu ambaye ndiyo ameteuliwa kuwa Mkurugenzi pale TIRA? Wewe msomali ulipoteza bahatiee...” ilikuwa sauti ya binti mmoja.

  “Ndiyo huyo huyo” ilijibu sauti ile. “Lakini hilo sio la maana.” aliendelea.


  2002

  “Tulikuwa mwaka wa pili na penzi letu lilikuwa ndiyo kwanza linaanza kuchanua. Nilimpenda Mentor na yeye alionesha kunipenda sana. Alikuwa ni wale wakaka wapole unajua, wao ni kitabu na mpira tu. Hata alivyokuja kunitongoza nilibaki najiuliza alinioneaga wapi?

  Basi bwana tukaenda hivyo hivyo hadi hii 2003 wakati tumeenda kwenye mazoezi kwa vitendo (field).

  Nikakutana na mkaka ambaye yeye alikuwa anafanya kazi pale. Alikuwa mzuriiii! Basi yeye kila siku anavaa suti tu. Ni wale tunawaita; tall-dark-handsome, halafu anavaa miwani yake full kutabasamu. Halafu hana hata miaka mingi hapo tayari keshapandishwa cheo mara mbili tangu aajiriwe.

  Kidogo kidogo akaanza kunizoea, mara akipita kwenye meza yangu aniguse bega, siku nyingine aniletee chocolate, mara biskuti, ali mradi hakosi kitu cha kunishtua kila siku.

  Mwanzoni nilikuwa namchukulia poa maana nilikuwa na Mentor lakini kadri siku zilivyoenda nilizidi kumzoea. Alinifanyia mpango hata baada ya kumaliza field niwe naenda kazini kwa masaa machache na ilinisaidia sana kupata uzoefu. Kidogo kidogo hata muda wa kukaa na Mentor ukaanza kupungua maana kule kazi, shule na vimtoko vya kuibia na huyu mpya.

  Siku ya siku, bwana yule akanitamkia wazi kuwa ananipenda, anataka kunioa nitakapomaliza tu chuo. Ilibidi nimueleze tu kuwa nina mpenzi mwingine. Akanisisitizia ari yake lakini akanipa wiki moja nimpe jibu.

  Nilitaka niwe nao wote maana kila mmoja alikuwa na sifa yake tofauti na mwenzake. Lakini baada ya muda nilikaa nikatafakari nikaona ninachofanya si kizuri, sikulelewa hivyo mimi. Nikatafakari kati ya hawa wawii ni nani nilikuwa nampenda zaidi. Hivyo nikamfuata Mentor nikamueleza kuwa sitaweza kuendelea naye tena kwani nimempata mwanaume mwingine. Nilimuomba msamaha sana maana nilijua nilimuumiza lakini ilibidi nimueleze ukweli.

  Ulikuwa ni mwezi mrefu sana kwangu maana ndiyo tulikuwa tumeingia mwaka wa tatu sasa. Mentor kichwani kwake alijua tukimaliza chuo tu ndiyo ndoa. Nakubali nilikuwa nikimpenda Mentor lakini baada ya kukutana na huyu kaka niligundua sikuwa nikimpenda vva kutosha.

  Mentor alinisumbua sana akitaka hata nimpeleke kwetu akaongee na wazazi wangu kama shida ni ndoa. Alikuwa tayari kwa lolote maskini kaka wa watu.

  Hata hivyo baada ya muda alikubali kushindwa nami nikaanza penzi jipya na huyu mwingine. Maisha yalikuwa nusu mbingu nusu dunia. Alikuwa mtaratibu mno, mcheshi na zaidi alipenda kuzungumzia mambo magumu magumu ya maisha. Alinifanya kila siku nijifunze jambo jipya niangalie habari kiasi kwamba hata masomo yangu yalipanda maana nilikuwa ninasoma mambo hayohayo.

  Wakati nikimalizia mwaka wangu wa mwisho nilipata fursa ya kuomba kwenda kufanya kazi makao makuu ya Umoja wa Mataifa maana tukiwa chuo nilikuwa mhudhuriaji mkubwa wa makongamano na miradi yao. Hiyo nafasi hiyo ilipojitokeza wale wawezeshaji (facilitators) wa upande wa Tanzania walinihimiza kuiomba nafasi hiyo na walinithibitishia wataongeza neno lao na nitapata nafasi hiyo.

  Ilikuwa kazi ya muda/mkataba wa miaka mitatu tu lakini niliiona kuwa ni fursa nzuri sana. Nilimueleza mpenzi wangu na alifurahi sana. Aliahidi kunisaidia katika mchakato mzima.

  Huku shule ikielekea ukingoni, nami nilikuwa namalizia viambatanisho vya mwisho vya maombi yangu. Kama sio yeye sidhani kama ningemaliza maana mambo yalikuwa mengi mno.

  Siku moja nikiwa natoka darasani, miezi miwili kabla ya kufanya mitihani ya mwisho, nilisikia kichefuchefu ghafla na nilitapika. Wala bila kuuliza nilielekea duka la dawa na kununua vihusika na kama ilivyokuwa nilikuwa na ujauzito.

  Nilipata mawazo mengi; shule, kazi, nyumbani. Mambo haya yalinipa msongo wa mawazo maana kiukweli sikutarajia kupata ujauzito wakati huu. Nilitaka nami nijifungue ndani ya ndoa. Katika msongo wote huo wa mawazo kitu pekee kilichonipa tabasamu ni kumfikiria baba mtoto maana siku zote alikuwa akinitania, “Yani mtoto wetu atatoka mzuri balaa kama shombe wa Kisomali!

  Nilitabasamu maana nilimuona anavyofurahia kumuona mwanetu. Nilisahau hata nitawaelezaje wazazi na ndugu zangu maana Msomali mimi ndiyo nilikuwa mfano wa ndugu na wadogo zangu. Kila kitu kizuri lazima Msomali nitajwe kama mfano wa kuigwa. Nilisahau kazi ambayo niliiomba na itakuwaje kwenda huko na ujauzito. Nilisahau yote hayo, nilitoka chooni nikiwa na tabasamu kama vile nimeambiwa Yanga na Chelsea wameshinda ligi! Hahah

  Nilichukua simu na kumpigia ili kumtaka kuongea naye baadaye jioni. Alikubali na kama tulivyoongea jioni alikuja na maua mazuri ambayo alinikabidhi, bado nilikuwa nikitabasamu.

  Nilimueleza kuhusu ujauzito wangu na hapo ndipo nilipona maajabu. “Hapana Msomali! Siko tayari na kulea mtoto kwa sasa..hapana! Ulipataje sasa na wewe ulisema ulikuwa siku salama? Hapana msomali.

  Hata nilipojaribu kuomba msaada kupitia rafiki zake na baadhi ya ndugu alinitukana, alinisema vibaya. Alionesha dhahiri hataki kusikia juu ya mimba wala mtoto.

  Kwa jioni ile aliondoka bila kusema zaidi ya hapo na nilijifariji kuwa huenda ni ule mshituko wa kuwa baba. Niliamua kumpa muda ajitafakari na baadaye atatulia.

  Hali haikuwa kama nilivyotarajia maana kadri siku zilivyoenda ndivyo alivyozidi kuwa mkali. Alifikia hadi hatua ya kuniambia niitoe mimba. Niliumia sana. “Mimba au mimi”, ndiyo zilikuwa chaguzi zangu.

  Kumbe wakati mimi naandika maombi yangu ya kwenda kufanya kazi naye alikuwa anafanya maombi ya kwenda shule nchi ile ile ambayo nami nilikuwa naenda kufanya kazi. Kwa bahati nzuri yeye alikuwa ameshapata na majibu kuwa amekubaliwa na angeondoka mwezi Novemba mwaka huo. Alikuwa ameiweka kama siri ili aje kuniambia baadaye. Sikuwa nimefahamu hadi siku moja kabla hajaondoka ambapo alinipigia kuniambia kuwa anaondoka kesho yake.

  Lengo hasa la simu yake halikuwa kuniaga ila kisingizio kutaka kujua kama niliitoa mimba ile au la maana tangu aniache siku ile hatukuwa tumeonana tena.

  Nilimaliza chuo huku nikitafakari sana kuitoa mimba ile lakini nashukuru Mungu nilipata rafiki wazuri walionishawishi kutoitoa mimba ile. Siwezi kuelezea yote waliyoniambia ila somo liliniingia nikaamua nirudi nyumbani kwa wazazi wangu niwaeleze lililotokea. Kinyume na matarajio yangu, nyumbani walinipokea vizuri sana tena wazazi na ndugu waliojua mkasa ule walinionea huruma sana. Niliendelea kubaki nyumbani hadi Novemba hiyo aliyonipigia simu.

  Baada ya kukata simu yake ndipo nami nikakumbuka maombi yangu niliyoyatuma. Nilifahamu kuwa kwa taratibu za huko hata kama mtu umekosa nafasi ni lazima wakuambie. Hivyo niliingia kwa mategemeo ya kukuta barua pepe yenye kunijulisha nimekosa. Sikuwa nimeingia tena huko tangu jioni ile nilipoachwa maana pia vitu vingi alikuwa akivifanya yeye. Alikuwa na nywila yangu.

  Niliangalia barua pepe zote mpya na sikuona yoyote ya kuhusu hilo hadi nilipoangalia vyema na kukuta moja ambayo ilikwishafunguliwa kumaanisha aliiona na hakuniambia. Ilikuwa ikihitaji mimi kuongeza 'referee' mmoja zaidi maana nilikuwa nimeandika wawili tu. Niliumia sana kwamba hakuniambia na hata nilipoenda kwenye 'portal' yao hakuwa ameongeza chochote. Kigezo hicho kimoja, kikawa kimenikosesha kazi, niko nyumbani na ujauzito na siwezi kwenda kuomba kazi mahali kwa hali ile. Nahisi nilikuwa na miezi sita hivi.

  Maisha yalienda kama kawaida, nikajifungua vyema mtoto wa kike ambaye nashukuru Mungu alifanana na mimi karibia kila kitu. Sasa yeye ndo alikuwa shombeshombe, msomali, wa ukweli. Nilitamani nimueleze baba yake lakini nilijizuia maana hakutaka kujua chochote kuhusu mwanaye.

  Nakumbuka wakati mmoja kabla hajarudi nilijikuta tu nikimtumia picha za mwanaye, walau amuone tu. Nahisi aliona nataka kumuomba pesa au kurudisha mahusiano hivyo aliipuuzia barua ile.

  Baada ya muda moyo ulianza kupoa hasa baada ya hasira za kutelekezewa mtoto na hisia za mapenzi kwake kuisha.

  Nilianza zangu kazi miezi sita tu baada ya kujifungua na maisha yamekuwa yakiendelea kama kawaida. Sasa hivi nimeolewa na mume wangu tunaishi vyema kabisa na wala sifahamu huyo jamaa yuko wapi.” alimalizia kusimuliza Msomali.

  Niligeuka na kuendelea kunyata kurudi ukumbini maana niliyoyasikia yalitosha, yalitosha kunikumbusha miaka zaidi ya kumi iliyopita ambapo nilimpoteza binti niliyempenda. Niliiangalia saa yangu na kugundua nimebakiza dakika kumi kabla muda wangu ufike wa kutoa mada yangu. Niliamua kujikaza kutokukuonesha hisia zozote maana kwa vyovyote vile, lazima maisha yaendelee...


  Wasalaam wapendwa,
  Mentor.
   
 2. feitty

  feitty JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2016
  Joined: Jul 10, 2015
  Messages: 1,860
  Likes Received: 2,021
  Trophy Points: 280
  Nimejifunza kitu kwenye hii story
  Kweli usiache mbachao kwa msala upitao.
   
 3. hill and portion

  hill and portion JF-Expert Member

  #3
  Oct 19, 2016
  Joined: Sep 26, 2014
  Messages: 1,236
  Likes Received: 557
  Trophy Points: 280
  Waooooo nice story mentor huwa napenda sana story zake zinaburudisha na zina ujumbe kabambe ....big up
   
 4. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #4
  Oct 19, 2016
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 19,299
  Likes Received: 9,770
  Trophy Points: 280
  Mkuu feitty watu wanaweza kuwa na mitazamo tofauti kwenye hilo.
  Thanks for appreciating mkuu.
   
 5. Amoxlin

  Amoxlin JF-Expert Member

  #5
  Oct 19, 2016
  Joined: May 30, 2016
  Messages: 3,610
  Likes Received: 3,659
  Trophy Points: 280
  Hii story naifananisha na yaliyomkuta binti flan...
  Ama kweli kupanga ni kuchagua.
   
 6. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #6
  Oct 20, 2016
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 19,299
  Likes Received: 9,770
  Trophy Points: 280

  hebu tupe summary mkuu!
   
 7. kabanga

  kabanga JF-Expert Member

  #7
  Oct 20, 2016
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 31,105
  Likes Received: 4,632
  Trophy Points: 280
  Vijana huwa tunashikwa na kigugumizi sana pale ujauzito unapoingia na ukizingatia hamjatarajia au ile wanaume tunasema Piga na usepe...!!
   
 8. Amoxlin

  Amoxlin JF-Expert Member

  #8
  Oct 20, 2016
  Joined: May 30, 2016
  Messages: 3,610
  Likes Received: 3,659
  Trophy Points: 280
  Huyo binti nilifahamiana nae mwaka juzi, ni mwenyeji wa Rombo. Binti huyu alikua anasoma medical assistant chuo flani kipo Iringa. Alibahatika kupata mpenzi aliempenda sana na kumjali ktk shida zake sambamba na kumshauri mara kwa mara.

  Jamaa alikua tayaribkumuoa binti na waanze maisha ya familia baada ya masomo ila binti alileta nyodo nyingi, alidai hana mpango wa kiolewa na jamaa alipomwambia yupo tayar kusubiri binti alizidi kumkatisha tamaa.

  Kwa vituko vyake hivyo kumbe binti alikua na mpenzi wake mwinginea aliyeitwa Nuhu, ambae alikua anasoma udaktari ktk chuo kingine mkoa mwingine. Jamaa huyu hakuwa akimsaidia binti kwa lolote japo binti alikua na maisha magumu.

  Tuseme binti alimpenda tu sababu ya mvuto wake japo hakunufaika na kitu zaidi ya maneno. Hali hii ilimkatisha tamaa jamaa yule mwenye mapenzi ya dhati kwakua alishatumia mbinu nyingi mpaka kutumia ndg zake xo akaamua kuachana nae.

  Ilipofika mwaka jana kwa mara ya kwanza yule binti alilala na mpenzi wake (Nuhu) ambapo ndio alimtoa usichana wake. Na siku hiyo hiyo binti yule aliweza kupata ujauzito ila hakutambua kwa wakati huo mpaka alipoona dalili mbeleni.

  Siku zikaenda na mimba ikakua, jamaa hakumhudumia kwa chochote mpaka alipojifungua ndio wakaonana (ilibidi binti akaishi kwa shangazi yake kwani wazaz wake walishatengana na aliogopa kuwaeleza kama ana ujauzito).

  Miezi miwili baada ya kujifungua kwa OP Nuhu alikua busy sana, yupo online lakini hamtafuti mzazi mwenzake hata wiki nzima. Akaanza kuonesha ishara zisizo njema, alimtumie sms isemayo "natamani huyo binti akue akuache ifanye mambo yako". Baada ya siku kadhaa akaamua kumwambia ukweli kwamba hawezi kumuoa kwani ana mchumba na walishapelekana mpaka kwa wazazi xo hakuna jinsi.

  Binti alichanganyikiwa kwani mpaka sasa mtoto ana miezi mitatu, ajira hazijatoka, Nuhu hatoi matunzo, bado anaishi kwa shangazi na hajuu atawaambia nin wazaz wake kama alomzalisha hatomuoa.
   
 9. P

  Pohamba JF-Expert Member

  #9
  Oct 20, 2016
  Joined: Jun 2, 2015
  Messages: 16,603
  Likes Received: 25,770
  Trophy Points: 280
  Wasomali ndio Binadamu Wenye ngozi laini zaid Duniani bila ya kujali Jinsia zao!
  Kama huo ndo ugonjwa wako basi hapo ndo kwenyewe
   
 10. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #10
  Oct 20, 2016
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 19,299
  Likes Received: 9,770
  Trophy Points: 280

  Ila kama ni kigugumizi mbona wengi huwa hawajirudi baada ya muda?

  Ninafahamu wadada wengine watatu ambao mpaka sasa watoto wana - miezi 9, miaka 2, miaka 5 - na hao wanaume mpaka leo hawajui watoto wao wakoje!
   
 11. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #11
  Oct 20, 2016
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 19,299
  Likes Received: 9,770
  Trophy Points: 280

  Duuuh mbona hii stori kama ya Honey Faith na RRONDO!???

  Anyway, to be honest inashtua! Duh mi sijui vijana huwa tuna tatizo gani...ni wepesi sana kumwaga ndani ila inapokuja kulea matokeo tunakuwa wagumu sana aisee..I don't know why!!!
   
 12. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #12
  Oct 20, 2016
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 19,299
  Likes Received: 9,770
  Trophy Points: 280

  Ahahah mkuu hii tafiti yako uliifanyia wapi hahaha!
   
 13. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #13
  Oct 20, 2016
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 30,380
  Likes Received: 29,135
  Trophy Points: 280
  Mkuu nimehama mji at least nisahau lakini naona unafanya jitihada kubwa kunikumbusha!
   
 14. M

  Mapambano kag Senior Member

  #14
  Oct 20, 2016
  Joined: Aug 29, 2013
  Messages: 117
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Story nzuri sana,bora hukuweka masuala ya ukimwi
   
 15. Kasinde

  Kasinde JF-Expert Member

  #15
  Oct 20, 2016
  Joined: Dec 29, 2013
  Messages: 5,978
  Likes Received: 3,606
  Trophy Points: 280
  Mentor hadithi au simulizi ni nzuri ila inahuzunisha ......:(

  Binafsi nimeshashuhudia wadada wengi tuu wakijilaumu bora ningemkubali yule ambaye sikuwa nimempenda kuliko niliyempenda kanizawadia mtoto na kanitelekeza.

  Jana niliona kwenye taarifa ya habari kuna mwanamke ametelekeza mtoto wa miezi 5 ubungo, katoto ka kike. Inasikitisha kiukweli hata kama hatujasikia na kufahamu yaliyomsibu huyo mama bado haitoi kibali cha kumruhusu huyo mama atelekeze mtoto.

  Iwe isiwe umepata mimba kisha mwanaume kakuacha kaenda oa mwingine au hata alikuwa hakupendi basi (mwanamke) ukiamua kulea mimba jikaze ulee mtoto na si uzae kisha umtupe au umtelekeze.

  Binafsi hayajanikuta hayo ila machungu ya kuachwa nayafahamu maana hata mie nilishawahi kuachwa nilipopenda. .... mbaya zaidi ule wimbo wa C. Bella -Kuachwa ni Shughuli Pevu ndo ulikuwa umetoka.... Acha asikwambie mtu maumivu yake.... yale maneno ya ule wimbo yanachoma na kuumiza moyo....

  Aaah shida yangu Mentor unaifahamu siwezi kuweka muhtahsari au habari kwa ufupi matokeo yake najikuta natoka nje ya mada.....

  Acha niweke kalamu chini japo bado sijamaliza. ..

  Alamsiki till the lunch day.:)
   
 16. Nifah

  Nifah JF-Expert Member

  #16
  Oct 20, 2016
  Joined: Feb 12, 2014
  Messages: 26,070
  Likes Received: 24,930
  Trophy Points: 280
  Naam..."Kivyovyote vile,lazima maisha yaendelee"
  Moja kati ya msemo niupendao sana.
  Asante Mentor
   
 17. Kasinde

  Kasinde JF-Expert Member

  #17
  Oct 20, 2016
  Joined: Dec 29, 2013
  Messages: 5,978
  Likes Received: 3,606
  Trophy Points: 280
  Halafu.....

  Hapo kwenye binti wa kisomali umenikumbusha wakati flani...... Kweli wakati ukuta....

  Kwa mtazamo mwingine mahusiano yana mambo mengi sana. Kwenye simulizi yako huyo binti wa kisomali hakufanya sawa kwa Mentor hasa pale alipomuacha tuu kwakuwa alipata mpenzi mwingine akiwa field. Hapo ndo kuna tofauti ya moyo wa kike na wa kiume. Mschana anapenda toka moyoni na kama hajapenda hata huyo anayependa ajue iko siku atazinguliwa au ataachwa tuu.
  Kwa sehemu nyingine binti wa kisomali alifanya vizuri kumuacha Mentor kwa kumwambia ukweli kuliko angeendelea kuwa na wapenzi wawili kwa wakati mmoja. Hapo namsifu msomali.

  Ila huyo mpenzi mpya nae anatabia mbaya, kwanini hata asingemdanganya kuwa wee lea mimba mtoto akikua nami nikirudi tutaona walau hii ingemfanya Msomali asiwe na msongo wa mawazo na kulea kiumbe kilichoko tumboni kwa afya.

  Mentor ni miaka 10 sasa msomali alishaolewa na anafamilia yake na mumewe mwingine, ila mentor bado hajaoa. ..... mpango wako ukoje? na yule aliyempa mimba msomali nae sijui kama alioa au nae bado yuko single.........

  Just food for though...

  Eeeh hivi kumbe nilishasema Alamsiki na nilishaweka kalamu chini khaaa! ! Sasa kifuatacho ITV ni kuzima kama friji heheheheheheee

  Ciao:);):p:p
   
 18. Yegomasika

  Yegomasika JF-Expert Member

  #18
  Oct 20, 2016
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 9,613
  Likes Received: 37,969
  Trophy Points: 280
  Kasinde, natafuta mchumba, naomba nilete posa kwako! Kiuchumi bado natafuta, siko alosto kivile; ila sina BMW! Wasemaje weye?
   
 19. Kasinde

  Kasinde JF-Expert Member

  #19
  Oct 21, 2016
  Joined: Dec 29, 2013
  Messages: 5,978
  Likes Received: 3,606
  Trophy Points: 280
  Hahahahahahaa haraka haraka nimesoma kuwa unataka nikusaidie kutafuta mchumba ili upeleke posa kwao uoe.
  Hahahahahaa nilipofika hapo kwenye BMW kuwa hauna looh ndo nikashtuka na kuanza kusoma upya.

  Wee fanya ufanyalo (ila tuu usiibe) hakikisha unakuja na BMW jina la kadi lisome Kasinde Yegomasika basi unakuwa ushamaliza kila kitu. Utakula wali mboga 12 ugali mboga 21 hadi useme pooo. .......

  Hehehehehehehhee kidali poooh looh.
   
 20. Padri Mcharo

  Padri Mcharo JF-Expert Member

  #20
  Oct 21, 2016
  Joined: Feb 28, 2015
  Messages: 1,933
  Likes Received: 3,343
  Trophy Points: 280
  Hata sijaelewa story inahusu nini exactly.
  Dhamira kuu ni ipi hasa...

  #Chief Eng
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...