Msoma mita wa Dawasco afikishwa mahakamani

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,933
22,095
Msoma mita wa Dawasco afikishwa mahakamani

Kuruthum Ahmed


MSOMA mita wa Kampuni ya kusambaza maji jijini Dar es Salaam(Dawasco), Chobines Mabega (38), jana alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinonondoni, akikabiliwa na tuhuma mbili ikiwemo ya kuomba hongo.


Katika shtaka la kwanza ilidaiwa na Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya kupambana na kuzuia Rushwa (PCCB), Ronald Manyiri kuwa mtuhumiwa anakabiliwa na shtaka la kuomba hongo.


Akisoma hati ya shtaka hilo, mbele ya Hakimu Sundi Fimbo, Manyiri alidai Januari 20 ,eneo la Mikocheni katika Hotel ya keys, mtuhumiwa ambaye ni mwajiriwa wa Dawasco aliomba Sh milioni 1,500,000 kama kishawishi cha kutomchukulia hatua za kisheria kwa kuunganisha maji kinyume cha utaratibu.


Katika shtaka la pili, mwendesha mashtaka huyo alidai Januari 22, maeneo ya Bar Blue Star, mtuhumiwa alimshawishi mtu ampatie Sh 750,000 zikiwa ni sehemu ya hongo,kutoka kwa mlalamikaji Kinabo Masawe.


Hata hivyo, mtuhumiwa alikana mashtaka hayo na yupo nje kwa dhamana , kesi hiyo iliahirishwa hadi Februali 16 mwaka huu.

Wakati huo huo, Yusuph Said alifikishwa katika mahakama hiyo akikabiliwa na shtaka la kumbaka msichana mwenye umri wa miaka (14)


Akisoma hati ya shtaka hilo mwendesha mashtaka wa polisi inspekta Nassor Sisiwahy alidai mbele ya hakimu Linna Msanga kwamba Desemba mwaka jana, saa 10:00 jioni, maeneo ya Boko, mtuhumiwa alimbaka msichana mwenye umri wa miaka 14.


Hata hivyo mtuhumiwa alikana shtaka hilo nayupo ndani kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana na kesi hiyo iliahirishwa hadi Februali 16.
 
Back
Top Bottom