Swali linajitosheleza wakuu, MSM, WAP, naongezea hapo na APN , DATA ROAMING maana na kazi zake.
Mkuu zamani za kale kabla ya chrome, whatsapp, fb na app unazozijua za sasa simu zilikuwa hazina uwezo wa kutuma picha wala kuperuzi internet vizuri.
Mms (multimedia message) yenyewe ndio ilitumika kama whatsapp, ukichat na mtu ukitaka kumtumia picha unatumia mms, na ilikuwa inatumia internet kutuma. enzi hizo hata simu za vitochi sio common mpaka visimu vidogo vina uwezo wa internet. Na kulikuwa hakuna vifurushi ukituma mms inakula salio vibaya mno (1mb sh 200 salio linakatwa).
Wap yenyewe ni setting kama za internet sema inakuwa na proxy. Zamani browser za simu hazikuwa na uwezo kama za pc hivyo unapofungua web kubwa inaleta matatizo sana, inaweza kujifunga kwa kuzidiwa ama kuwa slow sana, hii proxy ya wap ilikuwa inasaidia kupunguza huo mzigo. Na hata website kipindi kile tulikuwa tunaita website za wml kama wapsite na za html kama website, na ukivisit google za wap zinakuwa na kialama cha simu.
Data Roaming yenyewe inatokea eneo ambalo wewe mtandao wako haupo na unaazima minara ya mtandao mwengine. Mfano TTCL haipo nchi nzima ukiwa maeneo ambayo hakuna minara ya TTCL itaandika Roaming na utaconect mnara wa Tigo.
Apn ni setting za internet ambazo mtandao wa simu unazisoma na kuzitumia kama gateway kukuunganisha na website na vitu vyengine unavyotumia. Hio mms, wap, web, internet etc ni mifano ya Apn.