Msiwasafirishe walimu kwa malori-CWT

kilimasera

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Messages
3,073
Points
1,225

kilimasera

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2009
3,073 1,225
AJIRA YA UALIMU SIJUI INA MKOSI GANI YAANI UKIPATA KAZI YA UALIMU UNAKUA MTU WA KUNYANYASIKA TU
ETI KARNE HII WAALIMU WANASAFIRISHWA KAMA MIZIGO NDANI YA MALOLI KWENDA KUSIMAMIA MITIHANI

CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT) wilayani Chamwino kimeitaka Idara ya Elimu katika
halmashauri hiyo isitumie malori kuwasafirisha walimu wakati wakiwapeleka kwenye vituo vya kusimamia mtihani wa darasa la saba unaoanza leo.

Mwenyekiti wa CWT wilayani humo, Amani Msanga alitaka yatumike mabasi au magari
madogo kufanikisha hilo.

Aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matayarisho ya mitihani hiyo katika wilaya yake.

Msanga alisema kuwa hali ya maandalizi ya mtihani huo wilayani humo, kwa kiasi kikubwa,
yamekamilika na kwamba kinachosubiriwa ni kuwasambaza wasimamizi hao katika vituo
walivyopangiwa.

Alisema asingependa kuona walimu hao wakibebwa kwenye malori badala yake, yatumike
mabasi au magari madogo.

Alisema kuwa kila mwaka wasimamizi wa mtihani wamekuwa wakibebwa katika malori kupelekwa kwenye vituo vyao vya kusimamia bila kujali usalama wa maisha yao.

"Kama wahusika wa maandalizi ya mtihani huu wameshatoa pesa kwa ajili ya kukodi malori,
tafadhali warudishieni pesa zao kwa kuwa walimu hawatapanda hayo malori," aliagiza
Msanga.

Msanga alisema kuwa malori ni kwa ajili ya kubeba mizigo na si kusafirishia watu kwani kwa
kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na kanuni za usalama barabarani.

"Kama walimu watalazimishwa kutumia malori hayo, wachukue namba za magari hayo na kupiga simu Polisi na naomba ushirikiano kutoka kwa Jeshi letu la Polisi," alisema.

Aidha Mwenyekiti huyo aliwataka watahiniwa kuwa makini katika kujibu mtihani wao ili
waweze kufaulu na kujiunga na kidato cha kwanza mwakani.
 

Forum statistics

Threads 1,390,292
Members 528,138
Posts 34,048,527
Top