Msitu wa mauzauza wa Hoia-Baciu Romania

Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
6,064
2,000
Nchini Romania, Kusini Magharibi mwa nchi hiyo, jirani na mpaka wa nchi ya German ndiko hupatikana msitu wa wauzauza wa Hoia-Baciu.

Tukiachana na msitu wa mauzauza wa Njombe tuliouzoea, msitu wa mauzauza wa Hoia-Baciu ni noma, hauna kuku wa maajabu, ila una maajabu ya kutisha. View attachment 1633433

Katikati ya msitu kuna eneo la mfano wa duara, hapo hapaoti miti na ndio panatajwa kwamba ni eneo la kushukia viumbe wa ajabu waitwao eliens ambao hutua eneo hilo kwa vyombo vyao visivyojulikana virukavyo angani.

View attachment 1632667

Msitu umepata jina lake baada ya bwana Hoia-Baciu mfugaji mahiri wa kondoo kuingia msituni kulisha kondoo wake 200, yeye na kondoo wake walimezwa na msitu na hawakuwahi kupatikana tena. View attachment 1633434

Miongoni mwa mauzauza ambayo yamekuwa takiwapata watu wanaotembelea msitu huo ni pamoja na :-
° Kupotea. Wengi wa wanaoingia msituni humo hupotea na hawarudi kabisa.

° Kupatwa na magonjwa ya ajabu. Kuna ambao walibahatika kutoka kwenye msitu wa Hoia-Baciu lakini walirudu na magonjwa ya ajabu.

Wapo waliopata upele ambao haujawahi kuonekana duniani,wapo waliopatwa na majeraha ya Moto, na wapo waliopatwa na kipandauso

Pia wapo waliopatwa kichefuchefu kikali. Msitu huu pia huitwa Bermuda of Romania. Waromania Ni mahiri kwa uchawi, ushirikina na utumizi wa nguvu za giza View attachment 1633435
Waromania ni Wachawi sana na wanaamini sana katika Uchawi. Nadhani katika Europe ndiyo wanaongoza katika mambo ya Uchawi. Serikali inawatamua na wachawi inawatoza kodi. Wao utasikia huyu ni mchawi kizazi cha tatu, sijui mchawi kizazi cha kwanza. Wana hadi vyama vyao na hawajifichi.

Mkuu ushawahi kuona movie inaitwa drug me to hell? Nahisi na Wahispania wanga sana
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
61,114
2,000
Waromania ni Wachawi sana na wanaamini sana katika Uchawi. Nadhani katika Europe ndiyo wanaongoza katika mambo ya Uchawi. Serikali inawatamua na wachawi inawatoza kodi. Wao utasikia huyu ni mchawi kizazi cha tatu, sijui mchawi kizazi cha kwanza. Wana hadi vyama vyao na hawajifichi.

Mkuu ushawahi kuona movie inaitwa drug me to hell? Nahisi na Wahispania wanga sana
Hatari sana
 

East Wind

JF-Expert Member
Jun 17, 2020
2,818
2,000
Wapo Uingereza, wanaishi kwenye makazi yasiyo rasmi, wengi huishi kwenye matrela ya kukokotwa na magari.
Wana hali duni, ila wanatunza asili yao
Awamu ingine ukienda uingereza nichukulie mmoja.. natanghliza shukrani zangu kwa kunifanikishia
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom