Msisitizo; CHADEMA kuna ombwe la uongozi

Msisitizo; CHADEMA kuna ombwe la uongozi

Juliana Shonza

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
2,009
Reaction score
1,607
Leo nitaanza bila salamu,
Ndugu wanajamvi, kwa siku za nyuma kidogo, takribani mwaka mmoja uliopita niliwahi kuandika hapa kuwa CHADEMA kuna Ombwe la Uongozi na nikasema katika maneno ya hitimisho la andiko langu hilo kuwa;
Moja ya sifa ya Mwerevu, ni yule ambae haumwi na nyoka mara mbili, anayejikwaa akaanguka kisha asiishie kuangalia alipoangukia bali hugeuka kwa umakini na kutazama alipojikwaa, ni nini hasa kimemuangusha..Popularity ya CHADEMA na Upinzani imeshuka na inaendelea kushuka kwa kasi, HAWAJIULIZI.

Viongozi wameacha kuchangia hoja za msingi ndani ya Vikao, wameshikwa na woga na wengine wamesusa, Mwenyekiti Mbowe ambae Mimi binafsi nilishamuita ZERO tukiwa ndani ya Kikao changu cha Mwisho nikiwa KAMANDA wa CDM, ameendelea kwenda Mrama kwa kasi ya ajabu...kila jipya analoliamua ni baya kuliko la jana..

Nakumbuka vizuri, niliambulia matusi mengi kama ninavyotaraji hata leo pia. Kama nilivyosema wakati huo nitasema tena leo kuwa WATANZANIA wameshapoteza IMANI na chadema na uongozi wake. Wasomi, wanataaluma, na makundi mengine yenye influence kwenye jamii hawaiungi tena mkono chadema, nimeshangazwa hata bodaboda na machinga nao wanajitenga mbali na chadema.

Waandishi makini wameacha kabisa kuwaunga mkono chadema, hata wale ambao waliwaandika vizuri kwenye social media akina Mwanakijiji, Chahali na hata Pasco wamekuwa wakiwashushua kila uchao juu ya maamuzi yao na uelekeo wao.

Kwa mara nyingine tena, LEO umefanyika uamuzi mwingine wa kuchekesha na wenye kuudhi. Uamuzi unaoendelea kuthibitisha kuwa Uongozi wa CHADEMA umekosa dira, maono na hawana tafakuri sahihi juu ya mabadiliko ya wakati na namna bora ya kuendesha siasa za sasa. Walipodhani kuwa FEDHA zinaweza kuwa THINK TANK ya chama na kusahau BRAINS matokeo yake ndio haya, mnakosa strategic plan na mnaishia kughairisha mikakati bila sababu za msingi zenye kueleweka kwa watu na kupoteza influnce zaidi, actually hata wanachama wanawadharau kwa mwendo huu.

Labda ilikuwa utani, lakini UONGOZI wa chadema wanapaswa kufahamu kuwa Naibu Katibu Mkuu wao na wanachama wao 27 wako korokoroni hivi sasa kwa sababu ya mpango wao wa hovyo. Watu hawa tumaini lao ilikuwa ni kuungwa mkono lakini uongozi wao umewasaliti, umewatanguliza kama CHAMBO then mpango umeahirishwa. Lakini kuna vijana chungu mzima, ambao walikuwa driven na UKUTA wakajikuta wanamtukana Mkuu wa Nchi na Serikali yake nao wananyea debe wakati uongozi wao unaghairisha kiutani utani, opresheni iliowafikisha jela.

Hivi visingizio kuwa familia ya Nyerere imekutana na Lowassa na kumuomba, naomba nisitolee maelezo ila nitampigia simu personally msemaji wa familia hiyo Ndugu Makongoro ili ikiwezekana kesho ama keshokutwa afanye press, au aende Clouds au Efm kuthibitisha kuwa walikutana na Lowassa na kumuomba a-abort mpango mzima.

UKUTA chali, kama nilivyotegemea.

Jioni Njema...!!
 
Ni lini uliitakia mema CDM mara ya mwisho tena!? lengo lako ni kugonganisha siyo, umechelewa endelea kula makombo huko! Au wewe ni mmojawapo wa madracula wanyonya damu mliokosa damu ya kesho!!??

Salum Mwalimu siyo mjinga kama wewe akusikilize upuuzi wa kugonganisha!! Kama ni kesi umeambiwa viongozi 230 wana kesi katika mahakama mbali mbali. Would you mind to stop popping your nostrils to our leaders and CDM please!! You have no damn business with CDM.
 
Dada chuki ni mbaya sana katika maisha inakosesha baraka Na mafanikio umeondoka chadema waache chadema na mambo yao amani ya nchi aiwezi kuletwa Na ccm Bali pande zote mbili za upinzani Na watawala hekima ni Bora kuliko Mali nawapongeza chadema kwa kutumia hekima
 
Mnyika hii ni aibu, trh 17 baada ya kuongea na viongozi wa dini ulitoka hadharani na kutangazi dunia, kuwa pamoja na kuombwa na viongozi wa dini UKUTA uko palepale. Kauli ya mwenyekiti wako kuwa mumeombwa na viongozi wa dini ni dhihaka. Mliwadharirisha siku ya kwanza ya mazungumzo yenu leo mnajidai mmewaelewa ni aibu
 
Leo sijaona hoja yako Juliana!Ingawa ni kweli Mbowe anawepleka chaka wenzie lakini amefaya vema kutokushindana na dola!Sijamuelewa tu kutaka kuendeleza kwake ukuta mwezi october!Hapa kama amekosa washauri mie nitamshauri aachane na UKUTA, haulipi!Apoe kwanza, homa ya uchguzi iishe na serikali itekeleze majukumu yake then pengine watapata cha kukosoa!Lakini kwa sasa hakuna, na watz hawatawaunga mkonio
 
Usiku wa deni hauchelewi najua leo mtatubeza sana na kejeli juu tumejiandaa tar 1 sio mbali maandalizi yanaendelea
 
Hivi kuna anayeshabikia CHADEMA kwa sasa? Hakika hiki chama kimegeuka kuwa The Comedy ama Futuhi
 
Leo nitaanza bila salamu,
Ndugu wanajamvi, kwa siku za nyuma kidogo, takribani mwaka mmoja uliopita niliwahi kuandika hapa kuwa CHADEMA kuna Ombwe la Uongozi na nikasema katika maneno ya hitimisho la andiko langu hilo kuwa;

Nakumbuka vizuri, niliambulia matusi mengi kama ninavyotaraji hata leo pia. Kama nilivyosema wakati huo nitasema tena leo kuwa WATANZANIA wameshapoteza IMANI na chadema na uongozi wake. Wasomi, wanataaluma, na makundi mengine yenye influence kwenye jamii hawaiungi tena mkono chadema, nimeshangazwa hata bodaboda na machinga nao wanajitenga mbali na chadema.

Waandishi makini wameacha kabisa kuwaunga mkono chadema, hata wale ambao waliwaandika vizuri kwenye social media akina Mwanakijiji, Chahali na hata Pasco wamekuwa wakiwashushua kila uchao juu ya maamuzi yao na uelekeo wao.

Kwa mara nyingine tena, LEO umefanyika uamuzi mwingine wa kuchekesha na wenye kuudhi. Uamuzi unaoendelea kuthibitisha kuwa Uongozi wa CHADEMA umekosa dira, maono na hawana tafakuri sahihi juu ya mabadiliko ya wakati na namna bora ya kuendesha siasa za sasa. Walipodhani kuwa FEDHA zinaweza kuwa THINK TANK ya chama na kusahau BRAINS matokeo yake ndio haya, mnakosa strategic plan na mnaishia kughairisha mikakati bila sababu za msingi zenye kueleweka kwa watu na kupoteza influnce zaidi, actually hata wanachama wanawadharau kwa mwendo huu.

Labda ilikuwa utani, lakini UONGOZI wa chadema wanapaswa kufahamu kuwa Naibu Katibu Mkuu wao na wanachama wao 27 wako korokoroni hivi sasa kwa sababu ya mpango wao wa hovyo. Watu hawa tumaini lao ilikuwa ni kuungwa mkono lakini uongozi wao umewasaliti, umewatanguliza kama CHAMBO then mpango umeahirishwa. Lakini kuna vijana chungu mzima, ambao walikuwa driven na UKUTA wakajikuta wanamtukana Mkuu wa Nchi na Serikali yake nao wananyea debe wakati uongozi wao unaghairisha kiutani utani, opresheni iliowafikisha jela.

Hivi visingizio kuwa familia ya Nyerere imekutana na Lowassa na kumuomba, naomba nisitolee maelezo ila nitampigia simu personally msemaji wa familia hiyo Ndugu Makongoro ili ikiwezekana kesho ama keshokutwa afanye press, au aende Clouds au Efm kuthibitisha kuwa walikutana na Lowassa na kumuomba a-abort mpango mzima.

UKUTA chali, kama nilivyotegemea.

Jioni Njema...!!
Tafsiri ya ukuta ni mwisho wa kufikiri...Makonda,Tatizo kubwa la Mbowe ni kuanzisha hoja zisizo na ushawishi kwa wananchi baada ya kushindwa analialia....hadi leo asubuhi kulitoka taarifa kuwa wameahirisha wakaleta propaganda kukanusha,matokeo yake..,chali ndembendembe kifo cha mende...chaliiii!
 
Execuse zinazotolewa ndio zinaudhi zaidi, Siku kumi nyuma unasema tumekutana na Viongozi wa dini tumezungumza nao na mkasema kuwa UKUTA uko pale pale leo mnasema tumezungumza na Viongozi wa dini (kama vile ni kitu kipya) na kuongeza tumezungumza na familia ya Mwalimu Nyerere (haijawahi kutokeo) tumeamua Kughairisha UKUTA, sio kuvunja kabisa bali kughairisha eti wakitegemea kutakuwa na tension kama ya awali.

Hesabu mbofu sana hii
 
Ukuta umebaki maneno tu nyuma ya keyboard ni aibu sana kwa wanaojiita eti makamanda
 
Hizo research zako za kuwa machinga na bodaboda wameacha kuiunga mkono CHADEMA ulizifanyia wapi?

Na ulienda kwa hao watu ukiwa katika sura ipi maana asikwambie mtu ile kuwaruhusu machinga warudi kufanya biashara maeneo mliyowakataza kidogo mkarejesha matumaini ila wengi wao bado hawana imani na siasa ya chama chako wewe mtoa uzi.

Kiukweli napenda nikushauri urejee maneno alioyaongea Mbunge wa Chama chako Ndg Bashe alisema serikali inacheza muziki wa CHADEMA so lengo limetimia kwa asilimia nyingi sana nguvu walizotumia serikali kuhakikisha UKUTA never exist ni nyingi sana utadhani walikuwa wanapambana na watu wale wa Uturuki waliotaka kupindua nchi.

Juliana Shonza bado haujakomaa kisiasa kwa hizo tathmini zako zisizo na uhakika. Umeshhakuwa na uhakika wa chakula cha kila siku hapo ulipo hauna kashikashi ya aina yoyote kama ilivyo kwa upinzani ila hayo ulioyaandika wewe yakiandikwa kwa serikali inakuwa ni uchochezi.Ila time will tell

Machinga hawana imani na serikalo tena wala hao bodaboda hawana hiyo imani nanyi tena wanasubiri tu ikifika muda wa kuwahukumu kwenye mabox ya kupigia kura watafanya kile wanachokililia sasa hivi maana wanapitia wakati kgumu sana katika historia ya Tanzania.

Jifikirie upya kabla ya kuja na hizo blabla zako hata kama familia ya Mzee Nyerere hawajaongea na Lowasa ila kwa hatua waliyofikia CHADEMA ni nzuri sana katika kufanya siasa yaani mlikuwa mnawatangaza kwa wananchi bila kupenda katika majukwaa yenu ya siasa wao wapo Indirect kupitia vinywa vya wanasiasa wenu.

Usiwe mbeya sana hayo ya kumpigia simu huyo mtoto wa Mzee Nyerere wala sisi hayatuhusu.

Tunahitaji siasa safi na utawala bora unaofuata sheria na katiba ya nchi .
 
Back
Top Bottom