Msipotoshe, CCM haijatawala Miaka 50

Msipotoshe, CCM haijatawala Miaka 50

Binti Magufuli

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2011
Posts
7,479
Reaction score
5,160
Huu ndiyo ukweli na ni lazima tuuelezenchama cha mapinduzi hatujaongoza nchi kwa miaka 50 Iko hivi .

1--1961 tulipopata uhuru TANU ndiyo iliongoza Tanganyika na si Tanzania hadi 1977 ni miaka 16.

1964 zanzibar ilifanya mapinduzi matakatifu na ASP ndiyo iliingoza nchi .

2--1964 tuliunganisha nchi kuwa Tanzania lakini vyama viliongoza eneo lake na si chama cha mapinduzi .

3--1977 ndipo tuliunganisha vyama vya TANU na ASP na kuzaliwa CCM hivyo ccm iliiongoza tanzania toka 1977 hadi 1995 tulipofanya uchaguzi wa vyama vingi ni takribani miaka 18 tu na hao wanaojiita wapinzani wakiwemo ndani ya serikali yaCCM.

Hivyo hawana sababu ya kukwepa amma kuzusha amma kuongopa kua hawakuwemo amma kushiriki na kutoa michango yao kwa miaka 34 toka tupate uhurub1961 hadi 1995.

4--Baada ya uchaguzi 1996 ndipo CCM kwa kuaminiwa na wananchi tulikabidhiwa kuwaongoza na kuiongoza nchi ni miaka19 tu na si 50 kama inavyodaiwa na kupotoshwa na vyama na wanachama wa vyama vya upinzani Tanzania.

5--Kwa mtazamo wako kwa akili na busara usikubali kudanganywa na upotoshaji huu usio na tija wala faida hauna takwimu wala tafiti za kweli na za maana zilizofanyiwa kazi kwa umakini nao.

6--Hii ni kuthibitisha kua wanachama wa vyama vya upinzani hawapo tayari kuwaambia watanzania ukweli na kuukubali ukweli sababu wamezoea kupinga na kusema uongo daima.

7--Nawaomba na kuwashauri watanzania kuwa makini kutowasikiliza na kutowapigia kura 25 oktoba sababu nia na madhumuni yao hayapo wazi ni kututumbukiza katika matatizo makubwa.

8--Chagua kilicho bora chagua chama cha mapinduzi na viongozi wake kwa manufaa maendeleo na mustakabali mzuri wa taifa letu kwa amani utulivu upendo na maendeleo.

Mungu awabariki sana muwe na busara na hekima muchague chama cha mapinduzi kuanzia madiwani wabunge na raisi.

9--Mungu ibariki tanzania na watu wake tujaalie afya busara na hekima.

Imetengenezwa nami HALFAN SAIDI DOSI kada wa chama cha mapinduzi.
 
Mwendelezo ;
Umesahau na ndani ya miaka hiyo 19,
10) Sumaye amekuwa waziri mkuu kwa miaka 10, na 11)Lowasa kwa miaka karibu 3. Wakiwa kama wasimamizi wakuu wa shughuli zote za serikali.
12) ndani ya kipindi cha Sumaye, yeye ndiye aliidhinisha uuzwaji wa nyumba za serikali.
13) Richmond dili ilisimamiwa na Lowasa akiwa waziri mkuu
Naomba wengine waendeleze
 
Ulitaka ongea nin hapo mana hauleweki kabisaa
 
CCM ipo katika hatua za mwisho za urushaji mateke ya kukata roho,dalili ni nyingi,Push ups katika mikutano ya Siasa,Tafiti tata za Twawezwa na REJECT,Maandalizi kabambe ya Goli la Mkono,iga iga ya kauli mbiu,ahadi danganya toto zisizohesabika wala kutekelezeka,Kuandaa matamasha badala ya mikutano,nunua nunua ya Viongozi wasaliti na Wasanii mizigo wakati wana Mabadiliko ni Wananchi ambao hawanunuliki,sombasomba ya wanachama na wasio wanachama kwa malori na mabasi,honga honga ya fedha,kanga,vitenge,Tshirts na Kofia,kejeli na matusi kwenye majukwaa ya Siasa,kusambaratika kwa timu ya watu 32 ya Kampeni ya CCM,n.k!Wana UKAWA tunasema ‪#‎HapaZikaTu‬!..Lowassa TOSHA KABISA!!..Mwenyezi MUNGU atawaumbua kwa kila Ovu walipangalo!!!
 
CCM ikikuwepo toka Uhuru, nikuwa 1977 ilibadili jina kutoka TANU kuwa CCM.
Ndio maana hata Mali zote za TANU zilirithiwa na CCM,kama ingekuwa TANU ndio imekufa pale basi Mali zingekuwa zimerejeshwa kwa wananchi na ccm ingeanza a fresh kwa kila kitu.
Usitudanganye wakati hata watumishi waliendelea na nyazifa zao zilezile toka Tanu kwenda ccm
 
Hata kama ingetutawala wiki moja tu, bado kwa matendo ya muda wa Utawala wake, tunaiondoa madarakani!!
 
CCM ikikuwepo toka Uhuru, nikuwa 1977 ilibadili jina kutoka TANU kuwa CCM.
Ndio maana hata Mali zote za TANU zilirithiwa na CCM,kama ingekuwa TANU ndio imekufa pale basi Mali zingekuwa zimerejeshwa kwa wananchi na ccm ingeanza a fresh kwa kila kitu.
Usitudanganye wakati hata watumishi waliendelea na nyazifa zao zilezile toka Tanu kwenda ccm

Je mwaka 1961 kulikuwa na Chama cha CCM?
Ni kama vile Useme ukawa ilikuwepo tokea 2010 kwa kuwa tu vyama vya umoja huo vilikuwepo miaka hiyo.

Jiongezee
 
Miaka yote hiyo wananchi wameshuhudia Tembo wakiisha, Dhahabu inatoweka, almasi kwishnei, Gas nayo wanalazimisha iwanufaishe wazungu ... CCM kizazi cha nyoka
 
Kimfumo inafika kwani kulikuwa ni muendelezo wa sera zilezile ila majina ya chama yalikuwa yanabadilika tu
 
Binti Magufuli, sasa tuna miaka 54 ya Uhuru. Ni vyama vingapi vimebadilishana kutawala Tanzania?

Vv
 
Miaka yote hiyo wananchi wameshuhudia Tembo wakiisha, Dhahabu inatoweka, almasi kwishnei, Gas nayo wanalazimisha iwanufaishe wazungu ... CCM kizazi cha nyoka
Kama ccm kizazi cha nyoka mbona watoto wake ndio tumewapa usukani wanaendesha ukawa. Lowasa na Sumaye na kundi lao lililotoka ccm. Sasa sisi tunajipambanuaje? ? Embu tuanzie hapo! !
 
kwahiyo hatujawahi kutawaliwa na mkoloni kwa vile tunaitwa Tanzania sasa?????kwa minajili hiyo ccm sio chama cha ukombozi kilichoitoa nchi yetu mikononi mwa mkoloni mzungu????

Binti Magufuli analeta hoja duni mno kiasi kwamba huenda akasababisha ama thread yake itupiwe kapuni kwa sababu ya milipuko ya wachangiaji au watu wapigwe ban humu ndani.

Vv
 
Miaka yote hiyo wananchi wameshuhudia Tembo wakiisha, Dhahabu inatoweka, almasi kwishnei, Gas nayo wanalazimisha iwanufaishe wazungu ... CCM kizazi cha nyoka
Katika miaka 19 ccm iliyatawala, miaka 10 alitawala Sumaye na miaka 2 na ushee alitawala Lowasa katika nafasi ya uwaziri mkuu. Embu tuambie matendo gani waliyofanya katika kuzuia maufisadi hayo. Kwa mifano. Kwa sababu yalifanyika wakati wakiwa madarakani. Au na wao walishiriki katika maufisadi hayoo? ?
 
Huo ndio ukweli hao wawili ndio waliyoimaliza nchi hii Leo wanawasingizia ccm haijafanya kitu wakati wao ndio waliovurunda nchi hii hiyo miaka 19 moja kakaa miaka 10, mmoja 3, wanafiki masikini nawaonea huruma watu wafata mkumbo tu kiza kinene kipo mbele yao
 
Back
Top Bottom