Msingi wa Taifa kwanza hujengwa kwenye mioyo ya watu

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,655
Kijana anapokua anatakiwa kutayarishwa ili akue kiakili . Aweze kutimiza majukumu yake katika familia yake lakini pia aweze kutimiza majukumu katika jamii yake na taifa lake.

Ni wajibu wa jamii kutengeneza raia wanaowajibika kwa taifa lao. Jamii inaposhindwa kutimiza haya itashindwa kujenga taifa imara.

Ni wajibu wa jamii kujenga raia wanaojitambua. Kwasababu bila kujitambua kwa raia wetu ni kazi ngumu kwa taifa letu kuendelea.

Swali la kujiuliza tunawatayarishaje vijana kuingia katika mambo yote haya? Kutoka katika utoto wao, ujana wao hadi kuingia katika jamii , katika familia na mahusiano yake na jamii na taifa, akiwa anajitambua na akiwa anajua wajibu wake? Elimu yetu inasaidiaje katika kujenga hili?


Nchi yetu imekosa hivi vitu na bila ya hivi hatutaweza kuendelea. Tunahitaji kujenga kujitambua kwanza. Bila kujitambua huku hatutakuwa na mwelekeo kama taifa. Huu ndio msingi ambao tunapaswa kuujenga kwanza. lTunapaswa kuijenga Tanzania katika mioyo ya watu.

Tanzania inapoharibika ni sababu watu wameharibika. Nchi hujengwa kwanza ndani ya watu. Ndani ya akili na mioyo ya watu. Alafu mambo mengine yanafuata.

Msingi wa kwanza hujengwa kwenye mioyo ya watu. Watu wanapokubali kujitolea kwaajili ya taifa lao ndipo taifa hilo huendelea. Nchi haijengwi kwa watu wabababishaji inajengwa na watu wanaojua wanachokifanya na wenye maono ya mbali.

Watu wetu wanatakiwa kuamshwa kutoka usingizini na kuwafanya kuwa na malengo na ndoto kwa taifa lao. Kwasababu wana uwezo huo. Wanaweza kulifanya taifa hili kuwa kubwa kama wakiamua. Kuna mifano mingi sana ya mataifa yaliyokuwa madogo lakini kwa juhudi na maarifa ya watu wao yalinyanyuka na kuwa mataifa makubwa duniani. Hili linawezekana na liko chini ya uwezo wetu. Linahitaji juhudi tu ya pamoja na kujitolea. Na kiongozi mwenye akili na maono.

Sioni kama tutashindwa kama tutakuwa na maelewano na kama tutakuwa wamoja. Kama tutakuwa na fikra moja juu ya ujenzi wa taifa hili hatutashindwa. Tatizo ni ubinafsi wetu ambao unaturudisha nyuma na kutufanya tusiendelee.
 
Back
Top Bottom