Mwanga Lutila
JF-Expert Member
- Nov 10, 2016
- 4,138
- 13,826
Wasalaam,
Miezi ya 4 mpaka wa 10 ndio miezi ya watu kufunga ndoa na pilika pilika za harusi.
Na ndio miezi ambayo huwa na ugomvi na kuchukiana kwa sababu ya wingi wa Kadi za harusi mpaka inageuka kuwa kero, mtu mmoja ambaye ni wa 'kucheka cheka na watu' anajikuta ana kadi za harusi zaidi ya tano.
Mimi binafsi mpaka sasa nina kadi nne, Kadi moja ni ya Sendoff, mchango Elfu hamsini, Kadi tatu za harusi mbili ni Elfu hamsini na nyingine Laki.
Na mwingine aliniletea huyu naye ilikuwa Laki moja, nikamwambia Bwana Chukua hii Elfu 20 itawasaidia kuongeza bajeti na kadi yako nenda nayo maana hali ni ngumu.
Hawa wengine sikuweza kuwakatalia kwasababu ni 'wanyalukolo' hivyo ingepelekea kununiwa mwaka mzima.
Kwa kifupi huu ndio muda wa kero za michango kuanza. Wengine unaweza kuwakwepa na wengine huwezi kuwakwepa.