Michango ya harusi imekua kero kwangu, mbona mimi sikuchangisha mtu ata senti moja

Archnemesis 2-0

JF-Expert Member
Aug 25, 2024
566
1,164
Habari za kuchakarika wakuu,

Aisee hapa navyoandika nimeungwa kwenye magroup matatu ya harusi zinazokuja mwisho wa mwaka huu, 1 ni binti ndugu wa ukoo sio immediate family link kwa mababu huko, mmoja ni jamaa nilitinga nae job kabla sijahamia nilipo, mwingine jamaa tumesoma wote high school.

Me nilioa harusi ya kiislam very simple hawakuzidi watu 200 hv vyakula ilikua chai ya maziwa, tende, sambusa, kabab, cookies, kuku za kukaanga na juice za azam embe vichupa vidogo na maji vichupa vidogo na watu wote walikula na kubeba , eneo nyumba ya ndugu yake wife (hatukutaka ukumbi), kwa kifupi nilitoa 2M tu kufanikisha shughuli + mapambo, usafiri.

Kusema ukweli ukiangalia vzuri sku hz watu wanatumia michango kutafuta mitaji or else mana haiwezekani eti unaweka kiwango cha chini labda 100,000/=

Unakuta mtu hamjaongea kitambo hakuna ukaribu unashangaa simu imeita unapewa taarifa! punde umeungwa kwenye group watu wametiririka ma plege.

Mwezi uliopita kuna jamaa mwngine aliniunga kwenye group pledge kiwango cha chini 200,000 nikamwambia me ntakusupport laki akasema poa ila nilibanwa nikatuma 50k nikamwambia ingne ntamalizia. Asee simu zkawa za usumbufu nikawa simpokelei hadi sku naona status kaoa nikampa hongera akanilia buyu blue tick tu. Nikaja kuonana nae town ananipa attitude nkasema safi ndo imeisha hiyo ila najuta ata kwann nlituma 50 yani unamaind kisa sina? Na muda huo najua kabisa washkaji wetu wengine kweny hiyo circle hawakutoa kabisa.

Wadau mnaonaje hv inakuaje u force michango hivyo kwa jambo linalokuhusu ww na huyo mwenzio kwann utuwajibishe watu kutoa ma ahadi ya kishingo upande imradi tu tusigombane wakati hali yenyewe mambo kizungumkuti songombingo mafrekeche ya kutosha.

Kama hujajipanga kuoa si kausha kwanza, watu tuna support ila imekua too much imekua ni shuruti sasa dah, usipotoa unaonekana mbinafsi na haufungamani na jamii.

Sijioni nikiendelea kua mtoa michango sijioni kabisa kwanza in real sense nakuchangia kwenda kukojozana kwenye hotel honeymoon uko... Shabaash,!!
 
Haya mambo bhana! Kuna mtu mmoja kwa ofisi namfahamu alitengeneza group Iko na watu 500+ aiseee nikaona kabisa hapa mbona kama WIZI? na Binafsi sipendi michango ya Harusi ama sendoff! Natamani tubadilike, unataka sherehe fanya jambo moja! Kusanya hela yako 3-5m, alika watu wahudhurie party ndogo hapo home waje na zawadi basi. Japokuwa michango ni sehemu ya social networking
 
Plan yangu ya kuoa nimepanga watakao hudhuria harusi yangu ni wazazi wangu na ndugu watatu, wazazi wa mwanamke na ndugu zake 10 hakuna kuomba michango, wala hakuna habari za mziki na kukodisha kumbi za sherehe ndoa inafungwa Asubuhi hadi saa 12 kila mtu anarudi kwake.
 
Kuchanga siyo lazima ni kuwa na msimamo tu
sahihi.

mdogo wangu alinibana kwenye sherehe yake, ikabidi nitenge saa nzima la kumpatia elimu. alielewa ama hakuelewa atajua mwenyewe!

kama mtu anataka ufahari wa dunia hii akamsujudie ibilisi, ataupata! kuna haya ma-secret societies ya kisheitwani, ila hatima yake atakuja kujua kuwa hajui.

Mathayo 4 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁸ Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake,
⁹ akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom