Msimlaumu Mbowe, ni hulka yetu kama Profesa Shaba&Co.!

Msimlaumu Mbowe, ni hulka yetu kama Profesa Shaba&Co.!

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,584
Reaction score
27,838
Mbowe ingawaje simjui zaidi ya kumsoma na kumuona kwenye vyombo vya habari, lkn najua kwamba ameng'ang'ania Uongozi wa chadema na kwamba sababu anazotoa yeye pmj na watu wake n kwamba bila ya yeye chadema itaanguka, yaani ameitoa mbali sana chadema hivyo kama akiondoka basi pia chadema itaondoka naye!

Mawazo haya siyo mageni hapa kwetu, inanikumbusha enzi hizo nakuwa kulikuwa na Madaktari tuliowaita bingwa kama vile Shaba, Mzee Sarungi &Co. hawa ndo tuliokuwa tunawaita mabingwa wa sijui mifupa, sasa walikuwa wanajiona kwamba wao ndo wao na bila ya wao hakuna bingwa wa mifupa TZ, na hata walikuwa wanakataa ku-recruit au wanasabotage kwa makusudi kabisa ujio wa wengine kwa maana walitaka Umungu mtu kwamba wabakie wao tu.

Hivyo hata Mbowe ni hivyo amejiaminisha kwamba chadema inamuhitaji yeye tu na bila uwepo wake basi haiwezekani, siajabu hata anaficha ujuzi alio nao wa jinsi ya kuiendesha chadema kwa walio chini yake ili tu abakie yeye tu, na kuabudiwa yeye tu, lkn kama walivyo akina Shaba, Sarungi, Mbowe &Co. wanashindwa kuelewa jambo moja, fahari ya kitu ni kuona ulichokianzisha au kukisaidia kukua kinapata mrithi na kuendelea kunawili na siyo fikira zenu potofu kwamba fahari ni kubakia wewe tu na kuabudiwa forever!

Binafsi siyo big fan wa Mlw. Nyerere ila kwenye hili namkubali na kumsifu kwamba aliliona hili, na matokeo yake tunayaona yeye haupo lkn CCM ipo, strong and powerful as ever Mbowe hauna cha kujifunza hapo? Acha ubinafsi , ...

*Nimetumia jina Sarungi, Shaba kama mfano tu lkn sina uthibitisho wowote, hivyo usiniletee!
 
Hivi nyie maccm na lichama lenu lichafu, mbowe na chadema inawahusu nini?
Wote wanaong'ania Mbowe aachie uongozi ni maccm...
Hebu pambaneni na hali zenu huko lumumba nyie mazwazwa!!
 
Back
Top Bottom