Msimharibie Rais Samia Suluhu

Thadei Ole Mushi

Verified Member
Oct 13, 2018
28
100
Na Thadei Ole Mushi.

Siku zote Marais wanapoingia madarakani huingia wakiwa Safi kabisa ni sawa na mtu anayepewa Karatasi jeupe achore au aandike yale aliyonayo kichwani.

Magufuli alipoingia madarakani Naye Alipewa Karatasi task Nyeupe. Kilichofanyika waliokuwa wamemzunguka walifanikiwa kuchukua kalamu yake nao wakachora na kuandika yao kwenye Karatasi aliyokuwa nayo JPM.

Jambo kubwa waliokuwa wamemzunguka walichofanya ni kumwaminisha JPM kuwa Jamii ya wachaga hawafai kabisa. Walipambana haswa ili aamini hilo kuwa Jamii hiyo haifai kabisa.

Kwa Sasa kuna watu nao wanataka ku- hack karatasi ya mama SAMIA na kinachoimbwa SASA ni kwamba kuna kitu kinaitwa SUKUMA Gang. Kila mahali sasa wanye agenda hii wanataka tuwachukie Wasukuma

Linalofanyika SASA lilifanyika pia kwa wachaga kuanzia 2015. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema "Dhambi ya ubaguzi ni kama kula Nyama ya Mtu, huwezi kuacha" yaani baada ya kuwabagua Wachaga SASA tunaenda kuwabagua wasukuma na baada hilo atakayekuja Naye atachagua wengine.

Nimuombe Mama SAMIA, Kusikiliza kila mtu, lakini kwenye kuamua amshirikishe Mungu tu. Msimsaidie Kuandika kwenye Karatasi ya Mama SAMIA, msimchafulie Karatasi yake.

Dhambi ya Ubaguzi ni mbaya sana. Kwa Miaka mitano iliyopita nilihukumiwa Sana kwa uchaga wangu kila nilipojaribu kutoa mawazo yangu.

Je hiki kinachoitwa SUKUMA Gang ni Kweli kipo? Kama kipo tunashughulika nacho vipi? Kama hakipo kwa nn tunalazimisha kiwepo?

Kama tunataka kuliponya hili Taifa tumsaidie mama Samia kusema ukweli.

Ukweli ni kwamba wanaobeba agenda hizi za Ubaguzi ni watu wanaotaka kuingia kwenye system au ni watu ambao wapo kwenye system wanataka kumwaribia Kiongozi.

Agenda hii ikikomaa Kiongozi huweza kutoka kwenye kushughulika na mambo ya Msingi kwa maslahi ya Taifa akaanza kupigana Vita ya watu wengine bila kujua. Tukianza kutaja taja haya makabila tutagusa mizimu ya wazee wetu.

Ole Mushi
0712702602.
 
mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
2,027
2,000
Mkuu umeongelea jambo la muhimu mno katika mada yako. Ni kweli kabisa wakati wa awamu ya hayati JPM Wachaga walisimangwa sana kwa ajili tu ya kabila lao. Sasa linakuja hili la Wasukuma, sijui wenye ajenda hii wana nia gani!?

Umoja, mshikamano na utengamano wa kitaifa ni nguzo muhimu mno kwa ujenzi wa taifa letu. Mashabiki wa mambo ya ukabila ni watu hatari mno kwa mustakabali mwema wa taifa letu.
 
Babe la mji

Senior Member
Dec 14, 2019
108
250
Wewe jamaa no mchumia tumbo tu maana Kila siku ulikua unasema, Hayati JPM aongezewe muda wa kutawala kwa kubadilisha katiba. Sababu eti hakuna Kama yeye nchi hii.unafaa kufungwa kabisa jela.

Kuanzia kipindi nilikuona mpuuzi ,manake kuvunja katiba kunaweza Leta hata Vita.

Punguza uchumia tumbo itakua mchambuzi mzuri.
 
Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
14,657
2,000
Mkuu umeongelea jambo la muhimu mno katika mada yako. Ni kweli kabisa wakati wa awamu ya hayati JPM Wachaga walisimangwa sana kwa ajili tu ya kabila lao. Sasa linakuja hili la Wasukuma, sijui wenye ajenda hii wana nia gani!?

Umoja, mshikamano na utengamano wa kitaifa ni nguzo muhimu mno kwa ujenzi wa taifa letu. Mashabiki wa mambo ya ukabila ni watu hatari mno kwa mustakabali mwema wa taifa letu.
Wakati wasukuma wakijiona Miungu watu mlikemea? Wasukuma wote walitamani hata Tundu Lissu akamatwe Awambwe Msalabani. Kisa tu anakosoa sera mbovu za mtu wao.
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
45,122
2,000
Mpuuzi wewe mbona hukuandika kipindi dikteta yupo hai? muda wote ulikuwa unasifia unatafuta uteuzi. Shame on you
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
45,122
2,000
Wewe jamaa no mchumia tumbo tu maana Kila siku ulikua unasema, Hayati JPM aongezewe muda wa kutawala kwa kubadilisha katiba. Sababu eti hakuna Kama yeye nchi hii.unafaa kufungwa kabisa jela.

Kuanzia kipindi nilikuona mpuuzi ,manake kuvunja katiba kunaweza Leta hata Vita.

Punguza uchumia tumbo itakua mchambuzi mzuri.
Huyu mzee ni mpuuzi sn mkuu, alikuwa anashangilia mateso ya watu.
 
mgaka12

JF-Expert Member
Mar 19, 2017
443
1,000
Mr Ole Mushi zamu zenu bado jipangeni kusifia au kukashifu mitandaoni hakutowaletea faida yoyote
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom