Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,483
- 40,011
Ameanza Spika na sasa kaja Mwanasheria Mkuu; na sitoshangaa baadaye atakuja waziri Mkuu na Rais au squadi zima la viongozi walioshindwa. Ati wanataka Zitto agombee wanakotaka wao! Kwa ubavu gani walio nao na kwa heshima gani?
Zitto kama Mtanzania mwingine anaweza kugombea mahali popote katika Muungano wetu na wananchi wa eneo hilo ndio watakuwa waamuzi. Mwacheni Zitto agombee anakotaka kugombea haitaji kibali wala baraka kutoka kwenu. Kama mnataka kumshauri zungumzeni naye pembeni.. hivi na yeye akianza kuwachagulia mgombee au msigombee si itakuwa ugomvi? (inawezekana ana sababu kubwa kweli ya nyinyi kutokugombea na sitoshangaa wananchi wakamsikiliza)..
Mwacheni achague mwenyewe; vinginevyo na sisi wengine tuna ushauri kama mnastahili hata kuwepo hapo Bungeni; viongozi mlioshindwa, mabingwa wa porojo, magwiji wa utani, na mahiri wa kutokuwajibika! Mnajiinua kana kwamba taifa zima linahitaji baraka zenu ili tufanikiwe.. haliitaji.
Ni ushauri wa bure tu..