Elections 2010 Msimchagulie Zitto Jimbo; hamna hadhi hiyo!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Ameanza Spika na sasa kaja Mwanasheria Mkuu; na sitoshangaa baadaye atakuja waziri Mkuu na Rais au squadi zima la viongozi walioshindwa. Ati wanataka Zitto agombee wanakotaka wao! Kwa ubavu gani walio nao na kwa heshima gani?

Zitto kama Mtanzania mwingine anaweza kugombea mahali popote katika Muungano wetu na wananchi wa eneo hilo ndio watakuwa waamuzi. Mwacheni Zitto agombee anakotaka kugombea haitaji kibali wala baraka kutoka kwenu. Kama mnataka kumshauri zungumzeni naye pembeni.. hivi na yeye akianza kuwachagulia mgombee au msigombee si itakuwa ugomvi? (inawezekana ana sababu kubwa kweli ya nyinyi kutokugombea na sitoshangaa wananchi wakamsikiliza)..

Mwacheni achague mwenyewe; vinginevyo na sisi wengine tuna ushauri kama mnastahili hata kuwepo hapo Bungeni; viongozi mlioshindwa, mabingwa wa porojo, magwiji wa utani, na mahiri wa kutokuwajibika! Mnajiinua kana kwamba taifa zima linahitaji baraka zenu ili tufanikiwe.. haliitaji.

Ni ushauri wa bure tu..
 
Wengine hao presha juu, wanahofu anaweza kugombea kwenye majimbo yao, na wakadhalilika!
Huyu dogo wanamwelewa kuwa ni tishio, ndio maana bila aibu wanajifanya washauri wake, na kubwabwaja kwenye vyombo vya habari!
Mimi nami ngoja niingie kwenye list ya 'WASHAURI", kwa kumwambia ..afanye utafiti na ajiridhishe mwenyewe, na pia awasikilize washauri wake, na si kila mwanasiasa mwenye kihoro!
 
Ni kweli Mwanakijiji lakini kule kwetu Tanganyika tunamuhitaji pia. Hao CCM watafurahi sana ikiwa Zitto atagombea Jimbo lingine nje ya Kigoma Kaskazini, ninafurahi kuwa NEC haijaliunganisha Jombo la Kigoma Kaskazini na Kigoma Mjini maana mpango ulikuwa ndo huo sijui wameshituka kitu gani hadi wameamua kuliacha Jimbo la Zitto huru.
 
Yeah lakini na yeye amezidi papara hawezi kuwa na jimbo zaidi ya moja
achague moja! kaka maji yamemfika shingoni sasa!

Uaminifu wake kwa wananchi unaleta mashaka
hasa anapoonyesha instability katika kuchagua
wape ashike!
 
Kusema kweli haitakuwa busara kumzuia Zitto kugombea apendapo maana wananchi ndio waamuzi. Pili Zitto mwenyewe atakuwa ana sababu zake za msingi zilizompelekea yeye akaamua kusema angependa kugombea sehemu nyingine zaidi ya jimbo lake la sasa. Labda kuna mafanikioa jimboni kwake anataka ayapeleke na huko kwingine au labda ameona huk kwingine hawandewi haki anataka kuwapigania kutoa mfano. Maana kama Geita Mkapa enzi zake alisema wawekezaji wangejena miundo mbinu yakiwemo mabarabara na mashule lakini barabara zote zimejengwa na serikali shule nazo hakuna la maaana.

Mwacheni Zitto aamue mwenyewe angependa wapi.
 
huyu kiajana naye anapiga siasa tu sio kwamba anaweza kwenda popote wakamkubali, maana hutamsikia hata siku moja azungumzie ufisadi maana jamaa wamemuonjesha vijisenti. Ukiangalia zito umaarufu ni ule wa mwanzo anaingia kabla jamaa hawajamnyamazisha na kwa sababu alikuja na moto mkali bado uko kwenye akili za watu. ukiangalia kiundani in last two year zito amesema nini bungeni ndo utaona kwamba bado anatumia umaarufu wa mwanzo. maana wamempa vipesa sasa dogo tajiri haawaachi kumgeuka na kumwambia amezipata wapi. hivyo yeye aende skahuko huko mean kigoma
 
Ina maana mpaka sasa Zitto hajui (hana uhakika na) jimbo analotaka kugombea?
sidhani kama kuna mtu yeyote ana power ya kumchagulia Zitto jimbo, acha tu kila mtu aseme lakini mwamuzi ni Zitto mwenyewe
 
Huyo, kijana anaelekea kuvimba kichwa, hata asipogombea ni poa tu, ila uhuru ni wake. Angalizo, asibweteke maana safari bado ndefu.
 
Yeah lakini na yeye amezidi papara hawezi kuwa na jimbo zaidi ya moja
achague moja! kaka maji yamemfika shingoni sasa!

Uaminifu wake kwa wananchi unaleta mashaka
hasa anapoonyesha instability katika kuchagua
wape ashike!

zito mjanja.anawapoteza tu maboya maadau zake na kuwachanganya.ila mwenyewe anajua atagombea wapi.
 
huyu kiajana naye anapiga siasa tu sio kwamba anaweza kwenda popote wakamkubali, maana hutamsikia hata siku moja azungumzie ufisadi maana jamaa wamemuonjesha vijisenti. Ukiangalia zito umaarufu ni ule wa mwanzo anaingia kabla jamaa hawajamnyamazisha na kwa sababu alikuja na moto mkali bado uko kwenye akili za watu. ukiangalia kiundani in last two year zito amesema nini bungeni ndo utaona kwamba bado anatumia umaarufu wa mwanzo. maana wamempa vipesa sasa dogo tajiri haawaachi kumgeuka na kumwambia amezipata wapi. hivyo yeye aende skahuko huko mean kigoma

Jamaa anakubalika sehemu nyingi sana ndugu.Jana nilikuwa mahala watu wakawa wanadiscus sehemu ya yeye kugombania.nikawaulize akija arusha mta mpa wote kwa jumla wakaitika lazima wampe.SO, kijana bado anauza.
 
siasa za Tanzania zimekuwa za Kenya sasa lazma ukagombee kijijini kwenu la sivyo vigogo wanawika tena waziwazi pasipo na aibu!
 
Cha msingi nadhani ni kujua kaona mapungufu yepi huko anapotaka kwenda gombea, na je anakuja na mapya yepi kutatua hayo mapungufu. All in all, yu huru kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa mwakilishi wa jimbo lolote, provided yu'ayajua matatizo ya sehemu husika, nao wameridhia kuwakilishwa nae.
 
zitto ni kijana mwenye malengo ya mbali, nafikiri ndani ya muda mrefu anaweza kuja kugombea urais kwa hiyo lengo kuu ni kuonyesha kujali watu wote
ndio maana anapenda kuunganisha watu wa vyama vyote na pia amejijengea marafiki wengi ndani ya serikali na siasa tunamtakia kila la heri
 
zito mjanja.anawapoteza tu maboya maadau zake na kuwachanganya.ila mwenyewe anajua atagombea wapi.

Hakika nilichokuwanawaza ndicho umekisema, kwamba ana akili sana japo awali nilimwona kama mpaparikaji tu,
Nimeona anawayumbisha maadui zake wa kisiasa wasijue mapema atagombea wapi ili wasiwezze kuweka mikakati ya kumboa kisiasa.

Nawasiwasi Zito ana agenda ya muda mrefu kuhusu siasa zake, pengine mbele ya safari ana mpango wa kugombea urais hivyo anaweka mazingira mazuri mapema
 
Tatizo la wengi wetu tuko dhidi ya Zitto kwa chuki binafsi. Zitto anaanza karne ya siasa mpya ambazo wengi wetu hawajazizoea... hapo ndipo panakuwa shida. Tukubali tu Zitto ni kijana mwenye kipaji ambacho kingeweza kufananishwa na Mwalimu miaka mwishoni mwa 1950s na 1960s wakati wakumuondoa mkoloni. Zitto ni mmoja wa mwiba kwa CCM! Tatizo tunampinga kwa wivu na chuki binafsi. Tu-m-support Zitto... anaglia move zake katika politics utajua Zitto ni wa aina yake. Amebadili siasa za bunge na sera za madini ameibana serikali... Kugombea popote ktk jamuhuri kutaondoa ukabila, uzawa, udini na kuimarisha utaifa. Kijana ni wa karne ijayao.... Kudos Zitto! Hii ni karne ya siasa wazi
 
Hili ndilo tatizo letu watanzania, tunataka watu wote wawe na mawazo sawa. Simply kwa kuwa mtu anapingana na vitu fulani na Zitto aimanishi ya kuwa ni chiki binafsi, bali kuna sababu za msingi anapingana naye.
 
Zitto mwenyewe ana hadhi na heshima hiyo ya kugombea popote nchi hii? Ni Mrema peke alifikia hadhi hiyo tangu enzi za akina Mwalimu na akina Amir Jamal na Derek Bryceson. Hakuna ngazi ya uongozi wa kuchaguliwa ambako UKABILA na PESA umejikita kama Ubunge. Na Zitto si mjinga hivo, analijua hili, anajinadi tu kwenye vyombo vya habari.
 
Back
Top Bottom