Msimamo wangu

Msimamo wangu

MSIMAMO WANGU

1. Changu ni changu, cha mume/mpenzi wangu tunashea.

2. Mwanaume bahili akae mbali na mimi.

3. Sina huruma na pesa ya mwanaume, labda atakaekuwa mume wangu wa ndoa.

4. Ntafanya majukumu yote kama mpenzi/mke wake, lakini when it comes to my money asahau, imeandikwa "mwanamke atazaa kwa uchungu na mwanaume atakula kwa jasho" so let him provide.

5. Ni marufuku mambo ya joint a/c eti mmoja wetu anaweza kutoa pesa pasipo saini ya mwingine sitaki.

6. Pesa zangu ni zangu ata password simpi, bora nimpe Mama yangu ata nikifa ajifutie nazo machozi.

7. Hata kama nina pesa kuliko yeye, mwanaume ni lazima awajibike, sio pesa yake awanufaishe wengine, maana kuna wanaume ndani wabahili ila nje wanahonga balaa.

8. Nyumba tutasaidiana kujenga, na itakuwa na jina langu na lake, au kama tutakuwa na watoto nao tutawaweka humo.

9. Ni marufuku ndugu wa mume kujihusisha na mali zetu, narudia tena ni marufuku ndugu wa mume kujisogeza karibu na mali zangu mm na mume wangu! Hizi haziwahusu kabisa tena mkae mbali.

NIMEMALIZA
Kazi ipo kwa kweli

Sent from my iDevice using Tapatalk
 
Yaani umecopy na kupaste kabisa halafu unasema ndio msimamo wako?? kweli JF haiishi vituko

Sent from my iDevice using Tapatalk
 
Nilipokuwaga mdogo nilimwambia baba aninunulie ndege, nilichokuwa namaanisha tofauti na kilichokuja.
Nikaenda kumsemea kwa mama, napo akanambia niteme mate kiganjani kwake, akamchape, cha kushangaza akapiga kochi, ila nayo nafsi yangu ikaridhika, ni maajabu kwa kweli.

sio lazima sa hivi utanielewa hata badae tuu, we endelea kumsubiria huyo mshkaji
 
MSIMAMO WANGU

1. Changu ni changu, cha mume/mpenzi wangu tunashea.

3. Sina huruma na pesa ya mwanaume, labda atakaekuwa mume wangu wa ndoa.

6. Pesa zangu ni zangu ata password simpi, bora nimpe Mama yangu ata nikifa ajifutie nazo machozi.

9. Ni marufuku ndugu wa mume kujihusisha na mali zetu, narudia tena ni marufuku ndugu wa mume kujisogeza karibu na mali zangu mm na mume wangu! Hizi haziwahusu kabisa tena mkae mbali.

NIMEMALIZA

Ahsante. Sina maswali ya nyongeza ndugu mheshimiwa.
 
Hupati mwaume kama kweli uliyoandika yako kwenye matendo ninakuonea Huruma watakutumia utachakaa
 
Ukionda mwanamke ana masharti mengi kiasi hiki ujue nimbaya wa sura mpaka umbo na pia amelelewa kwenye familia duni mno.

Hahahaaa. Uzuri maamuzi ya maisha au misimamo ni ya mtu binafsi, haina uhusiano na sura wala mazingira uliyonayo, inategemea sababu gani zimepelekea afikie hayo maamuzi.
 
Back
Top Bottom