View attachment 1463194
Huu ndio msimamo wangu. Sababu ipo wazi kabisa, sioni namna hata dalili kipande kwamba uchaguzi mkuu utakuwa huru na haki.Kama unaiona nionyeshe.
Kibaya zaidi serikali ya awamu ya tano imejipambanua kwa vitendo kutokufuata misingi ya kidemokrasia na hata sheria iliyojiwekea. Mnataka wafanye nini ili uamini? Hukushuhudia uchaguzi za mitaa,hushuhudii ukandamizaji wa viongozi wa upinzani?
Hukumsikia muheshimiwa akitamka wazi kuwa haiwezekani mkurugenzi alipwe mshahara,apewe nyumba na gari halafu mpinzani atangazwe mshindi. Kauli hii iliwahi kukanushwa?
Sitapiga kura uchaguzi mkuu
Heshima sana mkuu 'BOBAN SUNZU'.
Napenda uniruhusu nikushawishi ubadili hayo mawazo yako kwa heshima na taadhima, kwa sababu wewe ni kati ya watu wenye msimamo ninaowafahamu katika jukwaa hili la JF.
Sijui huu msimamo wako umeanza lini. Utakataje tamaa kwenye mapambano mkuu wangu, nani atapambana kwa niaba yako?
Kwa nini ujisalimishe kiasi hiki wanachokitafuta kwa kila njia CCM kitokee?
Pengine utanishangaa nikikueleza kwamba ni bora kabisa kujitokeza na kwenda kuwapigia CCM kura kuliko kuacha kupiga kura. Yes, it is as drastic as that!
Siku zote nimekuwa nikihimiza watu wenye msimamo kama wako wasiiangushe Tanzania.
Kutopiga kura ndio ushindi wa chee huo kwa CCM.
Kuna sababu gani ya kuwarahisishia kazi kiasi hicho?
Jitokezeni kwa wingi wenu, wengi zaidi ya asili mia tisini ikiwezekana.
Kapigeni kura mnavyoona nyinyi inafaa.
Mkisha fanya kazi hiyo kama hamtaki kushiriki kuhakikisha kura zenu zinahesabika kihalali, waachieni wengine wanaotaka haki zao zisipotee bure. Hawa watu wapo, na mtakuwa mmewapa sababu nzuri ya wao kujitokeza na kulinda haki zenu.
Kwa nini hata hawa mnawakatisha tamaa?
Hawa watasaidia kuhakikisha ushahidi upo wa kura zenu za kuwakataa CCM ndani ya box la kura; kwa sababu kura hizo zitakuwemo.
Kama hazimo kwa sababu ya kususia kwenu ushahidi watautoa wapi wa kuendeleza mapambano?
Licha ya hayo mapambano yatakayoanzishwa kwa kuzitegemea kura zenu kama ushahidi wao, hao wezi wa CCM wenyewe wataogopa kufanya lolote ovu kwa wingi wa kura zenu mlizopiga kuwakataa, na ulimwengu mzima utakuwa unajua hata wakilazimisha kubaki madarakani kwa nguvu.
Kutojitokeza kwenu ni ushahidi kwao kwamba wananchi wameridhika na yaliyopo, na dunia nzima haiwezi kupinga hilo!
Mkuu BOBAN SUNZU wewe unao uelewa mkubwa wa haya mambo. Huwezi kamwe kukimbia mapambano kwa njia hii ya kumhalarisha adui yako.
Nakuomba ulipo uwe kiini cha mabadiliko.
CCM wametuvuruga sana, hasa chini ya uongozi huu wa Mh Magufuli.
Kuachia hali hii iendelee kwa miaka mingine mitano au zaidi ni kuiumiza Tanzania tunayoipenda sote.
Kumbuka, hakuna atakayekuja nyumbani kwako kukuhoji kwa nini umepiga kura.
Nenda kapige kura vyovyote uonavyo wewe inafaa.
Huku ndiko kutakakokuwa mchango wako katika mapambano haya.
Usiache kuwa mshiriki katika kuleta mabadiliko Tanzania.
Shiriki kwa kadri uwezavyo, hata kama huoni kuwa kushiriki kwako huko kutasaidia kuleta mabadiliko.
Polisi hatakuja kukupiga mabomu kwa kupiga kura tu basi, na kuwaachia wengine wailinde kura yako.
Nitafurahi kusikia kutoka kwako juu ya jambo hili mhimu sana kwa nchi yetu.