Msimamo wangu: Sitapiga kura Uchaguzi Mkuu

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,176
103,656
EZO679CWoAAmg1O.jpeg

Huu ndio msimamo wangu. Sababu ipo wazi kabisa, sioni namna hata dalili kipande kwamba uchaguzi mkuu utakuwa huru na haki.Kama unaiona nionyeshe.

Kibaya zaidi serikali ya awamu ya tano imejipambanua kwa vitendo kutokufuata misingi ya kidemokrasia na hata sheria iliyojiwekea. Mnataka wafanye nini ili uamini? Hukushuhudia uchaguzi za mitaa,hushuhudii ukandamizaji wa viongozi wa upinzani?

Hukumsikia muheshimiwa akitamka wazi kuwa haiwezekani mkurugenzi alipwe mshahara,apewe nyumba na gari halafu mpinzani atangazwe mshindi. Kauli hii iliwahi kukanushwa?

Sitapiga kura uchaguzi mkuu
 
Mimi hata sifuatilii habari za uchaguzi,naapa kutoka sakafu ya koyo wangu katika maisha yangu yote yaliyobakia bila tume huru sitakanyaga kwenye kituo chochote cha kupiga kura!
 
View attachment 1463194

Huu ndio msimamo wangu. Sababu ipo wazi kabisa, sioni namna hata dalili kipande kwamba uchaguzi mkuu utakuwa huru na haki.Kama unaiona nionyeshe.

Kibaya zaidi serikali ya awamu ya tano imejipambanua kwa vitendo kutokufuata misingi ya kidemokrasia na hata sheria iliyojiwekea. Mnataka wafanye nini ili uamini? Hukushuhudia uchaguzi za mitaa,hushuhudii ukandamizaji wa viongozi wa upinzani?

Hukumsikia muheshimiwa akitamka wazi kuwa haiwezekani mkurugenzi alipwe mshahara,apewe nyumba na gari halafu mpinzani atangazwe mshindi. Kauli hii iliwahi kukanushwa?

Sitapiga kura uchaguzi mkuu
Ni haki yako
 
Kususia uchaguzi sioni kama ni njia nzuri.

Nenda kwenye uchaguzi, shiriki, wakifanya ujinga wao dunia nzima itajua, hapo ndipo mtapata foundation ya malalamiko yenu, wapo waangalizi, kususia maana yake nini? na 2025 tena mtasusa ....2030 mtasusa, sasa nini maana ya kuwa chama cha siasa?

Kama Katiba imeshindikana bora mkalime tu, siasa acheni.
 
Mkuu hata Mimi mara ya Kwanza na ya mwisho kupiga kura ilikuwa 2015.

Hata haya maboresho ya daftari Mimi hata sikujisumbua kwenda maana Sina ratiba ya kupiga kura uchaguzi ujao
 
Kutokupiga kura ni fahari ya CCM kwani wao wataagiza uchaguzi uendelee na kuna miaka mitano mingine ya taabu katika maisha yako.
Kauli njema ni kusema bila ya TUMEHURU utahakikisha unashirikiana na wengine UCHAGUZI USIFANYIKE.
Hilo linawezekana kabisa, kwa namna gani sio vema kuweka wazi sasa hivi muhimu NIA HIYO KUWEPO TUU
 
Kususia uchaguzi sioni kama ni njia nzuri.

Nenda kwenye uchaguzi, shiriki, wakifanya ujinga wao dunia nzima itajua, hapo ndipo mtapata foundation ya malalamiko yenu, wapo waangalizi, kususia maana yake nini? na 2025 tena mtasusa ....2030 mtasusa, sasa nini maana ya kuwa chama cha siasa?

Kama Katiba imeshindikana bora mkalime tu, siasa acheni.
Ahaaaaa.
 
Naunga mkono hoja. Ndo kusema ,kupiga kura ilihali unamjua mshindi Ni Ujinga. Mimi siji kupiga kura Tena.
 
View attachment 1463194

Huu ndio msimamo wangu. Sababu ipo wazi kabisa, sioni namna hata dalili kipande kwamba uchaguzi mkuu utakuwa huru na haki.Kama unaiona nionyeshe.

Kibaya zaidi serikali ya awamu ya tano imejipambanua kwa vitendo kutokufuata misingi ya kidemokrasia na hata sheria iliyojiwekea. Mnataka wafanye nini ili uamini? Hukushuhudia uchaguzi za mitaa,hushuhudii ukandamizaji wa viongozi wa upinzani?

Hukumsikia muheshimiwa akitamka wazi kuwa haiwezekani mkurugenzi alipwe mshahara,apewe nyumba na gari halafu mpinzani atangazwe mshindi. Kauli hii iliwahi kukanushwa?

Sitapiga kura uchaguzi mkuu
Heshima sana mkuu 'BOBAN SUNZU'.

Napenda uniruhusu nikushawishi ubadili hayo mawazo yako kwa heshima na taadhima, kwa sababu wewe ni kati ya watu wenye msimamo ninaowafahamu katika jukwaa hili la JF.

Sijui huu msimamo wako umeanza lini. Utakataje tamaa kwenye mapambano mkuu wangu, nani atapambana kwa niaba yako?

Kwa nini ujisalimishe kiasi hiki wanachokitafuta kwa kila njia CCM kitokee?

Pengine utanishangaa nikikueleza kwamba ni bora kabisa kujitokeza na kwenda kuwapigia CCM kura kuliko kuacha kupiga kura. Yes, it is as drastic as that!

Siku zote nimekuwa nikihimiza watu wenye msimamo kama wako wasiiangushe Tanzania.
Kutopiga kura ndio ushindi wa chee huo kwa CCM.

Kuna sababu gani ya kuwarahisishia kazi kiasi hicho?

Jitokezeni kwa wingi wenu, wengi zaidi ya asili mia tisini ikiwezekana.

Kapigeni kura mnavyoona nyinyi inafaa.

Mkisha fanya kazi hiyo kama hamtaki kushiriki kuhakikisha kura zenu zinahesabika kihalali, waachieni wengine wanaotaka haki zao zisipotee bure. Hawa watu wapo, na mtakuwa mmewapa sababu nzuri ya wao kujitokeza na kulinda haki zenu.

Kwa nini hata hawa mnawakatisha tamaa?

Hawa watasaidia kuhakikisha ushahidi upo wa kura zenu za kuwakataa CCM ndani ya box la kura; kwa sababu kura hizo zitakuwemo.

Kama hazimo kwa sababu ya kususia kwenu ushahidi watautoa wapi wa kuendeleza mapambano?

Licha ya hayo mapambano yatakayoanzishwa kwa kuzitegemea kura zenu kama ushahidi wao, hao wezi wa CCM wenyewe wataogopa kufanya lolote ovu kwa wingi wa kura zenu mlizopiga kuwakataa, na ulimwengu mzima utakuwa unajua hata wakilazimisha kubaki madarakani kwa nguvu.

Kutojitokeza kwenu ni ushahidi kwao kwamba wananchi wameridhika na yaliyopo, na dunia nzima haiwezi kupinga hilo!

Mkuu BOBAN SUNZU wewe unao uelewa mkubwa wa haya mambo. Huwezi kamwe kukimbia mapambano kwa njia hii ya kumhalarisha adui yako.

Nakuomba ulipo uwe kiini cha mabadiliko.

CCM wametuvuruga sana, hasa chini ya uongozi huu wa Mh Magufuli.

Kuachia hali hii iendelee kwa miaka mingine mitano au zaidi ni kuiumiza Tanzania tunayoipenda sote.

Kumbuka, hakuna atakayekuja nyumbani kwako kukuhoji kwa nini umepiga kura.

Nenda kapige kura vyovyote uonavyo wewe inafaa.

Huku ndiko kutakakokuwa mchango wako katika mapambano haya.

Usiache kuwa mshiriki katika kuleta mabadiliko Tanzania.

Shiriki kwa kadri uwezavyo, hata kama huoni kuwa kushiriki kwako huko kutasaidia kuleta mabadiliko.

Polisi hatakuja kukupiga mabomu kwa kupiga kura tu basi, na kuwaachia wengine wailinde kura yako.

Nitafurahi kusikia kutoka kwako juu ya jambo hili mhimu sana kwa nchi yetu.
 
Nawakaribisha wakuu kwa mchango wangu hapo juu #19.

Najua ni haki yenu kutopiga kura; lakini kuitumia haki hiyo wakati kama huu ni kuisaliti nchi yetu bila wenyewe kutambua kuwa mnaisaliti.
Naunga mkono hoja. Ndo kusema ,kupiga kura ilihali unamjua mshindi Ni Ujinga. Mimi siji kupiga kura Tena.
Hapana mkuu, tafadhali badili msimamo
Kupiga kura afrika Ni usaniii
Hapana.
Kutopiga kura ni kuwaunga mkono CCM. Mwache CCM afanye "usanii" kwa kuichezea kura yako inayoweza kumtokea puani. Usipopiga kura umempa tiketi ya moja kwa moja kuendeleza usanii. Ni lazima pawe na mwanzo wa kuukataa usanii. Naomba unisome hapo #19.
Me nitahakikisha napiga kura yangu ila siwezi kumpa CCM mpaka nakufa.
Ahsante mkuu 'Bambala255', hayo ndio mapambano halisi.
Kwenda kupiga kura nchi hii Kwa sasa ni matumizi mabaya ya muda
Jaribu kunisoma mkuu 'Maketz',; hapo #19. Pengine hitimisho lako hili unaweza kuligeuza?
Kwa kuonesha hasira zaidi nitaendelea kuwakataa CCM Kwa njia ya kura
Asante sana, nadhani tunaweza kuwasaidia wengi, kama akina mkuu 'Chibolo' kuongeza wingi wa jeshi letu
 
View attachment 1463194

Huu ndio msimamo wangu. Sababu ipo wazi kabisa, sioni namna hata dalili kipande kwamba uchaguzi mkuu utakuwa huru na haki.Kama unaiona nionyeshe.

Kibaya zaidi serikali ya awamu ya tano imejipambanua kwa vitendo kutokufuata misingi ya kidemokrasia na hata sheria iliyojiwekea. Mnataka wafanye nini ili uamini? Hukushuhudia uchaguzi za mitaa,hushuhudii ukandamizaji wa viongozi wa upinzani?

Hukumsikia muheshimiwa akitamka wazi kuwa haiwezekani mkurugenzi alipwe mshahara,apewe nyumba na gari halafu mpinzani atangazwe mshindi. Kauli hii iliwahi kukanushwa?

Sitapiga kura uchaguzi mkuu
Siku zote upigi lakini mabadiliko si unayaona nyie buku 7 kampeni yenu ya kuwavunja moyo watu ili msichezee kipigo inafahamika
 
Back
Top Bottom