Msimamo wa Kanisa Katoliki kuhusu uzazi wa mpango

Kuelewa kitu kipya wakati huo wewe binafsi unakitu chako unachokielewa basi itakuwa kazi sana kuelewa kile ambacho wenzio wanataka uelewe! Kanisa lipo sahihi kabisa na ni kwamujibu wa biblia
 
Mkuu kwahili JPM alikuwa sahihi ...
HE was totally wrong kwa kuwahadaa watu wake, huku akijua kwamba kila mtu anabeba msalaba wake, na kwamba serikali haina uwezo wa kuwahudumia watoto wanaozalishwa kama panya
 
Nijuavyo kanisa Katoliki linaruhusu uzazi wa mpango kwa kutumia njia za asili. Au, imebadilika? Nakumbuka mwanzoni mwa miaka ya 90 kwa msaada wa Fr. Lucas Mziwanda, aliletwa Sr. Brigta, nadhani alitokea Ndanda Mission Hospital ya kanisa Kikatoliki ambaye alikuwa daktari wa binadamu- MD kufundishisha njia za uzazi wa mpango kwa njia za asili ( kufuatilia ute unaotoka kwa mwanamke). Wakati huo nilikuwa nasoma IFM Dar.
 
Haijawahi kubadilika
..kanisa katoliki halikatai uzazi wa mpango bali linapendekeza njia sahihi na salama...
 
Mkuu ukisoma hilo bandiko Kanisa utaona uzazi wa mpango haukubaliki. Kama kumwaga nje mbegu ni chukizo kwa Mungu ni mbinu ipi itakuwa salama?
 
Kanisa lenyewe linawafundi waamini watiii mamlaka na hizo mamlaka ndizo Huweka uzazi wa mpango. Kikubwa kanisa likataa uuaji uzuiaji wa kiumbe kutokea kupitia uzazi wa mpango. Ikiwa baba atatengana na mama kwa muda kwa ajili ya kupanga uzazi kanisa halikatai lakini sio kwa mfano eti baba avae kondom au afanye vasektomi au mama ameze dawa huko ni kuzuia uumbaji. N.k.
 
Uko sahihi, Pro life Tz wanafundisha vzr kabisa cjui kwnn wanapotosha na kwa faida ya nan
 
Mkuu ukisoma hilo bandiko Kanisa utaona uzazi wa mpango haukubaliki. Kama kumwaga nje mbegu ni chukizo kwa Mungu ni mbinu ipi itakuwa salama?
Kulingana na mafunzo ya Sr. Brigita( MD), mbobezi katika masuala ya uzazi, hutakiwi kufanya siku za hatari. Kwa hiyo humwagi, unajizuia kufanya tendo la ndoa. Ute unaotoka kwa mwanamke unatabia zake ambazo unatakiwa kuzisoma na kuzifuatilia. Ni zoezi gumu kwa watu wanaotumia killevi na wale wa mfumo dume. Kufanisha njia hii inahitaji ushirikiano wa kutosha kati ya mke na mme. Na njia ya ute inaaminika sana hata kuliko ile ya kalenda na hata kondom.
 
Mkuu ukisoma hilo bandiko Kanisa utaona uzazi wa mpango haukubaliki. Kama kumwaga nje mbegu ni chukizo kwa Mungu ni mbinu ipi itakuwa salama?
Hii ni tafsiri yako wewe. Mambo ya kumwaga nje kuwa ni chukizo la MUNGU sababu tu kuna Mtu alikufa baada ya kufanya hivyo ni tafsiri yako wewe ya kifungu husika.Hata shetani alimjaribu YESU kwa kutumia kifungu cha Biblia, na alikitasiri kwa tafsiri yake yeye. Biblia hiyo hiyo inaelekeza kuwalea watoto katika njia ipasayo ili watakapokua wasiiache Kamwe. Sasa wewe tengeneza shule huku huna uwezo halafu uone kama hutakuza vibaka.
 
Asante sana mkuu. Andiko lako hili litatusaidia wengi.
 
Siku hizi dhambi zinategemeana na dhehebu lako au mapokeo ya kanisa husika? Sikuhizi kila dhehebu la dini limeainisha dhambi wanazozijua wenyewe huku kukiwa na utofauti mkubwa kati ya dhehebu moja na jingine.

Kama wewe una watoto wengi kama siafu pambana na hali yako usiwe kikwazo kwa waliamua kupanga uzazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…