Msimamo wa Kanisa Katoliki kuhusu uzazi wa mpango


TAJIRI MSOMI

TAJIRI MSOMI

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2014
Messages
243
Likes
191
Points
60
TAJIRI MSOMI

TAJIRI MSOMI

JF-Expert Member
Joined Jun 19, 2014
243 191 60
Kuelewa kitu kipya wakati huo wewe binafsi unakitu chako unachokielewa basi itakuwa kazi sana kuelewa kile ambacho wenzio wanataka uelewe! Kanisa lipo sahihi kabisa na ni kwamujibu wa biblia
 
M

mysterio

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2011
Messages
1,952
Likes
2,237
Points
280
M

mysterio

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2011
1,952 2,237 280
Mkuu kwahili JPM alikuwa sahihi ...
HE was totally wrong kwa kuwahadaa watu wake, huku akijua kwamba kila mtu anabeba msalaba wake, na kwamba serikali haina uwezo wa kuwahudumia watoto wanaozalishwa kama panya
 
M

mechard Rwizile

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Messages
1,465
Likes
695
Points
280
Age
62
M

mechard Rwizile

JF-Expert Member
Joined Sep 21, 2011
1,465 695 280
Hili ni jibu kwa swali lililoulizwa na muumini mmoja juu ya uzazi wa mpango.

Jibu; Katika mafundisho yanadhihakiwa na Wakristu wengi ni yale yanayohusu utumiaji wa njia za kisasa katika uzazi wa mpango. Wakatoliki wengi na kwa asimilia kubwa sana hudondoka hapa japo Kanisa limeweka bayana kuhusu jambo hili. Pia inasikitisha zaidi kwamba Kanisa Katoliki ndilo limeweka wazi fundisho lake. Madhehebu mengine huonekana kukubali utumiaji wa njia hizi ama huonekana kutokemea kana kwamba kuonea aibu. Hivyo Kanisa linabaki peke yake katika vita hii inayowashinda waumini wake wengi.

Lakini haikua hivi toka mwanzo. Mpaka mwaka wa 1930, Waprotestanti karibu wote walikubaliana na Kanisa Katoliki kuhusu fundisho hili. Kitu gani sasa kilitokea hadi mabadiliko? Mwaka huo wa 1930 ulifanyika mtukano wa kanisa la Anglikana (Uingereza) huko Lambethi na mkutano ukapitisha njia hizo za kisasa za uzazi wa mpango ziruhusiwe katika hali mbalimbali. Ikapita miaka mbele na jinsi msukumo wa dunia ulivyoendelea, utumuaji huo ukafika hadi kuhalalishwa na madhehebu mengi tu hadi hivi leo. Njia za kisasa za uzazi wa mpango zinatumika kwa amani tu na Wakristu. Hata ikafika wakati baadhi ya Maaskofu katika Kanisa Katoliki nao wakashawishika kukubali matumizi haya. Jambo hili likaleta mzogo mkubwa ndani ya Kanisa. Katika kuona haya, Baba Mtakatifu (Papa Mwenyeheri Paulo VI) katika barua yake (Human Vitae, 1968) kwa Maaskofu wote duniani yaani Encyclical akaweka msimamo katika fundisho la Kanisa kwamba halibadiliki na kila Mkatoliki akubali kwa ajili ya wokovu wa roho yake. Barua hii inasifiwa sana kwa utabiri wake kwani ilisema kuwa ndoa nyingi zitavunjika na familia kutengana kutokana na wingi wa matumizi ya vifaa hivi hapo baadaye. Ndio mambo tunayoyaona kipindi hiki

Kanisa Katoliki linafundisha kuwa utumiaji wa njia hizi za kisasa ni dhambi kubwa atendayo muumini. Biblia imefundisha hili pamoja na Mapokeo ya Mitume yaani Apostolic Tradition. Lakini kwanza tuangalie maelezo juu ya njia hizi.

Uzazi wa mpango kwa njia za kisasa maana yake ni njia mbalimbali ambazo binadamu kwa kusaidiwa na tekinolojia ama vifaa mbalimbali analenga kuzuia utunzi wa mimba ambayo inadhaniwa kuleta madhara ya aina moja ama nyingine. Hivyo binadamu anatafuta njia za kisasa kuzuia mpango wa Mungu na kuenda kinyume na kile alichopanga Mungu. Kwamba tendo la ndoa liweke wazi uwezekano wa mimba kutungwa na kuzaliwa mtoto. Vifaa hivyo basi vinapewa nguvu kubwa ya kumzidi Mungu kwa kumuamuru asitengeneze uwezekano wa mimba kutungwa. Hivyo nafsi inadhamiri kumzuia Mungu. Mtu aliyekusudia kukwepa mimba kwa mbinu yoyote anafikia kwa urahisi fulani uamuzi wa KUIUA. Hapa anakua haui mimba bali anakua ANAUA binadamu

Njia hizi za kisasa ni zipi?

Baadhi ya njia hizo za kuzuia uzazi ni: mipira kiume na ya kike yaani Kondomu, kufunga daima kizazi kwa upande wa mwanaume/mwanamke. Vingine vizuizi mimba ni Vidonge (Pills), Sindano, Poda, Vitanzi na Vipandikizi

Biblia inatufundisha nini juu ya hili jambo?

Uzuiaji wa mimba si jambo la kigeni bali toka enzi za mababu hata kabla ya Kristu, binadamu walitumia njia mbalimali kuzuia kizazi. Huko Misri, katika kipindi cha wakristu wa mwanzo palipatikana vitabu vilivyoonyesha matumizi ya njia hizi mbalimbali za kuzuia mimba zikiwamo pamba zinazonyonya mbegu za kiume, sumu inayoshambulia tumbo la kizazi(uterus), mipira ya kiume inayotengenezwa na ngozi za wanyama pamoja na njia nyingine ya kizuizi. Moja ambayo ni ya kitambo sana lakini hutumika mpaka hivi leo ni ile ya kumwaga mbegu za kiume nje ya tumbo la kizazi (Withdrawal). Njia hizi humkasirisha Mungu na ametupa mfano wa hasira yake katika kitabu cha Mwanzo cha Biblia. Tunamwona Onani mwana wa Yuda aliyeuawa hapo hapo kwa kumwaga mbegu nje ya tumbo la kizazi (Mwanzo 38). Kutokana na tamaduni za Kiyahudi, Onani alipewa amri ya kuendeleza kizazi cha kaka yake kwa kuzaa na mjane wa kaka yake. Lakini yeye alikataa hilo, akaamua kufanya starehe tu lakini asitoe mbegu za mtoto. Kuhusu yeye Biblia inaandika “……ikawa, alipoingia kwa mke wa nduguye, akamwagia chini asimpe nduguye uzao. Neno hili alilolifanya likawa baya machoni pa Bwana, basi akamwua yeye naye” (Mwanzo 38:9-10)

Cha kusikitisha, ili kuweza kuhalalisha dhambi, Wakristu hata baada ya kuona mfano huu, wanaubadilisha maana yake wakisema Mungu hakumwua Onani kwasababu ya kumwaga mbegu nje bali kwasababu ya kukataa kwake kuendeleza uzao wa kaka yake. Je, ni kweli hivi? HAPANA. Ukisoma kitabu cha Kumbukumbu la Torati 25:7-10, utagundua kuwa adhabu ya kukataa kuendeleza kizazi cha ndugu haikua kifo, bali ilikua ni kufanywa aibu kubwa mbele ya watu (Public Humiliation). Kitabu kinasema, baada ya mtu kukataa kulala na mjane wa ndugu yake ili aongeze kizazi, “......ndipo mke wa nduguye amkaribie mbele ya hao wazee, amvue kiatu chake mguuni mwake, na kumtemea mate ya uso..... Na jina lake katika Israeli liitwe, Nyumba ya mvuliwa kiatu (Kumbukumbu la Torati 25:9,10). Hivyo adhabu ilikua ni AIBU na sio KIFO. Lakini Onani yeye alipewa hukumu kali ya kifo kwa maana alimchukiza Mungu kwa tendo lake la kumwaga nje mbegu zake za kiume.

Kwa hali hii, Watakatifu Mababa wa Kanisa (Church Fathers) na wao hawakua mbali kukemea hali hii. Katika baadhi ya maandishi yao wanasema:

Mt. Clement wa Alexandria (Mwaka 191): “Kutokana na kuwekwa na Mungu aliye Mtakatifu, mbegu (ya kiume) haitakiwi kumwagwa nje (ya tumbo la kizazi), wala kuharibiwa na sio ya kutupwa” (The Instructor of Children 2:10:91:2)

Mt. Hyppolytus wa Roma (Mwaka 255): Akiwaandikia baadhi ya wanawake wakristu waliofanya uzinzi na watumwa/wafanyakazi wao anawaambia, “...wanatumia madawa ya kutengeneza utasa/ugumba ama wanajifunga kwa nguvu ili wafanikiwe kutoa kiumbe ambacho kimeshatungwa kama mimba tumboni mwao”

Mt. Agustino (Mwaka 419): Akiwaandikia wenye ndoa
wanaokutana kwa ajili tu ya starehe bila kuwa na nia ya kutengeneza mtoto anawaambia, “.....wale wanaofanya hivyo, japo wanaitwa mume na mke, hawaishi katika hali ya ndoa, bali wamebeba jina la aibu. Mara nyingine, tamaa hizo za mwili zinafika hadi kuwafanya watengeneze madawa ya ugumba na utasa”

Tofauti na Wakristu Waprotestanti wa siku hizi, inabidi Waprotestanti pia wakumbuke kua waanzilishi wa Uprotestanti kama Martin Luther walikemea sana tabia hizi ya uzuizi wa Mimba. Luther, akiongelea uovu wa Onani aliyeuawa na Mungu kwa kosa lake anasema “..Ni kosa kubwa la fedheha...Yeye (Onani) alistahili kuuawa na Mungu. Alifanya uovu mkubwa, hivyo Mungu akamwadhibu”

Naye Mprotestanti John Calvin, mwanzilishi wa kanisa la Presbetaria anasema kuhusu dhambi ya Onani “Jambo la kumwaga nje mbegu za kiume katika tendo la ndoa kati ya wawili ni jambo la uovu mkubwa. Kuuondoa uume nje ili mbegu zimwagike ni uovu mkubwa kwa maana tendo hili linaondoa tumaini la kizazi na kuua kabla hata ya kuzaliwa yule aliyetegemewa.

Naye mwanzilishi wa kanisa la Methodisti, John Wesley anasema kuhusu dhambi ya Onani, “..alichokifanya Onani, kilimuudhi Mungu na lazima (kitendo hicho) kiogopwe....kwa kuwa kitu hiki, bado kinamchukiza Mungu na kinateketeza roho (za watu)”

Sasa tunajiuliza, kama pia waanzilishi wa madhehebu hayo ya kiprotestanti makubwa ya Kikristu walikemea na kupinga njia hizi, kwanini Wakristu katika madhehebu hayo siku hizi wanakubali kutumia yale ambayo waanzilishi walikataza? Jambo la kutafakari

Mwisho kabisa, madhara yanayojitokeza siku hizi kutokana na matumizi hayo ni makubwa kwa taifa la Kristu. Madawa hayo yameongeza kwa kasi kubwa vitendo ya uzinzi na uasherati. Wana ndoa wengi kwa kuwezeshwa na vifaa hivyo wanatembea nje ya ndoa zao wakijua wanayo silaha tosha ya kutotengeneza mtoto nje ya ndoa. Matokeao ni ndoa kuvunjika na watoto kutekelezwa.

Vijana nao wamejiingiza katika ngono kwa kuwa hawana tena hofu ya kutengeneza mtoto kabla ya ndoa

Wanawake nje ama ndani ya ndoa wanageuzwa kuwa chombo tu cha starehe ambacho mwanaume anatumia kwa kijiridhisha muda wowote na tamaa zake

Source; Facebook page, idara ya uchungaji TEC, @ 2015
Nijuavyo kanisa Katoliki linaruhusu uzazi wa mpango kwa kutumia njia za asili. Au, imebadilika? Nakumbuka mwanzoni mwa miaka ya 90 kwa msaada wa Fr. Lucas Mziwanda, aliletwa Sr. Brigta, nadhani alitokea Ndanda Mission Hospital ya kanisa Kikatoliki ambaye alikuwa daktari wa binadamu- MD kufundishisha njia za uzazi wa mpango kwa njia za asili ( kufuatilia ute unaotoka kwa mwanamke). Wakati huo nilikuwa nasoma IFM Dar.
 
Aaron

Aaron

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2010
Messages
2,900
Likes
4,087
Points
280
Aaron

Aaron

JF-Expert Member
Joined Nov 18, 2010
2,900 4,087 280
Nijuavyo kanisa Katoliki linaruhusu uzazi wa mpango kwa kutumia njia za asili. Au, imebadilika? Nakumbuka mwanzoni mwa miaka ya 90 kwa msaada wa Fr. Lucas Mziwanda, aliletwa Sr. Brigta, nadhani alitokea Ndanda Mission Hospital ya kanisa Kikatoliki ambaye alikuwa daktari wa binadamu- MD kufundishisha njia za uzazi wa mpango kwa njia za asili ( kufuatilia ute unaotoka kwa mwanamke). Wakati huo nilikuwa nasoma IFM Dar.
Haijawahi kubadilika
..kanisa katoliki halikatai uzazi wa mpango bali linapendekeza njia sahihi na salama...
 
M

mechard Rwizile

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Messages
1,465
Likes
695
Points
280
Age
62
M

mechard Rwizile

JF-Expert Member
Joined Sep 21, 2011
1,465 695 280
Haijawahi kubadilika
..kanisa katoliki halikatai uzazi wa mpango bali linapendekeza njia sahihi na salama...
Asante sana, niliisha anza kufadhaika moyoni.
 
U

UKAWA2

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2014
Messages
2,115
Likes
1,559
Points
280
U

UKAWA2

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2014
2,115 1,559 280
Komaeni na New World Order, haya mengine yaacheni tu.
 
M

Mazindu Msambule

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Messages
5,456
Likes
2,788
Points
280
M

Mazindu Msambule

JF-Expert Member
Joined Feb 22, 2012
5,456 2,788 280
birth control and the new world order ambayo kanisa lenyewe ni muumini japo nyuma ya pazia.
Mkuu, nadhani wewe unalifahamu vizuri kanisa la RC, good!
 
MTAZAMO

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Messages
14,117
Likes
9,339
Points
280
MTAZAMO

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined Feb 8, 2011
14,117 9,339 280
Nijuavyo kanisa Katoliki linaruhusu uzazi wa mpango kwa kutumia njia za asili. Au, imebadilika? Nakumbuka mwanzoni mwa miaka ya 90 kwa msaada wa Fr. Lucas Mziwanda, aliletwa Sr. Brigta, nadhani alitokea Ndanda Mission Hospital ya kanisa Kikatoliki ambaye alikuwa daktari wa binadamu- MD kufundishisha njia za uzazi wa mpango kwa njia za asili ( kufuatilia ute unaotoka kwa mwanamke). Wakati huo nilikuwa nasoma IFM Dar.
Mkuu ukisoma hilo bandiko Kanisa utaona uzazi wa mpango haukubaliki. Kama kumwaga nje mbegu ni chukizo kwa Mungu ni mbinu ipi itakuwa salama?
 
mzamifu

mzamifu

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2010
Messages
4,172
Likes
1,343
Points
280
mzamifu

mzamifu

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2010
4,172 1,343 280
Kanisa lenyewe linawafundi waamini watiii mamlaka na hizo mamlaka ndizo Huweka uzazi wa mpango. Kikubwa kanisa likataa uuaji uzuiaji wa kiumbe kutokea kupitia uzazi wa mpango. Ikiwa baba atatengana na mama kwa muda kwa ajili ya kupanga uzazi kanisa halikatai lakini sio kwa mfano eti baba avae kondom au afanye vasektomi au mama ameze dawa huko ni kuzuia uumbaji. N.k.
 
S

Stella Stanford

Member
Joined
May 26, 2017
Messages
50
Likes
36
Points
25
S

Stella Stanford

Member
Joined May 26, 2017
50 36 25
Jamiiforums imevamiwa mnashindwa kutofautisha uzazi wa mpango wa kisasa na uzazi wa mpango....mleta mada unataka kuhalalisha kauli ya jpm ya kufyatua kwa kutumia hili andiko la kikatoliki.. Mimi ni mkatoliki na sikubaliani na njia za uzazi wa mpango wa kisasa...na kanisa halipi uzazi wa mpango bali unaelekeza njia sahihi za asili ambazo hazina madhara kwa ajili ya kupanga uzazi....hakuna sehemu kanisa linasema tufyatue bila mpangilio
Uko sahihi, Pro life Tz wanafundisha vzr kabisa cjui kwnn wanapotosha na kwa faida ya nan
 
M

mechard Rwizile

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Messages
1,465
Likes
695
Points
280
Age
62
M

mechard Rwizile

JF-Expert Member
Joined Sep 21, 2011
1,465 695 280
Mkuu ukisoma hilo bandiko Kanisa utaona uzazi wa mpango haukubaliki. Kama kumwaga nje mbegu ni chukizo kwa Mungu ni mbinu ipi itakuwa salama?
Kulingana na mafunzo ya Sr. Brigita( MD), mbobezi katika masuala ya uzazi, hutakiwi kufanya siku za hatari. Kwa hiyo humwagi, unajizuia kufanya tendo la ndoa. Ute unaotoka kwa mwanamke unatabia zake ambazo unatakiwa kuzisoma na kuzifuatilia. Ni zoezi gumu kwa watu wanaotumia killevi na wale wa mfumo dume. Kufanisha njia hii inahitaji ushirikiano wa kutosha kati ya mke na mme. Na njia ya ute inaaminika sana hata kuliko ile ya kalenda na hata kondom.
 
ighaghe

ighaghe

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2013
Messages
702
Likes
791
Points
180
ighaghe

ighaghe

JF-Expert Member
Joined Mar 25, 2013
702 791 180
Mkuu ukisoma hilo bandiko Kanisa utaona uzazi wa mpango haukubaliki. Kama kumwaga nje mbegu ni chukizo kwa Mungu ni mbinu ipi itakuwa salama?
Hii ni tafsiri yako wewe. Mambo ya kumwaga nje kuwa ni chukizo la MUNGU sababu tu kuna Mtu alikufa baada ya kufanya hivyo ni tafsiri yako wewe ya kifungu husika.Hata shetani alimjaribu YESU kwa kutumia kifungu cha Biblia, na alikitasiri kwa tafsiri yake yeye. Biblia hiyo hiyo inaelekeza kuwalea watoto katika njia ipasayo ili watakapokua wasiiache Kamwe. Sasa wewe tengeneza shule huku huna uwezo halafu uone kama hutakuza vibaka.
 
MTAZAMO

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Messages
14,117
Likes
9,339
Points
280
MTAZAMO

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined Feb 8, 2011
14,117 9,339 280
Kulingana na mafunzo ya Sr. Brigita( MD), mbobezi katika masuala ya uzazi, hutakiwi kufanya siku za hatari. Kwa hiyo humwagi, unajizuia kufanya tendo la ndoa. Ute unaotoka kwa mwanamke unatabia zake ambazo unatakiwa kuzisoma na kuzifuatilia. Ni zoezi gumu kwa watu wanaotumia killevi na wale wa mfumo dume. Kufanisha njia hii inahitaji ushirikiano wa kutosha kati ya mke na mme. Na njia ya ute inaaminika sana hata kuliko ile ya kalenda na hata kondom.
Asante sana mkuu. Andiko lako hili litatusaidia wengi.
 
MWEMBESI ONE

MWEMBESI ONE

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2015
Messages
917
Likes
1,445
Points
180
Age
27
MWEMBESI ONE

MWEMBESI ONE

JF-Expert Member
Joined Mar 16, 2015
917 1,445 180
Siku hizi dhambi zinategemeana na dhehebu lako au mapokeo ya kanisa husika? Sikuhizi kila dhehebu la dini limeainisha dhambi wanazozijua wenyewe huku kukiwa na utofauti mkubwa kati ya dhehebu moja na jingine.

Kama wewe una watoto wengi kama siafu pambana na hali yako usiwe kikwazo kwa waliamua kupanga uzazi
 

Forum statistics

Threads 1,262,089
Members 485,449
Posts 30,112,703