Msimamo wa Kanisa Katoliki kuhusu uzazi wa mpango

MTAZAMO

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Messages
14,117
Likes
9,338
Points
280
MTAZAMO

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined Feb 8, 2011
14,117 9,338 280
Hili ni jibu kwa swali lililoulizwa na muumini mmoja juu ya uzazi wa mpango.

Jibu; Katika mafundisho yanadhihakiwa na Wakristu wengi ni yale yanayohusu utumiaji wa njia za kisasa katika uzazi wa mpango. Wakatoliki wengi na kwa asimilia kubwa sana hudondoka hapa japo Kanisa limeweka bayana kuhusu jambo hili. Pia inasikitisha zaidi kwamba Kanisa Katoliki ndilo limeweka wazi fundisho lake. Madhehebu mengine huonekana kukubali utumiaji wa njia hizi ama huonekana kutokemea kana kwamba kuonea aibu. Hivyo Kanisa linabaki peke yake katika vita hii inayowashinda waumini wake wengi.

Lakini haikua hivi toka mwanzo. Mpaka mwaka wa 1930, Waprotestanti karibu wote walikubaliana na Kanisa Katoliki kuhusu fundisho hili. Kitu gani sasa kilitokea hadi mabadiliko? Mwaka huo wa 1930 ulifanyika mkutano wa kanisa la Anglikana (Uingereza) huko Lambethi na mkutano ukapitisha njia hizo za kisasa za uzazi wa mpango ziruhusiwe katika hali mbalimbali. Ikapita miaka mbele na jinsi msukumo wa dunia ulivyoendelea, utumuaji huo ukafika hadi kuhalalishwa na madhehebu mengi tu hadi hivi leo. Njia za kisasa za uzazi wa mpango zinatumika kwa amani tu na Wakristu. Hata ikafika wakati baadhi ya Maaskofu katika Kanisa Katoliki nao wakashawishika kukubali matumizi haya. Jambo hili likaleta mzogo mkubwa ndani ya Kanisa. Katika kuona haya, Baba Mtakatifu (Papa Mwenyeheri Paulo VI) katika barua yake (Human Vitae, 1968) kwa Maaskofu wote duniani yaani Encyclical akaweka msimamo katika fundisho la Kanisa kwamba halibadiliki na kila Mkatoliki akubali kwa ajili ya wokovu wa roho yake. Barua hii inasifiwa sana kwa utabiri wake kwani ilisema kuwa ndoa nyingi zitavunjika na familia kutengana kutokana na wingi wa matumizi ya vifaa hivi hapo baadaye. Ndio mambo tunayoyaona kipindi hiki

Kanisa Katoliki linafundisha kuwa utumiaji wa njia hizi za kisasa ni dhambi kubwa atendayo muumini. Biblia imefundisha hili pamoja na Mapokeo ya Mitume yaani Apostolic Tradition. Lakini kwanza tuangalie maelezo juu ya njia hizi.

Uzazi wa mpango kwa njia za kisasa maana yake ni njia mbalimbali ambazo binadamu kwa kusaidiwa na tekinolojia ama vifaa mbalimbali analenga kuzuia utunzi wa mimba ambayo inadhaniwa kuleta madhara ya aina moja ama nyingine. Hivyo binadamu anatafuta njia za kisasa kuzuia mpango wa Mungu na kuenda kinyume na kile alichopanga Mungu. Kwamba tendo la ndoa liweke wazi uwezekano wa mimba kutungwa na kuzaliwa mtoto. Vifaa hivyo basi vinapewa nguvu kubwa ya kumzidi Mungu kwa kumuamuru asitengeneze uwezekano wa mimba kutungwa. Hivyo nafsi inadhamiri kumzuia Mungu. Mtu aliyekusudia kukwepa mimba kwa mbinu yoyote anafikia kwa urahisi fulani uamuzi wa KUIUA. Hapa anakua haui mimba bali anakua ANAUA binadamu

Njia hizi za kisasa ni zipi?

Baadhi ya njia hizo za kuzuia uzazi ni: mipira kiume na ya kike yaani Kondomu, kufunga daima kizazi kwa upande wa mwanaume/mwanamke. Vingine vizuizi mimba ni Vidonge (Pills), Sindano, Poda, Vitanzi na Vipandikizi

Biblia inatufundisha nini juu ya hili jambo?

Uzuiaji wa mimba si jambo la kigeni bali toka enzi za mababu hata kabla ya Kristu, binadamu walitumia njia mbalimali kuzuia kizazi. Huko Misri, katika kipindi cha wakristu wa mwanzo palipatikana vitabu vilivyoonyesha matumizi ya njia hizi mbalimbali za kuzuia mimba zikiwamo pamba zinazonyonya mbegu za kiume, sumu inayoshambulia tumbo la kizazi(uterus), mipira ya kiume inayotengenezwa na ngozi za wanyama pamoja na njia nyingine ya kizuizi. Moja ambayo ni ya kitambo sana lakini hutumika mpaka hivi leo ni ile ya kumwaga mbegu za kiume nje ya tumbo la kizazi (Withdrawal). Njia hizi humkasirisha Mungu na ametupa mfano wa hasira yake katika kitabu cha Mwanzo cha Biblia. Tunamwona Onani mwana wa Yuda aliyeuawa hapo hapo kwa kumwaga mbegu nje ya tumbo la kizazi (Mwanzo 38). Kutokana na tamaduni za Kiyahudi, Onani alipewa amri ya kuendeleza kizazi cha kaka yake kwa kuzaa na mjane wa kaka yake. Lakini yeye alikataa hilo, akaamua kufanya starehe tu lakini asitoe mbegu za mtoto. Kuhusu yeye Biblia inaandika “……ikawa, alipoingia kwa mke wa nduguye, akamwagia chini asimpe nduguye uzao. Neno hili alilolifanya likawa baya machoni pa Bwana, basi akamwua yeye naye” (Mwanzo 38:9-10)

Cha kusikitisha, ili kuweza kuhalalisha dhambi, Wakristu hata baada ya kuona mfano huu, wanaubadilisha maana yake wakisema Mungu hakumwua Onani kwasababu ya kumwaga mbegu nje bali kwasababu ya kukataa kwake kuendeleza uzao wa kaka yake. Je, ni kweli hivi? HAPANA. Ukisoma kitabu cha Kumbukumbu la Torati 25:7-10, utagundua kuwa adhabu ya kukataa kuendeleza kizazi cha ndugu haikua kifo, bali ilikua ni kufanywa aibu kubwa mbele ya watu (Public Humiliation). Kitabu kinasema, baada ya mtu kukataa kulala na mjane wa ndugu yake ili aongeze kizazi, “......ndipo mke wa nduguye amkaribie mbele ya hao wazee, amvue kiatu chake mguuni mwake, na kumtemea mate ya uso..... Na jina lake katika Israeli liitwe, Nyumba ya mvuliwa kiatu (Kumbukumbu la Torati 25:9,10). Hivyo adhabu ilikua ni AIBU na sio KIFO. Lakini Onani yeye alipewa hukumu kali ya kifo kwa maana alimchukiza Mungu kwa tendo lake la kumwaga nje mbegu zake za kiume.

Kwa hali hii, Watakatifu Mababa wa Kanisa (Church Fathers) na wao hawakua mbali kukemea hali hii. Katika baadhi ya maandishi yao wanasema:

Mt. Clement wa Alexandria (Mwaka 191): “Kutokana na kuwekwa na Mungu aliye Mtakatifu, mbegu (ya kiume) haitakiwi kumwagwa nje (ya tumbo la kizazi), wala kuharibiwa na sio ya kutupwa” (The Instructor of Children 2:10:91:2)

Mt. Hyppolytus wa Roma (Mwaka 255): Akiwaandikia baadhi ya wanawake wakristu waliofanya uzinzi na watumwa/wafanyakazi wao anawaambia, “...wanatumia madawa ya kutengeneza utasa/ugumba ama wanajifunga kwa nguvu ili wafanikiwe kutoa kiumbe ambacho kimeshatungwa kama mimba tumboni mwao”

Mt. Agustino (Mwaka 419): Akiwaandikia wenye ndoa
wanaokutana kwa ajili tu ya starehe bila kuwa na nia ya kutengeneza mtoto anawaambia, “.....wale wanaofanya hivyo, japo wanaitwa mume na mke, hawaishi katika hali ya ndoa, bali wamebeba jina la aibu. Mara nyingine, tamaa hizo za mwili zinafika hadi kuwafanya watengeneze madawa ya ugumba na utasa”

Tofauti na Wakristu Waprotestanti wa siku hizi, inabidi Waprotestanti pia wakumbuke kua waanzilishi wa Uprotestanti kama Martin Luther walikemea sana tabia hizi ya uzuizi wa Mimba. Luther, akiongelea uovu wa Onani aliyeuawa na Mungu kwa kosa lake anasema “..Ni kosa kubwa la fedheha...Yeye (Onani) alistahili kuuawa na Mungu. Alifanya uovu mkubwa, hivyo Mungu akamwadhibu”

Naye Mprotestanti John Calvin, mwanzilishi wa kanisa la Presbetaria anasema kuhusu dhambi ya Onani “Jambo la kumwaga nje mbegu za kiume katika tendo la ndoa kati ya wawili ni jambo la uovu mkubwa. Kuuondoa uume nje ili mbegu zimwagike ni uovu mkubwa kwa maana tendo hili linaondoa tumaini la kizazi na kuua kabla hata ya kuzaliwa yule aliyetegemewa.

Naye mwanzilishi wa kanisa la Methodisti, John Wesley anasema kuhusu dhambi ya Onani, “..alichokifanya Onani, kilimuudhi Mungu na lazima (kitendo hicho) kiogopwe....kwa kuwa kitu hiki, bado kinamchukiza Mungu na kinateketeza roho (za watu)”

Sasa tunajiuliza, kama pia waanzilishi wa madhehebu hayo ya kiprotestanti makubwa ya Kikristu walikemea na kupinga njia hizi, kwanini Wakristu katika madhehebu hayo siku hizi wanakubali kutumia yale ambayo waanzilishi walikataza? Jambo la kutafakari

Mwisho kabisa, madhara yanayojitokeza siku hizi kutokana na matumizi hayo ni makubwa kwa taifa la Kristu. Madawa hayo yameongeza kwa kasi kubwa vitendo ya uzinzi na uasherati. Wana ndoa wengi kwa kuwezeshwa na vifaa hivyo wanatembea nje ya ndoa zao wakijua wanayo silaha tosha ya kutotengeneza mtoto nje ya ndoa. Matokeao ni ndoa kuvunjika na watoto kutekelezwa.

Vijana nao wamejiingiza katika ngono kwa kuwa hawana tena hofu ya kutengeneza mtoto kabla ya ndoa

Wanawake nje ama ndani ya ndoa wanageuzwa kuwa chombo tu cha starehe ambacho mwanaume anatumia kwa kijiridhisha muda wowote na tamaa zake

Source; Facebook page, idara ya uchungaji TEC, @ 2015
 
General Mangi

General Mangi

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2013
Messages
13,514
Likes
18,136
Points
280
General Mangi

General Mangi

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2013
13,514 18,136 280
Kichaa pekee ndo anaweza kukubaliana na kichaa mweziee.

Unajua wazi kabisa huna uwezo wa kusomesha, kulisha, kutoa ajira, kuhudumia huduma za afya.

Bado unasisitiza watu wazaee bila mipango.

Kweli kama Ney alivyosema, kichaa kapewa rungu, ndo naoa yanatokea
 
MTAZAMO

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Messages
14,117
Likes
9,338
Points
280
MTAZAMO

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined Feb 8, 2011
14,117 9,338 280
Kichaa pekee ndo anaweza kukubaliana na kichaa mweziee.

Unajua wazi kabisa huna uwezo wa kusomesha, kulisha, kutoa ajira, kuhudumia huduma za afya.

Bado unasisitiza watu wazaee bila mipango.

Kweli kama Ney alivyosema, kichaa kapewa rungu, ndo naoa yanatokea
Mkuu kwahili JPM alikuwa sahihi ...
 
MTAZAMO

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Messages
14,117
Likes
9,338
Points
280
MTAZAMO

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined Feb 8, 2011
14,117 9,338 280
ujue uzaz wa mpango umeanza na viongozi wenyewe wa kanisa kuzuiliwa kuoa na kuolewa?
papa ana watoto wangapi mkuu!!!??
Haina uhusiano na uzazi wa mpango.
 
inamankusweke

inamankusweke

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2014
Messages
5,137
Likes
3,197
Points
280
Age
31
inamankusweke

inamankusweke

JF-Expert Member
Joined Apr 24, 2014
5,137 3,197 280
Kichaa pekee ndo anaweza kukubaliana na kichaa mweziee.

Unajua wazi kabisa huna uwezo wa kusomesha, kulisha, kutoa ajira, kuhudumia huduma za afya.

Bado unasisitiza watu wazaee bila mipango.

Kweli kama Ney alivyosema, kichaa kapewa rungu, ndo naoa yanatokea
acha watu wazae,india na china wanatoka hukohuko...naunga mkono uzazi wa mpango ila napinga matumizi ya vidonge vya uzazi
 
General Mangi

General Mangi

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2013
Messages
13,514
Likes
18,136
Points
280
General Mangi

General Mangi

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2013
13,514 18,136 280
Mkuu kwahili JPM alikuwa sahihi ...
Alikuwa sahihi kivipi??

Mimi ningekua Rais ningeweka sheria kila atakae zaa lzm awe na uwezo wa kumudu malezi ya mtoto, vinginevyo hakuna kuzaa.

Watoto wengi wanateseka kwa wazazi wao kutomudu malezi yao.

Huwezi leta kiumbe duniani kije kupata matatizo
 
Crimea

Crimea

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2014
Messages
5,720
Likes
4,641
Points
280
Age
29
Crimea

Crimea

JF-Expert Member
Joined Mar 25, 2014
5,720 4,641 280
Nyumbu wanampinga JPM pamoja na kwamba ni wakatoliki..

Shida kweli
 
Aaron

Aaron

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2010
Messages
2,900
Likes
4,087
Points
280
Aaron

Aaron

JF-Expert Member
Joined Nov 18, 2010
2,900 4,087 280
Jamiiforums imevamiwa mnashindwa kutofautisha uzazi wa mpango wa kisasa na uzazi wa mpango....mleta mada unataka kuhalalisha kauli ya jpm ya kufyatua kwa kutumia hili andiko la kikatoliki.. Mimi ni mkatoliki na sikubaliani na njia za uzazi wa mpango wa kisasa...na kanisa halipingi uzazi wa mpango bali linaelekeza njia sahihi za asili ambazo hazina madhara kwa ajili ya kupanga uzazi....hakuna sehemu kanisa linasema tufyatue bila mpangilio
 
Aaron

Aaron

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2010
Messages
2,900
Likes
4,087
Points
280
Aaron

Aaron

JF-Expert Member
Joined Nov 18, 2010
2,900 4,087 280
Nyumbu wanampinga JPM pamoja na kwamba ni wakatoliki..

Shida kweli
Kama wewe si mkatoliki kaa kimya...haya mafundisho tunayajua zaidi ya jpm anayesema wafyatue bila mpangilio...acha kutetea ujinga.
 
B

BEHOLD

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2013
Messages
3,461
Likes
6,037
Points
280
B

BEHOLD

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2013
3,461 6,037 280
Inawezekana Raisi alihisi watu wote wanalishwa na kutunzwa na serikali na kupewa mshahara mnono kama yeye.

Aliyeshiba hamjui mwenye njaa, walisema Wahenga.
 
Grey256

Grey256

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2016
Messages
686
Likes
1,057
Points
180
Grey256

Grey256

JF-Expert Member
Joined Sep 1, 2016
686 1,057 180
Jamiiforums imevamiwa mnashindwa kutofautisha uzazi wa mpango wa kisasa na uzazi wa mpango....mleta mada unataka kuhalalisha kauli ya jpm ya kufyatua kwa kutumia hili andiko la kikatoliki.. Mimi ni mkatoliki na sikubaliani na njia za uzazi wa mpango wa kisasa...na kanisa halipi uzazi wa mpango bali unaelekeza njia sahihi za asili ambazo hazina madhara kwa ajili ya kupanga uzazi....hakuna sehemu kanisa linasema tufyatue bila mpangilio
Ni njia gani hizo za asili mkuu?...Tusaidiane
 
All TRUTH

All TRUTH

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2011
Messages
3,611
Likes
1,165
Points
280
All TRUTH

All TRUTH

JF-Expert Member
Joined Nov 20, 2011
3,611 1,165 280
Dah watakaokuelewa utawajua tu
 
MTAZAMO

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Messages
14,117
Likes
9,338
Points
280
MTAZAMO

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined Feb 8, 2011
14,117 9,338 280
Jamiiforums imevamiwa mnashindwa kutofautisha uzazi wa mpango wa kisasa na uzazi wa mpango....mleta mada unataka kuhalalisha kauli ya jpm ya kufyatua kwa kutumia hili andiko la kikatoliki.. Mimi ni mkatoliki na sikubaliani na njia za uzazi wa mpango wa kisasa...na kanisa halipi uzazi wa mpango bali unaelekeza njia sahihi za asili ambazo hazina madhara kwa ajili ya kupanga uzazi....hakuna sehemu kanisa linasema tufyatue bila mpangilio
Mkuu hujasoma hilo bandiko otherwise usingeandika hivi ....
 
Crimea

Crimea

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2014
Messages
5,720
Likes
4,641
Points
280
Age
29
Crimea

Crimea

JF-Expert Member
Joined Mar 25, 2014
5,720 4,641 280
Kama wewe si mkatoliki kaa kimya...haya mafundisho tunayajua zaidi ya jpm anayesema wafyatue bila mpangilio...acha kutetea ujinga.
Huna akili kabisa... Twambie sasa hayo mafundisho yanahusu nini zaidi ya kukataa hizo njia za uzazi wa mpango?
 
Aaron

Aaron

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2010
Messages
2,900
Likes
4,087
Points
280
Aaron

Aaron

JF-Expert Member
Joined Nov 18, 2010
2,900 4,087 280
Huna akili kabisa... Twambie sasa hayo mafundisho yanahusu nini zaidi ya kukataa hizo njia za uzazi wa mpango?
Hahaha sasa wewe si mkatoliki na unakaza kichwa...!!! Ni hivi kanisa katoliki halikatazi uzazi wa mpango bali linaelekeza njia sahihi zitakazo tumika kupanga uzazi....!!
 
Ndalama

Ndalama

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2011
Messages
8,462
Likes
5,397
Points
280
Ndalama

Ndalama

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2011
8,462 5,397 280
Hili ni jibu kwa swali lililoulizwa na muumini mmoja juu ya uzazi wa mpango.

Jibu; Katika mafundisho yanadhihakiwa na Wakristu wengi ni yale yanayohusu utumiaji wa njia za kisasa katika uzazi wa mpango. Wakatoliki wengi na kwa asimilia kubwa sana hudondoka hapa japo Kanisa limeweka bayana kuhusu jambo hili. Pia inasikitisha zaidi kwamba Kanisa Katoliki ndilo limeweka wazi fundisho lake. Madhehebu mengine huonekana kukubali utumiaji wa njia hizi ama huonekana kutokemea kana kwamba kuonea aibu. Hivyo Kanisa linabaki peke yake katika vita hii inayowashinda waumini wake wengi.

Lakini haikua hivi toka mwanzo. Mpaka mwaka wa 1930, Waprotestanti karibu wote walikubaliana na Kanisa Katoliki kuhusu fundisho hili. Kitu gani sasa kilitokea hadi mabadiliko? Mwaka huo wa 1930 ulifanyika mtukano wa kanisa la Anglikana (Uingereza) huko Lambethi na mkutano ukapitisha njia hizo za kisasa za uzazi wa mpango ziruhusiwe katika hali mbalimbali. Ikapita miaka mbele na jinsi msukumo wa dunia ulivyoendelea, utumuaji huo ukafika hadi kuhalalishwa na madhehebu mengi tu hadi hivi leo. Njia za kisasa za uzazi wa mpango zinatumika kwa amani tu na Wakristu. Hata ikafika wakati baadhi ya Maaskofu katika Kanisa Katoliki nao wakashawishika kukubali matumizi haya. Jambo hili likaleta mzogo mkubwa ndani ya Kanisa. Katika kuona haya, Baba Mtakatifu (Papa Mwenyeheri Paulo VI) katika barua yake (Human Vitae, 1968) kwa Maaskofu wote duniani yaani Encyclical akaweka msimamo katika fundisho la Kanisa kwamba halibadiliki na kila Mkatoliki akubali kwa ajili ya wokovu wa roho yake. Barua hii inasifiwa sana kwa utabiri wake kwani ilisema kuwa ndoa nyingi zitavunjika na familia kutengana kutokana na wingi wa matumizi ya vifaa hivi hapo baadaye. Ndio mambo tunayoyaona kipindi hiki

Kanisa Katoliki linafundisha kuwa utumiaji wa njia hizi za kisasa ni dhambi kubwa atendayo muumini. Biblia imefundisha hili pamoja na Mapokeo ya Mitume yaani Apostolic Tradition. Lakini kwanza tuangalie maelezo juu ya njia hizi.

Uzazi wa mpango kwa njia za kisasa maana yake ni njia mbalimbali ambazo binadamu kwa kusaidiwa na tekinolojia ama vifaa mbalimbali analenga kuzuia utunzi wa mimba ambayo inadhaniwa kuleta madhara ya aina moja ama nyingine. Hivyo binadamu anatafuta njia za kisasa kuzuia mpango wa Mungu na kuenda kinyume na kile alichopanga Mungu. Kwamba tendo la ndoa liweke wazi uwezekano wa mimba kutungwa na kuzaliwa mtoto. Vifaa hivyo basi vinapewa nguvu kubwa ya kumzidi Mungu kwa kumuamuru asitengeneze uwezekano wa mimba kutungwa. Hivyo nafsi inadhamiri kumzuia Mungu. Mtu aliyekusudia kukwepa mimba kwa mbinu yoyote anafikia kwa urahisi fulani uamuzi wa KUIUA. Hapa anakua haui mimba bali anakua ANAUA binadamu

Njia hizi za kisasa ni zipi?

Baadhi ya njia hizo za kuzuia uzazi ni: mipira kiume na ya kike yaani Kondomu, kufunga daima kizazi kwa upande wa mwanaume/mwanamke. Vingine vizuizi mimba ni Vidonge (Pills), Sindano, Poda, Vitanzi na Vipandikizi

Biblia inatufundisha nini juu ya hili jambo?

Uzuiaji wa mimba si jambo la kigeni bali toka enzi za mababu hata kabla ya Kristu, binadamu walitumia njia mbalimali kuzuia kizazi. Huko Misri, katika kipindi cha wakristu wa mwanzo palipatikana vitabu vilivyoonyesha matumizi ya njia hizi mbalimbali za kuzuia mimba zikiwamo pamba zinazonyonya mbegu za kiume, sumu inayoshambulia tumbo la kizazi(uterus), mipira ya kiume inayotengenezwa na ngozi za wanyama pamoja na njia nyingine ya kizuizi. Moja ambayo ni ya kitambo sana lakini hutumika mpaka hivi leo ni ile ya kumwaga mbegu za kiume nje ya tumbo la kizazi (Withdrawal). Njia hizi humkasirisha Mungu na ametupa mfano wa hasira yake katika kitabu cha Mwanzo cha Biblia. Tunamwona Onani mwana wa Yuda aliyeuawa hapo hapo kwa kumwaga mbegu nje ya tumbo la kizazi (Mwanzo 38). Kutokana na tamaduni za Kiyahudi, Onani alipewa amri ya kuendeleza kizazi cha kaka yake kwa kuzaa na mjane wa kaka yake. Lakini yeye alikataa hilo, akaamua kufanya starehe tu lakini asitoe mbegu za mtoto. Kuhusu yeye Biblia inaandika “……ikawa, alipoingia kwa mke wa nduguye, akamwagia chini asimpe nduguye uzao. Neno hili alilolifanya likawa baya machoni pa Bwana, basi akamwua yeye naye” (Mwanzo 38:9-10)

Cha kusikitisha, ili kuweza kuhalalisha dhambi, Wakristu hata baada ya kuona mfano huu, wanaubadilisha maana yake wakisema Mungu hakumwua Onani kwasababu ya kumwaga mbegu nje bali kwasababu ya kukataa kwake kuendeleza uzao wa kaka yake. Je, ni kweli hivi? HAPANA. Ukisoma kitabu cha Kumbukumbu la Torati 25:7-10, utagundua kuwa adhabu ya kukataa kuendeleza kizazi cha ndugu haikua kifo, bali ilikua ni kufanywa aibu kubwa mbele ya watu (Public Humiliation). Kitabu kinasema, baada ya mtu kukataa kulala na mjane wa ndugu yake ili aongeze kizazi, “......ndipo mke wa nduguye amkaribie mbele ya hao wazee, amvue kiatu chake mguuni mwake, na kumtemea mate ya uso..... Na jina lake katika Israeli liitwe, Nyumba ya mvuliwa kiatu (Kumbukumbu la Torati 25:9,10). Hivyo adhabu ilikua ni AIBU na sio KIFO. Lakini Onani yeye alipewa hukumu kali ya kifo kwa maana alimchukiza Mungu kwa tendo lake la kumwaga nje mbegu zake za kiume.

Kwa hali hii, Watakatifu Mababa wa Kanisa (Church Fathers) na wao hawakua mbali kukemea hali hii. Katika baadhi ya maandishi yao wanasema:

Mt. Clement wa Alexandria (Mwaka 191): “Kutokana na kuwekwa na Mungu aliye Mtakatifu, mbegu (ya kiume) haitakiwi kumwagwa nje (ya tumbo la kizazi), wala kuharibiwa na sio ya kutupwa” (The Instructor of Children 2:10:91:2)

Mt. Hyppolytus wa Roma (Mwaka 255): Akiwaandikia baadhi ya wanawake wakristu waliofanya uzinzi na watumwa/wafanyakazi wao anawaambia, “...wanatumia madawa ya kutengeneza utasa/ugumba ama wanajifunga kwa nguvu ili wafanikiwe kutoa kiumbe ambacho kimeshatungwa kama mimba tumboni mwao”

Mt. Agustino (Mwaka 419): Akiwaandikia wenye ndoa
wanaokutana kwa ajili tu ya starehe bila kuwa na nia ya kutengeneza mtoto anawaambia, “.....wale wanaofanya hivyo, japo wanaitwa mume na mke, hawaishi katika hali ya ndoa, bali wamebeba jina la aibu. Mara nyingine, tamaa hizo za mwili zinafika hadi kuwafanya watengeneze madawa ya ugumba na utasa”

Tofauti na Wakristu Waprotestanti wa siku hizi, inabidi Waprotestanti pia wakumbuke kua waanzilishi wa Uprotestanti kama Martin Luther walikemea sana tabia hizi ya uzuizi wa Mimba. Luther, akiongelea uovu wa Onani aliyeuawa na Mungu kwa kosa lake anasema “..Ni kosa kubwa la fedheha...Yeye (Onani) alistahili kuuawa na Mungu. Alifanya uovu mkubwa, hivyo Mungu akamwadhibu”

Naye Mprotestanti John Calvin, mwanzilishi wa kanisa la Presbetaria anasema kuhusu dhambi ya Onani “Jambo la kumwaga nje mbegu za kiume katika tendo la ndoa kati ya wawili ni jambo la uovu mkubwa. Kuuondoa uume nje ili mbegu zimwagike ni uovu mkubwa kwa maana tendo hili linaondoa tumaini la kizazi na kuua kabla hata ya kuzaliwa yule aliyetegemewa.

Naye mwanzilishi wa kanisa la Methodisti, John Wesley anasema kuhusu dhambi ya Onani, “..alichokifanya Onani, kilimuudhi Mungu na lazima (kitendo hicho) kiogopwe....kwa kuwa kitu hiki, bado kinamchukiza Mungu na kinateketeza roho (za watu)”

Sasa tunajiuliza, kama pia waanzilishi wa madhehebu hayo ya kiprotestanti makubwa ya Kikristu walikemea na kupinga njia hizi, kwanini Wakristu katika madhehebu hayo siku hizi wanakubali kutumia yale ambayo waanzilishi walikataza? Jambo la kutafakari

Mwisho kabisa, madhara yanayojitokeza siku hizi kutokana na matumizi hayo ni makubwa kwa taifa la Kristu. Madawa hayo yameongeza kwa kasi kubwa vitendo ya uzinzi na uasherati. Wana ndoa wengi kwa kuwezeshwa na vifaa hivyo wanatembea nje ya ndoa zao wakijua wanayo silaha tosha ya kutotengeneza mtoto nje ya ndoa. Matokeao ni ndoa kuvunjika na watoto kutekelezwa.

Vijana nao wamejiingiza katika ngono kwa kuwa hawana tena hofu ya kutengeneza mtoto kabla ya ndoa

Wanawake nje ama ndani ya ndoa wanageuzwa kuwa chombo tu cha starehe ambacho mwanaume anatumia kwa kijiridhisha muda wowote na tamaa zake

Source; Facebook page, idara ya uchungaji TEC, @ 2015
Wanatuchanganya kuhusu Onani na maneno meengi, 1Kor 7:1-9 inaelezea kuzaa? au kutimiza tamaa ya mwili?
 
Forum statistics

Threads 1,262,077
Members 485,449
Posts 30,112,577