He is right to some extent! kiukweli historia haiibebi ccccm ila kuna kitu kigumu sana lazima wafanye ili kurudisha imani kwa wapiga kura. Ukweli uliodhahiri ni kwamba mara nyinyi watawala wa kiafrika huwa hawaamini kuwa ipo siku wananchi wao wanaweza kuwageuka. Kwa viongozi wenye kuona mbele wanatakiwa kuikubali hali halisi ili mabadiliko yasiathuri heshima yao na vizazi pamoja na hatma yao ya baadae. Matendo yoyote maovu kwa wapinzani ni kuzidi kuchochea chuki kati ya watawala na watawaliwa. Je siku wapinzani wakichukua dola kweli kuna usalama kwao?. Mfumo wa vyama vingi usiwe mtego kwetu, tumeukubali basitukubali na matokeo yake. Leo unmpiga kirungu kichwani mpinzani wako kwa kutumia polic keshokutwa anakuwa rais kibinadam hapo lazima mtataftana tu. So tukubali kukosolewa, cccm iheshim wapinzanni ijipange na kujisahihisha ili ipambane kwa hoja na sikutegemea nguvu za dola. Vinginevyo kuendelea kutumia dola mwishowa siku ikipoteza tu visasi havitaepukika