Msigwa umechemka kumsifia Kikwete

Msigwa umechemka kumsifia Kikwete

bora fidel castrol hajabadili msimamo wake kwa wamarekani. Kukataa kukutana na obama juz juz tu hapa na kisha kuziponda sera mbovu za marekani.

kwel siasa ni upepo...
 
Mkuu, Watanzania wengi hawamfahamu vizuri Mbowe. Mbowe ni mtoto wa mjini. Kama humjui ukiona anaongea unaweza kusema huyu ni mfia nchi. Mbowe ni mfanyabiashara wa siasa. Hili kosa ndo lilitufikisha hapa la kuwaamini watoto wa mjini kama akina Kikwete. Tanzania hakuna upinzani wa kweli
Mtoto mwingine wa mjini ni zzk, huyu yuko smart sana, ukiingia kichwa inakula kwako.
 
bora fidel castrol hajabadili msimamo wake kwa wamarekani. Kukataa kukutana na obama juz juz tu hapa na kisha kuziponda sera mbovu za marekani.

kwel siasa ni upepo...
Hata OJ Simpson, alibaki na msimamo wake wa NOT GUILT licha ya kila ushahidi kusema ye nduye muhusika wa mauaji, inatakiwa mtu uwe na msimamo, hata kama ni uongo, unausimamia kwako unakuw ukweli. Sada haw wenzangu somo la msimamo wanafeli kila siku.
 
Jk aliwaambiwa upinzani kuwa akitoka watamkumbuka,wakamkebehi na kumwona anajifurahisha tu.
 
Nilishasema zamani kabisa kwa upinzani wa nchi hii bora ccm itawale milele mpaka pale nchi itakuja kupata upinzani wa kweli hata ikifika 2050

Mr. Hero acha vihoja hapa.
CCM watawale milele kwa ubora upi hasa? Watu wameingia Ikulu kwa kupitia mlango wa nyuma(wizi na uchakachauji wa kura) halafu wewe unasema waendelee kutawala milele????Kweli? You must be sick in your head. Hii ndo tunaita uvivu wa kufikiri.

Alichosema Msigwa ni kwamba PAMOJA NA UDHAIFU WA SERIKALI YA A4 YA JMK BADO ILIRUHUSU BUNGWE KURUSHWA 'LIVE'! Hajasema ati Rais Kiwekte alikuwa Rais mzuri. Kinachoonekna wewe hukumwelewa Msigwa.
Msigwa allienda mbali na kusema kuwa Bunge la Serikali ya A5 ya Mhe. Magufuli limegeuzwa kama Bunge la UNYAGO( Kutahiriwa kwa wavulana au wasichana wadogo) kitu ambacho huwa ni siri na kinafanywa porini kwenye maficho ili watu wasione.

Jambo la msingi hapa ambalo Watz wanatakiwa kujiuliza ni kwanini Serikali ya JPM hawataki kuonys=esha Bunge Live? Jibu ni kwamba Serikali hii haijiamini na huenda huko baadaye ikawa ni dhaifu zaidi ya Serikali ya JK. Wanachoficha hapa ni UDHAIFU ambao unawanyemelea baada ya kumaliza kutumbua majipu watakuwa hawana jipya!!!

Time gonna tell. Just wait and see!
 
Mtoto mwingine wa mjini ni zzk, huyu yuko smart sana, ukiingia kichwa inakula kwako.

Kumbe nawe unawajua watoto wa mjini?? Hahahahaa
Kwa siasa za Bongo watu wasipokuwa makini tunaweza kuwa tunaingizwa mjini tu. Shida ya jamii yetu nadhani tumeishapoteza thamani ya utu. Ukiangalia nchi nyingi za Kiafrika ndo utagundua kuna tatizo kwenye jamii yetu. Siyo nchi za kiafrica tu ila sehemu yoyote wanakoishi watu wenye asili ya Africa kuna shida tu. Nilishughudia kisa kimoja wakati niko masomoni Ulaya. Nikapata Internship kwenye Kampuni moja hivi, Pale nikakuta Jamaa watatu wa Kiafrica. Mmoja mzaliwa wa nchi hiyo, mmoja kutoka Nigeria na mwingine Cameroon. Cha kushangaza kila wakati wanawake wakizungu walikuwa wanawalalamikia kwa usumbufu wa kutongoza kila mwanamke pale ofisini. Yaani Mtu hawezi kwenda sehemu akasema aisome hiyo jamii inaishije, principles za maisha yao zikoje ili aendane na mfumo wao wa maisha. Jamii yetu ni ujanja ujanja tu kila sehemu.
 
bora fidel castrol hajabadili msimamo wake kwa wamarekani. Kukataa kukutana na obama juz juz tu hapa na kisha kuziponda sera mbovu za marekani.

kwel siasa ni upepo...

Una uhakika unafuatilia vizuri haya mambo unayoyaleta hapa?? Wiki mbili zilizopita Fidel mwenyewe kamu endorse mdogo wake kwenye mkutano mkuu wa chama chao na kuwa anaunga mkono jitihada zote anazoendelea nazo. Uliyasikia haya? Au ulipoyasikia ulielewa nini?
 
Mr. Hero acha vihoja hapa.
CCM watawale milele kwa ubora upi hasa? Watu wameingia Ikulu kwa kupitia mlango wa nyuma(wizi na uchakachauji wa kura) halafu wewe unasema waendelee kutawala milele????Kweli? You must be sick in your head. Hii ndo tunaita uvivu wa kufikiri.

Alichosema Msigwa ni kwamba PAMOJA NA UDHAIFU WA SERIKALI YA A4 YA JMK BADO ILIRUHUSU BUNGWE KURUSHWA 'LIVE'! Hajasema ati Rais Kiwekte alikuwa Rais mzuri. Kinachoonekna wewe hukumwelewa Msigwa.
Msigwa allienda mbali na kusema kuwa Bunge la Serikali ya A5 ya Mhe. Magufuli limegeuzwa kama Bunge la UNYAGO( Kutahiriwa kwa wavulana au wasichana wadogo) kitu ambacho huwa ni siri na kinafanywa porini kwenye maficho ili watu wasione.

Jambo la msingi hapa ambalo Watz wanatakiwa kujiuliza ni kwanini Serikali ya JPM hawataki kuonys=esha Bunge Live? Jibu ni kwamba Serikali hii haijiamini na huenda huko baadaye ikawa ni dhaifu zaidi ya Serikali ya JK. Wanachoficha hapa ni UDHAIFU ambao unawanyemelea baada ya kumaliza kutumbua majipu watakuwa hawana jipya!!!

Time gonna tell. Just wait and see!

Kwa upinzani gani huu wa kwetu wa CDM halmashauri 4 zilizofanya vibaya mno nchini zinaongozwa na upinzani tuwaamini kwa lipi?
 
Hivi upinzani msimamo wao ni upi? Kuanza kumkumbuka Kikwete mapema hivi ni kujichimbia kaburi.

Msigwa kuanza kumsifia Kikwete bungeni inanipa picha kuwa upinzani unakufa mbele ya Magufuli. Mnashindwa kujenga hoja, mangapi Kikwete mlimsema leo tena mnamkumbuka. Upinzani ovyo kabisa hamna msimamo. Acha CCM watuongoze tu

Ukweli unatabia moja,haufi!

"Mimi nasikitishwa na jambo moja, tumefika hapa kutokana udhaifu wa Rais Kikwete, uzembe wa bunge na wabunge na tumefika hapa kutokana na upuuzi wa CCM, nasema hivi nina ushahidi.” Mnyika (2012)

Ni kweli si dhambi kuanza kumsifia JK lakini kwa jinsi walivyomkataa JK leo wanamkumbuka. Ni unafiki.
Kichwa cha habari na ulichokiandika haviendani. Haujaonesha kwa kina nini hasa umesifia ilitupime maudhui ya mada yako.
 
Mimi siamini kuwa Kikwete hakufanya jambo hata moja vizuri. Inawezekana kuna aliyoyafanya vibaya lakini siyo sahihi kusema Kikwete hakufanya chochote kabisa.

Lakini pia ikumbukwe kuwa binadamu ana kawaida ya kuangalia yale ambayo yamefanyika vibaya, huyasahau yale mazuri mpaka ije siku ambapo atapatikana mwingine ambaye atafanya vibaya katika yale ambayo mwenzake alifanya vizuri.

Wabunge wengi wanailaumu serikali hii kwa kufifiisha mhimili wa Bunge. Wakati wa Kikwete hawakuwahi kufikiria kuwa kuna siku utakuja utawala ambao utazuia kuoneshwa Bunge, hawakufikiria kuwa Bunge litakuwa linaendeshwa na serikali. Wengi walitarajia kuwa serikali itakayokuja ingeongeza uhuru wa Bunge. Sahizi ndiyo wanagundua kuwa kumbe uhuru uliokuwepo wakati wa Kikwete ulikuwa ni mkubwa kuliko waliokuwa wanautazamia.

Huo ni udhaifu wa mhimili wenyewe. Ulianza kumomonyoka wakati wa Anna Makinda,ambaye aliudhofisha muhimili huo na kuwa weak kwa serikali sasa hata ni matunda (majuto huwa ni mjukuu).
 
Back
Top Bottom