Msigwa: IGP wa ajabu ivi kumkamata Lissu kwa uchochezi huwa analipotia polisi, ila kusema anatishiwa maisha hawahusiki

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA) Mchugaji Peter Msigwa amefunguka na kuonyesha kutoridhishwa na kauli ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Nyakoro Sirro kusema Tundu Lissu hakuwahi kutoa taarifa juu ya watu wanaomfuatilia.

Sirro%20.jpg

Mbunge Msingwa ambaye sasa yupo nchini Kenya kwenye matibabu ya Tundu Lissu ameonyesha kusikitiswa na taarifa hiyo ya IGP ambayo aliitoa Septemba 8, 2017 katika mkutano wa waandishi wa habari na kusema kiongozi huyo hakuwahi kutoa taarifa yoyote polisi juu ya gari ambalo lilikuwa likimfuatilia kabla ya kupatwa na shambulizi hilo la kupigwa risasi.

"Kamanda Sirro Ulitaka Lissu atoe taarifa gani zaidi? Sisi wengine ni wanasiasa, hatuna mafunzo ya kijeshi, Polisi wala Kikachero. Silaha yetu kubwa ni kipaza sauti (microphone), kazi yetu ni kupaza sauti , hoja inapaswa kujibiwa kwa hoja! Siyo kwa mabomu ya machozi, sio kwa virungu na bunduki. Inaonyesha jeshi letu la polisi uwezo wake mkubwa ni kupambana na vyama vya siasa hasa CHADEMA na CUF kuwalinda wakuu wa wilaya na mikoa" aliandika Mchungaji Msigwa

Aidha Msigwa anasema anaumia kuona Tundu Lissu akiteseka kwa ajili ya kutetea haki na Demokrasia ya taifa la Tanzania na kusema alichofanyiwa Tundu Lissu kinampa ujasiri wa kusonga mbele.

"Mungu anakataza kumwaga damu isiyo na hatia! machozi yanitoka kuona rafiki yangu Tundu Lissu akiteseka kwa kutetea haki na demokrasia ya taifa letu, amewakosea nini? Inanipa ujasiri wa kusonga mbele, sitanyamaza, tunakupenda Lissu wewe ndiye shujaa wetu" aliandika Msigwa
Note:

Akisema humkamata kwa uchochezi bila kwenda kutoa taarifa polisi, ila aliposema anafuatwa na kutishiwa hao hao polisi walingojea akaripoti kwao.
 
Na Sasa "wanawasaka" watu wasiojulikana japo sina hakika kama lisu baada ya kufanyiwa unyama ameripoti polisi.....sijui kwanini hawakufanya hivyo mwanzo kabla shida hii yote haijatokea.
 
hivi huwa kuna ugumu gani kufuata taratibu tulizojiwekea kuripoti matukio kwenye vyombo husika hata kama hatuna imani na vyombo vyetu?

nawaza tu pembeni ya kasha. kuna matendo yanatia shaka kutetea kila kitu.
 
@tundulisu ndiye shujaa wetu tumuombee afya njema ili wabaya wake waabike
 
Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA) Mchugaji Peter Msigwa amefunguka na kuonyesha kutoridhishwa na kauli ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Nyakoro Sirro kusema Tundu Lissu hakuwahi kutoa taarifa juu ya watu wanaomfuatilia.

Sirro%20.jpg

Mbunge Msingwa ambaye sasa yupo nchini Kenya kwenye matibabu ya Tundu Lissu ameonyesha kusikitiswa na taarifa hiyo ya IGP ambayo aliitoa Septemba 8, 2017 katika mkutano wa waandishi wa habari na kusema kiongozi huyo hakuwahi kutoa taarifa yoyote polisi juu ya gari ambalo lilikuwa likimfuatilia kabla ya kupatwa na shambulizi hilo la kupigwa risasi.

"Kamanda Sirro Ulitaka Lissu atoe taarifa gani zaidi? Sisi wengine ni wanasiasa, hatuna mafunzo ya kijeshi, Polisi wala Kikachero. Silaha yetu kubwa ni kipaza sauti (microphone), kazi yetu ni kupaza sauti , hoja inapaswa kujibiwa kwa hoja! Siyo kwa mabomu ya machozi, sio kwa virungu na bunduki. Inaonyesha jeshi letu la polisi uwezo wake mkubwa ni kupambana na vyama vya siasa hasa CHADEMA na CUF kuwalinda wakuu wa wilaya na mikoa" aliandika Mchungaji Msigwa

Aidha Msigwa anasema anaumia kuona Tundu Lissu akiteseka kwa ajili ya kutetea haki na Demokrasia ya taifa la Tanzania na kusema alichofanyiwa Tundu Lissu kinampa ujasiri wa kusonga mbele.

"Mungu anakataza kumwaga damu isiyo na hatia! machozi yanitoka kuona rafiki yangu Tundu Lissu akiteseka kwa kutetea haki na demokrasia ya taifa letu, amewakosea nini? Inanipa ujasiri wa kusonga mbele, sitanyamaza, tunakupenda Lissu wewe ndiye shujaa wetu" aliandika Msigwa
Note:

Akisema humkamata kwa uchochezi bila kwenda kutoa taarifa polisi, ila aliposema anafuatwa na kutishiwa hao hao polisi walingojea akaripoti kwao.
Mkuu Mhe. Msigwa umenena sawa kabisa. Kamanda Sirro na Kamanda wa mkoa wa Dodoma ingawa wote wanatoka taasisi moja, ningetegemea wangesimamia maadili ya kazi yanayofanana, lakini kwa ajili tu ya kulinda wachache na siyo nchi, viongozi hao wamepingana hadharani. Kamanda Sirro alisema; ingawa Mhe. Lissu alizungumza na waandishi wa habari lakini kwa taratibu za kipolisi hawakuweza kuifanyia kazi taarifa ile ya Mhe. Lissu kwa kuwa hakwenda kuripoti Kituo cha Polisi. Jamani maneno hayo kayatamka Kamanda Sirro. Kamanda Polisi mkoa Dodoma kamsikia Katibu Mkuu CDM akiongea na waandishi wa habari kama alivyofanya Mhe. Lissu. Jana Kamanda mkoa Dodoma ameyasikia maneno ya Masinji na kuyafanyia kazi. Kamtaka Katibu Mkuu aende akatoe maelezo kwa DPP. Ikiwa Lissu aliyeongea na waandishi wa habari hakusikilizwa inakuwaje Masinji ambaye naye kaongea na waandishi wa habari akasikilizwa na kumfuatilia kwa kumtaka Masinji akatoe maelezo kwa DPP !!! Police Force kama taasisi ina double standards.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hivi huwa kuna ugumu gani kufuata taratibu tulizojiwekea kuripoti matukio kwenye vyombo husika hata kama hatuna imani na vyombo vyetu?

nawaza tu pembeni ya kasha. kuna matendo yanatia shaka kutetea kila kitu.

Hivi wewe ukisikia na kuthibitisha kuwa mwenyekiti wa mtaa wako anatongoza mkeo utapeleka mashitaka hayo kwake?
 
Back
Top Bottom