Uchaguzi 2020 Msigwa hana personal Attack japo hana mvuto ana hoja za msingi zimejibiwa kwa hoja na kwa kina

Nigrastratatract

JF-Expert Member
Sep 4, 2019
456
1,000
NIMEMSIKILIZA SANA MSIGWA NA HOJA ZAKE ZA KUTAPATAPA ALIPOONGEA NA WAANDISHI WA HABARI AKITANGAZA NIA YAKE YA KUGOMBEA URAIS 2020.

Nashukuru kuwa ameanza kwa kutambua jitihada za serikali ya CCM kuwa kuna mambo yamefanywa na CCM, japo kwa kubeza. Hii inadhihirisha ile kauli ya mmbunge Mmoja aliyesema kuwa wakiwa peke yao wanamsifia Rais Magufuli, ila wakiwa majukwaani wanawahadaa Watanzania. Anasema CCM imekuwa ikitamba kuwa imeleta maendeleo kwa Wanzania.

Ni kweli kuwa Serikali ya CCM ina mambo mengi ya kujitamba hasa serikali hii ya awamu ya 5 chini ya Rais #Magufuli.

Anasema CCM imekuwa ikitatua kero ambazo si maendeleo. Nasikitika kwa kuwa Mch Msigwa hajui hata maana ya Maendeleo. Na hajui namna gani maendeleo yanahusiana na kero. Labda Msigwa hajui kero ni nini. Umaskini ni kero, kutokuwepo kwa miundombinu ni kero, kutokuwepo kwa umeme ni kero, kutokuwepo shule ni kero. Sasa yeye alitaka serikali isiyafanye haya. Serikali inayafanya haya anasema serikali haileti maendeleo. Hana nia njema na maendeleo ya Tanzania hii ambayo Rais Maguful anaijenga kwa jitihada zote. Anataka watu wasipatw maji, umeme, miundombinu ya usafiri, hataki watu wapate elimu, hataki watu wapate huduma nzuri za afya.

Ameenda mbali zaidi na kusema kuwa Serikali iko busy kuliko business. Hii si kweli, watanzania tunajua wazi namna gani serikali imejikita kutatua matatizo na kuleta maendeleo makubwa sana kwa Watanzania. Mch. Msigwa ni kipofu. Watanzania wanajua kuwa U-busy wa Serikali ya CCM imepelekea yafuatayo japo nitayataja kwa uchache tu:
1. Makusanyo ya serikali kuongezeka mpaka Trilion 26.13 Tsh ambayo sawa na 93.2% ya lengo. Je, haya si maendeleo?

2. Ukuaji wa makusanyo ya TRA kwa 13.6% je, si maendeleo?

3. Umeme vijijini. Kutoka vijiji 2118 mwaka 2015 hadi vijiji 9112 Aprili 2020 kati ya vijiji elfu 12. Je, hayo si maendeleo?

3. Serikali imekuwa ikigharimia elimu kwa ngazi ya shule za msingi na sekondari. Mikopo kwa wakati vyuo vikuu.

4. U-busy wa serikali ya CCM ndio uliofanya hadi sasa ionekane kuwa ni nchi ya 10 kwa uchumi Barani Afrika kati ya nchi 54.( Nomino GDD USD Billions 61.032, Nomino GDP/per capital income USD 1,172.8. Je, haya si maendeleo?

5. Kuongezeka kwa pato la ndani kwa ongezeko la 69.1%

6. Ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo Reli (SGR). Barabara zilizojengwa tangu 2015 zenye jumla ya urefu KM 2624.27. Upanuzi na ujenzi wa Bandari ili kukuza uchumi. Je hayo si maendeleo?

7. Ununuzi wa ndege sambamba na ujenzi wa viwanja vya ndege. Hadi sasa serikali imeshanunua ndege 8. Kabla ya Mwaka kuisha nyingine zinakuja. Mch.Msigwa anasema ndege hazina msaada wowote kwa Tanzania. Huyu ni kipofu wa kupindukia wa kifikra hata kwa kuona. Kama Mtu wa dunia hii hajui umuhimu wa njia za anga hadi leo ana matatizo tena makubwa ya kiakili. Hafai kiwa Rais. Huwezi ongelea ukuaji wa uwekezaji, biashara, mahusiano ya kimataifa n.k bila kuboresha usafiri wa anga. Mch Msigwa anataka watalii, mazao ya mashambani na hata wawekezaji, wafanyabiashara wasafiri kwa basi kutoka ulaya kuja Tanzania. Msigwa wa Ajabu sana. Basi tumsamehw huyo ndiye mtia nia.

8. Nenda kwenye madini na maeneo mengine yote ambayo sijayataja hapo. Kwa kweli ni mambo mengi hadi siwezi kuyasema yote kwa sasa. Kwa miaka mingi serikali imekuwa hainufaiki vya kutosha kwenye sekta hii. Hadi tulipodikia sasa Watanzania wanajua. Hawa ndio walitutisha eti nchi itashtakiwa. Sasa aibu imetanda kwao.

Anasema ukuaji wa uchumi hauna uhusiano na maendeleo. Msigwa anakuwa kama haishi Tanzania. Serikali ya awamu ya tano imeleta mabadiliko makubwa sana kwenye uchumi kama nilivyofafanua hapo juu. Wanzania tutakupotezea tu Mch. Msigwa.

Kuhusiana na deni laTaifa. Hakuna nchi ambayo haikopi hapa Duniani. Kikubwa unaangalia uhimilivu wake. Hata nchi Tajiri tuniani zinakopa. Msigwa hajaangalia hata mataifa mengine. Ukiangalia hakuna nchi hapa duniani ambayo inaifikia Marekani kwa deni la Taifa. Ndilo Taifa lenye deni kubwa duniani kuliko nchi yoyote.

Mch. Msigwa anaenda kuwa aibu kwa CHADEMA, anaongea mambo ambayo yana sifa hizi: no concreteness, immeasurable, not feasible and no inspirational value.

Anguko la CHADEMA linajidhihirisha hata katika yale waongeayo. Wamechanganyikiwa. Hakuna ajenda zinazoeleweka kwa Watanzania. #Magufuli kamaliza zote.

Toleo linalokuja nitachambua vipaumbele vyake ambavyo ameviongelea kama sehemu ya mambo ambayo anajitamba. Hadi aibu. Ni Aibu sana kuongea na kuahidi kuwa utawafanyia watu vitu ambavyo hata ndani ya chama mmeshindwa. Je, nchi mtaiweza?


#hapakazituu
 

Munambefu

JF-Expert Member
Jun 24, 2012
1,178
2,000
Mkuu hiyo mikopo ya Elimu ya juu unayosena inatolewa kwa wakati ni asilimia ngapi ya wanafunzi wanapata ukilinganisha na 2015 kurudi nyuma?
Mathalani nimesoma enzi za JK ambapo mikopo ilikuwa karibu Kila fani,leo kuna Watu wanasoma zile fani ambazo enzi za JK zilikuwa zinapewa grants kabisa lakini hawana hata mkopo kwenye awamu hii.

Elimu bure msingi na sekondari lazima tuangalie pia ubora wa hiyo Elimu sio suala la bure tu.Kijijini kwangu kuna primary Imebidi wazazi wajichange ili wapatikane waalim wa kujaza nafasi.

Awamu ya tano Imefanya mengi Kama zilivo na nyingine lakini Madhaifu yapo pia ubaya ni kwamba mtu akionesha kuna udhaifu pahali fulani anaonekana adui,sio mzalendo nk
 

Pilitoni

JF-Expert Member
Jul 11, 2011
1,118
1,500
Hatutaki maneno kila mtu anaweza kuongea,tunataka vitendo vitendo vitendo. T2020JPM ndio namba inayosomeka kwa sasa Hayo maneno wawapelekee wake zao wakaimarishe ndoa zao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom