Himidini
JF-Expert Member
- May 8, 2013
- 5,534
- 4,190
Ukweli unabaki pale pale.. Hapa duniani hakuna mtaalamu wa ndoa.
Kuna wanaooana kwa mapenzi.. ndoa zinawashinda
Kuna wanaooana kwa mapenzi.. ndoa zinadumu
Kuna wanaooana bila mapenzi... ndoa zinawashinda
Kuna wanaooana bila mapenzi.. ndoa zinadumu
Kuna wanaoendana tabia kama mapacha.. ndoa zinawashinda
Kuna wasioendana kabisaaaaa.. ndoa zinadumu
Kuna wanaoishi kwa mazoea.. ndoa zinadumu
Kuna ambao hata hawajui kwanini walioana.. ndoa zinadumu!
Kuna wanaochunguzana miaka kumi.. ndoa zinawashinda
Kuna ambao hawaoani kabisa.. wanaishi tu.. miaka nenda rudi hawana tatizo.. wako happy
Kuna wanaokutana na kuoana ndani ya miezi miwili.. ndoa zinadumu.....nakadhalika.. nakadhalika.
AND VICE VERSA
Bottom line:
1. Kama unataka kuoa/olewa fanya hivyo pale utakapohamua. Kama hutaki/hujaamua ACHA.
2. Kama uko kwenye ndoa, live each day as it comes. Enjoy the moment
3. Kama ndoa yako ina amani, mshukuru Mungu wako.. usiseme ni kwasababu nilifanya hivi.. au nilifanya vile..
4. Ukioa/olewa ishi the best way unavyojua wewe. The end will justify the means
5. Mwisho, kumbuka ndoa ni ARTIFICIAL sio natural. Naturally, binadamu hauko wired kuishi na mtu mwingine for the rest of your life.
^^
Well said
^^