Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,259
- 20,914
Leo ni jumapili karibu asilimia kubwa ya walioko kwenye mahusiano yoyote watakutana leo
Hebu kwa wale mnaokutana leo jaribuni kujiuliza hili:
Hivi mapenzi tu ndo ynatosha kutufanya mimi na wewe kuoana?
Binafsi kuna kitu nimejifunza kwenye haya mambo
Watu wanaoana kwakuwa wana hisia hizi
Kila mmoja kwa mwenzake lakini baada ya muda wanaachana au wanaishi kwenye ndoa ya kimazoea tu huku kila mmoja akiwa na mahusiano nje
Kwanini?
FIKRA ZANGU KUHUSU HILI:
Mapenzi ni hisia tu kuna wakati zinatoweka na hapa zinapotoweka ndipo matatizo huanza,mimi nadhani inatakiwa watu kabla hawajaoana wanatakiwa wawe na kigezo zaidi ya hiki
Ndoa ni mahusiano ya maisha yote sio kipindi fulani tu hivyo unapoamua kuoana na mtu ni bora ukajiuliza kuhusu maisha yako yote yaliyobakia kuanzia hapo unapofunga ndoa
Mimi nadhani kuna jambo la muhimu,nalo ni mtazamo wa kila mmoja kuhusu maisha zaidi,hapa kunakuwa na mambo mengi sana kama vile malengo ya kimaisha,mazingira,familia na zaidi imani za wahusika n.k
Hua inafikia mahali wanandoa wanakuwa hawaitaji tena mapenzi kwa wenza wao kama kiunganishi kilikuwa ni hicho tu mahusiano yao yanayumba na kunakuwa na ufa mkubwa sana baina yao
Ni muhimu kuwe na zaidi ya kitu kimoja kinachowaunganisha,na kitu hiki kinatakiwa kisiwe ca muda mfupi,mapenzi yamekuwa kama ni kigezo cha mtu kuoana,lakini nyakati za mababu zetu walitazama mambo mengi sana
Kuna bibi mmoja aliniambia wakati anachumbiwa wale wapelelezi walikuja kukagua kama anaweza kufanya kazi[kulima],ana heshima,anajua kupika n.k
Nyakati hizi ni kama mapenzi hayakuwa kigezo na watu walizeeka wakiwa kwenye ndoa
Hebu jaribuni kujiuliza hili!!!!!!!!!