Msichana wa kazi (housegirl) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msichana wa kazi (housegirl)

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Purity1, Aug 7, 2011.

 1. P

  Purity1 Member

  #1
  Aug 7, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 15
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wanajamii, naomba kuuliza wapi anaweza kupatikana msichana wa kazi za ndani (housegirl/housemaid). mfanyakazi aliyepo anakaribia kumaliza mkataba wake na ameamua kutoendelea na mkataba kwa sababu anataka kuanza maisha mengine. amekaa miaka takribani minne na sababu ya kutoendelea na mkataba ni genuine kabisa

  maelezo mafupi kuhusu mwajiri:
  1. mwajiri anaishi Dar maeneo ya Boko,
  2. Nyumba ni ya mke na mume- wote wanafanya kazi
  3. kuna watoto wawili- mmoja miaka 6 na mwingine miaka 4 - watoto wanaenda shule asubuhi saa moja na nusu na kurudi nyumbani saa 9 na nusu alasiri; Mke anatarajiwa kujifungua mtoto mwingine baadae mwaka huu au mapema mwakani (Mungu amjalie)
  4. nyumba ni floor moja (siyo ya ghorofa);
  5. kuna houseboy anayefanya kazi za kusafisha mazingira ya nje na garden ndogo iliyopo. hakai kwa mwajiri - anakuja na kuondoka
  kazi anazotakiwa kufanya
  1. kusafisha nyumba ikiwemo kudeki na kusafisha madirisha
  2. kufua nguo hasa za watoto (houseboy anasaidia kazi hii marambili kwa wiki)
  3. kupiga pasi hasa za watoto (houseboy anasaidia kazi hii mara moja kwa wiki)
  4. kupika chakula
  5. Kulea watoto ikiwa ni kuhakikisha wanakula, wanaoga na kulala vizuri
  6. Mungu akijali mke akajifungua baadae mwaka huu au mapema mwakani, atahusika kulea mtoto mdogo ikiwa ni pamoja na kumlisha na kuhakikisha anakuwa katika hali ya usafi na huduma nyingine anazotakiwa kupewa mtoto
  7. kuhakikisha usalama wa nyumba (ikiwa na maana ahakikishe hatoki nyumbani bila sababu ya msingi wakati baba na mama wapo kazini (nyumba ina security wire)
  8. kuwakumbusha watoto kufanya homework pale wazazi wanapokuwa hawajarudi kutoka kazini
  Sifa za mfanyakazi
  1. awe mchapa kazi
  2. msichana mwenye umri unaomruhusu kufanya kazi kisheria
  3. awe mwaminifu na asiwe mwizi
  4. Awe muwazi na kumueleza mwajiri masuala yote muhimu mazuri na mabaya (ili hatua muafaka ichukuliwe)
  5. ajiheshimu na asiwe malaya
  6. Awe na mdhamini mmoja mwenye makazi na anuani inayoeleweka
  7. awe na upendo kwa watoto (watoto nao wamefundishwa kumpenda dada anayewalea)
  mshahara na marupurupu
  1. Mshahara wa mwezi ni Tsh 50,000 kianzio
  2. Atapata bonus ya miezi miwili (100,000) kwa kila mwaka anaokaa na itatolewa mwisho wa mwaka - asipotimiza mwaka hatapewa
  3. Atapata matiibabu bure
  4. Atapata chakula bure
  5. Atapata malazi (accomodation) ya bure (ataishi nyumbani kwa mwajiri)- atapewa chumba kilicho na kitanda
  6. Atakuwa anapewa bure vitu vyote vitakavyomwezesha kuwa katika hali ya usafi mfano sabuni, mafuta ya kupakaa, mswaki, nguo, n.k.
  7. Likizo ambapo atapewa nauli ya basi ya kwenda na kurudi nyumbani kwao. wakati wa kwenda likizo atapewa zawadi za kupeleka nyumbani kwa wazazi wake
  8. Akikaa muda usiopungua miaka 4 atapewa bonus ya kusomeshwa ufundi wowote atakaotaka ili umumsaidie huko mbeleni baada ya kumaliza mkataba
  kwa kuzingatia hali hii, kama kuna mtu mwenye taarifa wapi naweza kupata msichana wa kazi naomba ani-PM au aniandikie email jitihada@live.com
   
 2. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #2
  Aug 7, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,249
  Likes Received: 3,836
  Trophy Points: 280
  Hata mimi natafuta mkuu
  Mshaara 450,000/= kulala,kula na matibabu kwangu!

  Sifa: awe amemaliza f4,awe na cozi ya computer
  Kazi: mtoto mmoja tu sina nia ya kuongeza kabisa mtoto!
  Mahali: Dar

  Aliyetayari ani pm
   
 3. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  chukua gazeti la nipashe kuna job agent yupo sinza atakupatia maid
   
 4. u

  ureni JF-Expert Member

  #4
  Aug 8, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,272
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Mkuu umejieleza vizuri sana,vipi kuhusu NSSF utampatia pia?manake kwa mujibu wa sheria ilitakiwa apate.Halafu huyo house boy wakati wa mchana wakati nyie mmeenda kazini hawatakuwa mke na mme?


   
 5. P

  Purity1 Member

  #5
  Aug 8, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 15
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ureni Ahsante kwa ushauri nitauzingatia na nitatafuta mtalaamu wa sheria na HR anisaidie katika hilo na mengineyo yanayohusu ajira (so suala linalohusu sheria na haki za mfanyakazi tuliachie hapo); baada ya hilo basi naomba msaada wa taarifa wapi naweza kupata huyo mfanyakazi.

  nakushukuru New Mzalendo nitajitahidi kufuatilia gazeti la NIPASHE ila kama una namba zaohao jamaa wa Sinza naomba unisaidie!
   
 6. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #6
  Aug 8, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  labda mwenye contacts za recruitment agents wa house workers amsaidie
   
 7. miss msemakweli

  miss msemakweli Member

  #7
  Aug 8, 2011
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  piga no 0715404790 huyu kaka anao houg. from Tanga
   
 8. tama

  tama JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 604
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Jamani huo mshahara na marupupu ni ya kweli au ni maneno tu!!!!!
   
 9. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #9
  Aug 10, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  mimi nadhani mhusika atakuwa anamaanisha.. TAMA kwani hiyo hela 50K unaona nyingi? anyway mwenye kujua wapi jamaa anaweza kupata amsaidie
   
 10. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #10
  Aug 10, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,015
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280
  Hii kwa mabeki 3 wa IR wanafaa zaidi.
   
 11. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #11
  Aug 11, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Je wa kutoka Tanga na Mara vipi? sifa zao?
   
 12. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #12
  Aug 14, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Purity1 msichana umepata?
   
 13. P

  Prisila Member

  #13
  Sep 1, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Mkuu kna huyu bint atakufaa anatafuta kazi za ndani mtafute kwa namba hizi 0752916620
   
 14. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #14
  Sep 1, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Mh! Matangazo Weka na Bei zake anazotaka
   
Loading...