Msichana kanipenda lakini yupo na kigogo

Msichana kanipenda lakini yupo na kigogo

Bak byzo I.T

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2014
Posts
266
Reaction score
126
Msichana nampenda na yeye ananipenda sana ila baada ya kutongoza na kuwa nae kipindi cha takribani mwezi mmoja hivi.

Ameamua kuniambia ukweli kuwa chanzo cha yeye kupata kazi TANESCO ni baada ya kutembea na kiongozi wa pale.

Na tetesi zinasemwa kuwa yule kiongozi ana VVU na mie nishaanza kuweka malengo na huyu mwanamke.

Nitafanyaje?
 
Nendeni mkapime
Muoe
Mtafutie kazi sehemu nyingine
 
We jamaa niaje asee,we muulize kati yako na kigogo nani atakuwa spare tyre akikupa jibu njoo nikushauri.
 
Nendeni mkapime
Muoe
Mtafutie kazi sehemu nyingine

kama yeye pengine hana kazi atamtafutiaje huyo mwenzie kazi? yeye awe mpole kwani ni kawaida sana siku hizi ukiwa na mkeo ofisini lazima tu utabanduliwa. wewe unadhani wanaume wanaowaoa wanawake wakiwa kazini kisha wanawaachisha kazi na kuwafungulia biashara au miradi majumbani mwao ni wajinga? watu wanaona mbali mkuu.
 
kama yeye pengine hana kazi atamtafutiaje huyo mwenzie kazi? yeye awe mpole kwani ni kawaida sana siku hizi ukiwa na mkeo ofisini lazima tu utabanduliwa. wewe unadhani wanaume wanaowaoa wanawake wakiwa kazini kisha wanawaachisha kazi na kuwafungulia biashara au miradi majumbani mwao ni wajinga? watu wanaona mbali mkuu.

Umeongea kitu kile kile nilichomaanisha nilipoandika amtafutie kazi sehemu nyingine..

Halafu..ni kweli maofisini kuna usaliti,lakini sio lazima kama ulivyotilia mkazo.
 
Demu nampenda na yeye ananipenda sana ila baada ya kutongoza na kuwa nae kipindi cha takribani mwezi mmoja hivi..

Ameamua kuniambia ukweli kuwa chanzo cha yeye kupata kazi tanesco ni baada ya kutembea na kiongozi wa pale.

Na tetesi zinasemwa kuwa yule kiongozi ana VVU. Na mie nishaanza kuweka malengo na huyu mwanamke.

Nitafanyaje??

Hizo tetezi umezipata wapi? je ni za uhakika? au ni watu wasiopenda kuona wewe una hicho kiburudisho. nakushauri tuliza akili then taratibu fanya reseach
usije kumpoteza laaziz wako kwa kusikiza maneno ya nyumbu
 
Suala hili ni la kukaa pamoja na kuongea. Ufumbuzi ni lahisi kama Mtachanganya akili zenu.
 
Huyo anakudanganya ili uogope uachane naye! Anaona unambana ye anataka kutanua na hilo sugar daddy.
Hivyo anajua ukishajua kigogo ana ukimwi huwezi msogelea tena binti.
 
Siyo rahis sana mtu kukuambia ishu kama hyo..especially akiwa anakupenda..
Atakuwa anakupima..
Nendeni mkapime afya zenu then kama mko serious na mnapendana kweli past z nothng to worry abt.
 
Back
Top Bottom