Msichana huyu bado namtaka, nifanyaje?

Msichana huyu bado namtaka, nifanyaje?

Hatutaweza kamwe kuwaelewa wanaume!!!
Mwenzio kuumwa ndo unamtafutia mke mwenzake, hebu vaa hiyo kofia wewe halafu usikie uchungu wake, badala ya kumfariji unatafuta wa pili??? Au unafikiri yeye hakuwa na X wa kumfuata!! Acha uvulana kaa na mkeo
Ushauri huo
 
Hatutaweza kamwe kuwaelewa wanaume!!!
Mwenzio kuumwa ndo unamtafutia mke mwenzake, hebu vaa hiyo kofia wewe halafu usikie uchungu wake, badala ya kumfariji unatafuta wa pili??? Au unafikiri yeye hakuwa na X wa kumfuata!! Acha uvulana kaa na mkeo
Haoni hata haya mbio mbio kaja huku kufungua uzi. Wavulana wana mambo hawa.
 
Mpeni ushauri mwanaume mwenzenu. Imeshakuwa kawaida yenu mada ikimuhusu mwanaume mnaanza kutoa kasoro weee.

Ila ingekuwa ya mdada hapo huu uzi ungeshajaa.
Kwani kasema anataka ushauri kutokwa kwa wanaume tu?!


Mbona ww cha kwanza umemtoa kasoro badala ya kumpa ushauri.
 
Hahahaa, sicheki kwa mzuri aisee

Eti mliwekeana kiapo cha kutofanyaje?...halafu ukaamua kufanyaje vile....

Tena umefikia mpaka level ya kuoa mwengine na nina hakika huyo uliyemuoa asingepata matatizo ya kiafya basi wala usingemkumbuka huyo X wako.

NB:
- Mke kuwa na tatizo la kiafya, je mmeshajaribu kutafuta tiba mpaka kuambiwa kwamba tatizo lake haliwezi pona hata afanyaje?. Kama jibu ni ndio unaweza enedelea kuoa mke mwengine (ila si kwa kumlazimisha X wako maana ni kweli ulishaonyesha hukuwa na nia nae na ulifikia hatua ukamdharau)

- Mara nyingine Mungu huwaepusha waja wake na mambo ambayo wao wenyewe hawayajui. Huenda huyo X alyepushwa na jambo toka kwako, au wewe uliyepushwa na jambo toka kwa huyo X. Tafakari hilo pia na lifanyie kazi

Kila la kheri katika kutafuta mke wa pili...likifanikiwa hilo, tafadhali usimuache wala kumnyanyasa huyo mke uliyenae mwenye tatizo la kiafya
 
Back
Top Bottom