Msichana huyu bado namtaka, nifanyaje?

immasakha

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
489
281
Nilipendana na msichana tangia tukiwa kidato cha kwanza, uhusiano uliendelea mpaka nilipofika kidato cha sita wakati tukiwa katika mahusiano hakuna kitu chochote cha mapenzi tulichowahi kukifanya.

Wakati nikiwa kidato cha sita ashki za kutaka kufanya nae mapenzi yule msichana ilinijawa kiasi kwamba nilikubali kumfanyia kitendo chochote ili siku moja anipe mapenzi lakini jitihada zangu ziligonga mwamba nikaamua bora hata niachane nae, niliona ninafuga ng'ombe lakini maziwa sipati, kimya kilitawala katika mahusiano hayo kiasi kwamba kila mmoja aliamua kuishi kivyake.

Mara baada ya mwaka mmoja wa ukimya ule mimi nilitumia busara ya kutafuta mawasiliano yako mpaka ni pale nilipoyapata lakini kwa bahati mbaya aliniambia hana shida ya kuwasilina na mimi na namba yako akatoa amri ya kwamba nifute katika simu yangu lakini nilishindwa kutekeleza amri ya kufuta namba yake.

Mara nikakutana na msichana mwingine nikafanya maongezi nae na siku chache nikatangaza kufunga nae ndoa, yule mdada baada ya kusikia kwamba ninataka kufunga ndoa alinitafuta kutwa mara 5 lakini nikaamua kumkaushia mpk nilipo funga ndao yangu.

Kwa bahati mbaya mke wangu kapata tatizo la kiafya hawezi kutoa baadhi ya huduma katika ndoa, lakini baada ya kuona dini yangu inaruhusu kuongeza mke nikaamua kumtafuta yule msichana na hataki kabisa hata kuonana na mimi na jibu lake la mwisho ameniambia kwamba sikua na shida nae hapo mwanzo nije niwe na shida nae leo.

NB: Tuliwahi kulishana kiapo kwa mujibu wa dini yetu ya kwamba hatutoachana.

Je! Nifanye nini wakati yule msichana bado ninamtaka?
 
16465648_1726125371032438_6478344041527246848_n.jpg
Una tamaa sana aisee kama panya vile
 
Hatutaweza kamwe kuwaelewa wanaume!!!
Mwenzio kuumwa ndo unamtafutia mke mwenzake, hebu vaa hiyo kofia wewe halafu usikie uchungu wake, badala ya kumfariji unatafuta wa pili??? Au unafikiri yeye hakuwa na X wa kumfuata!! Acha uvulana kaa na mkeo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom