Msichana amkana mpenzi wake

Msichana amkana mpenzi wake

Tamalisa

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2015
Posts
2,542
Reaction score
907
Habari wakuu,

Vijana wanaume jifunze kitu hapa, yamkini hata na wewe siku yakakutokea, haijalishi hata kama umewahi kuona mkasa kama huu we tulia tu, wengine watajifunza.Hii ni serious ilimtokea kaka yangu. alimpenda mdada miaka michache iliyopita, alimpenda na dada akasema pia

Anampenda walipendana sana kaka yangu alijitoa kwa kila nanma kwa huyu dada, ambaye kwao ni kijijini huko Kigoma,siku moja yule binti akasafiri kwenda kwao kwa lengo tu kuwaambia wazazi rasmi zaidi ili mipango ianze kuelekea ndoa.

Kufika kwao sijui yule binti ilikuaje, gafla kamkana my kaka kabisa na live akasema sikutaki tena kaka yangu akabembeleza sana hadi akakata tamaa, wazazi wa binti ndio walikuwa chanzo cha haya japo zawadi zote alizopewa
binti awapelekee wazazi walizipokea.

Nikamwambia kaka achana nae na ukubali ukweli unaouona ndio hivyo. akatulia na maisha yakaendelea. baada ya kama mwaka hivi yule binti alikuja kwa spidi kali sana akiomba radhi, jamani wakaka hapa ndio pa kujifunza msiwe wepesi sana kurudiana na binti katika mazingira kama haya, chunguza kwa undani kwanza.

Nilimwambia kaka msamehe ila usimrudie, akaelewa, baada ya muda tukajua kumbe yule binti kwao wachawi noma, kaka alishukuru sana. akatulia katika maombi na Mungu akampatia mke wa ukweli ana 6 yrs katika ndoa na maisha ya furaha.

Binti naye akaolewa na katika harusi tulienda maana tulialikwa nakumbuka nilikaa siti moja na kaka akimuangalia binti ndani ya shela, badae binti mimba zikawa zinaharibika tukapata tetesi kuwa bibi
anachuka watoto kafara.

Wakaka kuweni na maamuzi ya moja kwa moja pindi ufanyapo maamuzi hasa katika hili suala la kuoa, binti akikukataa kwa jeuri akirudi usiwe mwepesi kumpokea,si kwamba nawaponda wanawake wenzangu, no ila unatakiwa kuwa mwangalifu tu.

Kinyume chake kwa wanawake.Mungu awabariki na kwa wale wanaotafuta wenza wa maisha (sio michepuko) nawatakia mafanikio mema muwaone wa kwenu na si wa rafiki zenu.
 
Aise hii bonge la funzo kwa vijana wetu asante mkuu
 
Ushauri unafaa kwa wadada pia, maana nao wakati mwingine wanakuwa wahanga katika mahusiano na wakaka wasiojielewa, anamuacha msichana ambaye wameweka makubaliano, upande aliotegemea ukiwa sio anarudi tena kwa yule wa kwanza. Wadada nanyi kuweni waangalifu kwa wakaka kama hao.
 
watu mna imani za ajabu...yaani mdada akipata miscarriage ni bibi anachukua watoto kafara!! Wee mkeo atapata miscarriage umpeleke kwa mganga badala ya hospital...elimika!

ndugu yangu iyo sio imani, ndo uhalisia huo.......
 
Last edited by a moderator:
Jamani acheni tu mimi nilikuwa namsupport sana girl wangu tukiahidiana kuoana ikiwa namlipia baadhi ya gharama za chakula na matumizi baadae akanikataa live niliumia sana kwani hata kwenda Chuo nilifacilitate mimi mara baada ya miezi mitatu akabadilika nikipiga cm hapokei ila ananiomba vocha hanipigii simu akawa ananijibu ovyo ila ckukata tamaa mpaka akaniacha matokeo yake mara baada ya mwaka na nusu akaja kwangu huwezi amini alimaliza chuo akapigika sana akawa ananishawishi mpaka kesho na now niko na kazi nzuri kipato kizuri na anahangaika hajapa ajira mwaka wa tatu sasa kweli wadada hawaaminiki jamani. Kafulia ubishoo kwisha
 
Laana hizo! unamkataaje mtu bila sababu? tatizo hawa dada zetu msimamo "F" na wengi ni "oppotunists" akishampata mtoa fedha lazima akutafutie sababu za kukutosa anasahau kabisaa! Be careful laana sio lazima itoke kwa mzazi...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom