Msichana ajirusha kutoka ghorofa la saba

kabla hujapenda,jiweke tayari kwa lolote na ukabiliane nalo kwa namna yeyote ila si kutoa uhai wako ambao Mungu amekupa utimize kusudi kubwa ulilolitegemea.
 
yani kama sababu ni malovee ..ni bora arudishwe juu ajirushe tena tuu..uupuuzi maridhawa
 
Dar...Inategemea na aina ya mpenzi...Kuna elimu bure...kilimo kwanza...:D:D:D:D:D:D
ha haha yote hayaniui mwenzio .. nilishapendaga wakati huo kama chizi hadi alikuwa ananipa mapenzi ya kimkataba siku niliyofunguka na kumpa kibuti duh moyo ukawa butu na kuahimshiamapenzi kwenye pesa
 
Dar es Salaam. Msichana Redna Raphael (19) jana alinusurika kifo baada ya kujirusha kutoka ghorofa ya saba katika jengo la Harbour View Tower, maarufu J.M. Mall lililopo katika makutano ya Mtaa wa Samora na Barabara ya Morogoro, jijini Dar es Salaam.

Redna ambaye ni mfanyakazi wa Kampuni ya Usangu Logistics Ltd yenye ofisi zake ndani ya jengo hilo, inadaiwa alichukua uamuzi huo muda mfupi baada ya kuzungmza na simu ya mtu ambaye bado hajafahamika wanahusiana vipi.

Hata hivyo, binti huyo alinusurika baada ya kuangukia kwenye moja ya mabomba yanayotoa moshi kwenye jenereta ya jengo hilo, lililopo ghorofa ya kwanza ambako walinzi wa jengo hilo walimuokoa.

Meneja wa Kampuni hiyo ya Usangu, Mazar Dadkarim alisema wakati tukio likitokea hakuwapo ofisini, bali alipatiwa taarifa na wafanyakazi wenzake waliokuwa ofisini.

Da!! siku hizi wanawake ni majasiri mnoooo! ile ya kunywa sumu haipo tena.
 
Back
Top Bottom