Msichana ajirusha kutoka ghorofa la saba

benghlasis

Member
Nov 29, 2016
49
125
Dar es Salaam. Msichana Redna Raphael (19) jana alinusurika kifo baada ya kujirusha kutoka ghorofa ya saba katika jengo la Harbour View Tower, maarufu J.M. Mall lililopo katika makutano ya Mtaa wa Samora na Barabara ya Morogoro, jijini Dar es Salaam.

Redna ambaye ni mfanyakazi wa Kampuni ya Usangu Logistics Ltd yenye ofisi zake ndani ya jengo hilo, inadaiwa alichukua uamuzi huo muda mfupi baada ya kuzungmza na simu ya mtu ambaye bado hajafahamika wanahusiana vipi.

Hata hivyo, binti huyo alinusurika baada ya kuangukia kwenye moja ya mabomba yanayotoa moshi kwenye jenereta ya jengo hilo, lililopo ghorofa ya kwanza ambako walinzi wa jengo hilo walimuokoa.

Meneja wa Kampuni hiyo ya Usangu, Mazar Dadkarim alisema wakati tukio likitokea hakuwapo ofisini, bali alipatiwa taarifa na wafanyakazi wenzake waliokuwa ofisini.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom