Mwili wa bilionea ambaye alikuwa anaendeshwa na dereva kwenye gari la V8, nyumbani hadi ofisini ni full ac. Ulinzi wa kutosha ili asiguswe hovyo hovyo...mmhhh lakini leo hata hao wanaoulilia hawezi kukaa naye zaidi ya masaa 36 tu,
Leo kaburi lake linachibwa na nzengo tena kuna,hiyo inaonesha koleo lililomchimbia masikini wa mwisho leo linamchibia bilionea..hapo ndio Mungu katupa usawa wa kila binadamu na ni fumbo kubwa.
Leo anashushwa kwenye saduku lilifugwa kila sehem na hakuna hata hewa ya kupita..yuko peke yake...
Aliondoka kapanda first class,lakini leo amebebanishwa na mizigo kama...
Kweli kifo kipo na kina mambo yake
Lakini pamoja na yote hayo bado katika uhai wake alikuwa anakula na wasikini,walemavu wa akili, vilema, na aliwafanya watu wanyonge kuwa wenye furaha... Ameacha kitu moyoni mwa watu..
R.i.p Mengi