Msiba mkubwa: Adam Lusekelo Mwakang'ata

Msiba mkubwa: Adam Lusekelo Mwakang'ata

Kwa ukweli hii ya Adam imenigusa sana, kwa wale wenzangu na mie ilikuwa kununua Sunday News na kukimbilia kwenye column yake. Kwa mara ya kwanza nilikutana naye nje ya Tanzania kama mara tatu hivi, na mara zote nilikuwa nakumbuka makala zake alizokuwa anaandika na baadaye kuzifuatilia kwenye mtandao kila ninapopata nafasi. Hata wale maadui zake walisoma kile ambacho ameandika. Natumaini sisi kama binadamu ni lazima tukubali hapa tunapita tu safari yetu bado ni ndefu. Rambi rambi zangu kwa Familia yake pamoja na ndugu na jamaa. Pumnzika kwa amani na mwenyezi mungu airehemu roho yako.
 
Utakumbukwa na Watanzania wengi kama mzalendo wa kweli, mwema mwenye upendo.

Kiuandishi, utakumbukwa na idadi kiduchu ya Watanzania wanaoelewa Sundays News.

Saluti.
 
Oh Kweli duniani tunapita. Nakumbuka miaka 2001 akiendesha kipindi cha Mgongano wa Mawazo, ITV.
 
MWANDISHI mahiri nchini, Adam Lusekelo (54), amefariki dunia usiku wa kuamkia jana wakati alipokuwa anakimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa matibabu, mke wa marehemu Scolastica Lusekelo amebainisha jana.

Alisema afya ya marehemu ilidhoofu usiku wa juzi na waliamua kumpeleka hospitali ya Aga Khan, lakini nao walikata shauri na kumhamishia Muhimbili na mauti ilimfika akiwa njiani kupelekwa hospitali hiyo ya rufaa.

“Oh, no! Tumempoteza kipenzi cha wasomaji wa gazeti la ‘Sunday News’,” alisema kwa masikitiko Mhariri Ichikaeli Maro mara baada ya kupokea taarifa za kifo cha Lusekelo.

Lusekelo atakumbukwa na wasomaji wa magazeti ya serikali ya Sunday News alikokuwa akichangia kwenye safu ya A Light Touch na HabariLeo kwenye safu ya Chombezo la Lusekelo.

Safu zake zilikuwa na utofauti kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuandika masuala muhimu ya kitaifa kwa lugha laini, jambo ambalo liligusa mioyo na nafsi za wapenzi wake.

“Mume wangu atapungukiwa na kitu kwa sababu alikuwa mpenzi sana wa safu ya Lusekelo,” alisema Joyce Sabuni, mfanyakazi wa Tanzania Standard Newspapers (TSN) inayochapisha magazeti ya DAILY NEWS, SUNDAY NEWS, HABARILEO na HABARILEO Jumapili, katika kitengo cha usambazaji.

Kaimu Mhariri Mtendaji wa TNS, Mkumbwa Ally ni miongoni mwa watu walioguswa na msiba wa kifo cha mwandishi huyo mkongwe aliyekuwa na kipaji cha hali ya juu katika fani ya uandishi wa habari.

Kaka wa marehemu, Ben Mwakang’ata alisema mipango ya mazishi inafanywa nyumbani kwake Ubungo na kuwa upo uwezekano mwili wa marehemu ukasafirishwa kesho kuelekea Rungwe, mkoani Mbeya.

Marehemu Lusekelo ameacha mke na watoto watatu, wakiwemo wawili wa kike.

Katika uhai wake alifanya kazi TSN kwa muda mfupi katika miaka ya 1980 kabla ya kujiunga na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kama mwandishi wa habari akiandikia akiwa Dar es Salaam.

HabariLeo | Adam Lusekelo afariki dunia
 
Almighty God rest his soul in eternal peace .....
 
NDUGU ZANGU,


NIMEPOKEA KWA MASIKITIKO MAKUBWA HABARI ZA MSIBA WA NDUGU YETU KATIKA MAPAMBANO, ADAM LUSEKELO MWAKANG’ATA. NIMEMEANZA KUMSOMA ADAM TANGU NIKIWA TAMBAZA SEKONDARI MIAKA YA 80. ADAM LUSEKELO NI KAKA YANGU KATIKA UANDISHI, NI KAKA WA WENGI.


KUPITIA KAZI ZAKE, KWANGU MIMI, KWA NAMNA YAKE, ADAM LUSEKELO AMEKUWA AKIFANYA KAZI YA KUAMSHA FIKRA ZA WATANZANIA ILI WAIFANYE WENYEWE KAZI YA KUJIKOMBOA KIFIKRA. ALIIFANYA KAZI HIYO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU TANGU ENZI ZA MFUMO WA CHAMA KIMOJA.


ADAM AMEWASAIDIA WATANZANIA WENGI KUJIBU SWALI WANALOJIULIZA LAKINI MAJIBU YAKE WANAPEWA NA WASIOTAKA SWALI HILO LIULIZWE, TENA KWA KUKIMBILIA KULIJIBU KABLA YA UMMA HAUJATAFAKARI NA KUTOA JIBU. SWALI NI HILI; NI NANI ADUI WA UMMA?


TUNAJUA, KUWA KATIKA KUIFANYA KAZI YAKE, KUNA AMBAO WALIMCHUKIA ADAM KWA KAZI YAKE YA KUWAAMSHA WATANZANIA KUTOKA USINGIZINI.


ADAM AMEONDOKA, LAKINI, BILA SHAKA, MOYONI ALIAMINI, KUWA AMEACHA WENGI WA KUIENDELEZA KAZI YAKE. NDIO, ADAM LUSEKELO AMEONDOKA WAKATI WATANZANIA WAKIWA KATIKA HATUA ZA MWISHO ZA KUJIKOMBOA KIFIKRA.


ADAM LUSEKELO ATAENDELEA KUISHI, ATAKUMBUKWA NA WENGI.


MAGGID MJENGWA,


IRINGA


JUMAMOSI, APRILI, 2, 2011


http://mjengwa.blogspot.com



( Chini ni moja ya kazi za Adam Lusekelo zilizo kwenye maktaba yangu. Ni kazi iliyobeba ujumbe mzito)
 
Sasa hii habani ni ya kweli? maana kama ni kweli, we have lost a great thinker:angry:
 
Aisee....dah....

RIP mpiganaji.....jamaa nilikuwa namkubali sana!!
 
Maggid
Asante kuileta hii kwenye jikwaa letu adhimu.
Adam amekuwa na style yake ya pekee ya kuandika as if he was jocking lakini ukimsoma in between the lines, ndipo unaupata ujumbe uliomo ndani yake.

Mara baada ya kutoka TSJ kituo changu cha kwanza nilishukia Daily News ya enzi hizo na ndipo nilipomfahamu Adam zaidi ya kumsoma maandishi yake. Jamaa ni kichwa.

Miaka ya 1997 Adam aliwahi kuwa mpinzani wangu mimi nikiendesha 'Kiti Moto' na yeye akiendesha "Malumbano ya Hoja" vipindi vyote vikiruka ITV. Upinzani uliishia kwenye kipindi tuu huku nje tukiwa wamoja kwenye viti virefu vya mviringo na hatuondoki mpaka muda wa kufunga ...

Adam ni mpiganaji wa kweli mpaka siku za mwisho mwisho, popote utakapo mkuta iwe ni Steers ya pale mjini , Mzalendo au Samaki Samaki pale Mlimani City amekuwa bennet na laptop yake akipiga kazi 'with a light torch'.

Poleni Daily News,
Poleni Watanzania
RIP ADAM LUSEKELO!.
 
Mungu amlaze mahala pema na awape faraja mkewe, watoto na familia yake yote kwa msiba mkubwa walioupata. Amen
 
R.I.P. Adam; your contribution to the fight against fisadis through your SATIRE will greatly be missed.
 
Ana mke alioko hai mkuu kama story invyosema. Alafu alikufa na kisukari.
Hapo pekundu, unajuaje kama mkewe bado yupo hai.

Vipi amefariki na ugonjwa gani?..kiswahili kigumu sana, na maanisha nini sababu ya kifo chake? na je kuna lolote la kujifunza kutokana na sababu ya kifo chake.

RIP Adam
 
Just wishing this was a 1st April joke?
With a Light Touch; R.I.P. Adam Lusekelo, may the Almighty rest his soul in Eternal peace!
 
sidhani kama uwongo.....
kuna mtu alikutana nae majuzi alikuwa sooo weak hata kujaza form za benki alikuwa hawezi jaza anaandikiwa....he was sooo sooo ill...baadhi walisema alikuwa na NGOMA......ila ana shori mkali kweli kweli anasukuma bonge la ndinga town hapa......

Hakuna sababu ya kuleta habari za kukisia kilichomuua. Hiyo unayoita ngoma haina nafasi kwa wakati huu, waache wanafamilia wa marehemu wamlilie ndugu yao kwa amani.
Ifike wakati wa kukomaa kimawazo, hakuna sababu ya maana ya kuleta neno ngoma hapa. Ukitaka unaweza kuanzisha thread yako ujadili hiyo ngoma. hapa tunataka kukumbuka ujasiri wa Adam wa kuweza kumkemea karibu kila mtu aliyevurunda katika uongozi.
 
Rest in peace my friend....I'll miss you a lot. Scolastika na watoto poleni kwa msiba huu mkubwa.
977.gif
 
Back
Top Bottom